DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Diwani wa Kata ya Swaya katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Shaban Saleh Nduta, ametangaza rasmi kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) tarehe 11 Juni 2025, akitoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Akizungumza mbele ya umati wa wananchi na viongozi wa chama, Nduta amesema uamuzi wake umetokana na kuvutiwa na utendaji wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, hususan katika kuimarisha maendeleo ya wananchi, kulinda amani na kusimamia haki kwa vitendo.
Nduta ameongeza kuwa sera na mwelekeo wa serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia umeonesha dhamira ya dhati ya kuwaletea Watanzania maendeleo shirikishi. Amesisitiza kuwa sasa ni muda wa kushirikiana kwa pamoja kuiunga mkono serikali ili kuhakikisha jitihada zinazofanywa zinazaa matunda kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Wananchi waliohudhuria hafla hiyo walipongeza hatua hiyo, wakisema ni ishara ya kuamini dira ya Rais Samia katika kujenga Tanzania ya kisasa na jumuishi.
Source: Manara Tv