Rupia: Hazina ya Mjerumani

Rupia: Hazina ya Mjerumani

Sasa hapa napingana na mshana anavyosema hakuna ulinzi wowote kule bali shimo likiwa halina watu hua wadudu hukaa, sasa nataka kujua huyo mdada naye anafanyaje huko kama sio kweli kwamba hawa wajerumani wamelinda mali zao kichawi?

Nawasilisha
Rudia kumsoma tena Mshana Jr
utaelewa...
 
Mbona Sasa Tunakufa Maskin Nawaka Upo Embu Fanya Makeke Twende Huko

Mshana Jr Atatupa Elim Zaid

Cc: Mshana Jr
Hai avae.... unajua kuna vitu unapima kipi bora kwako na kuangalia "stakes" zilizopo, kwa iyo ngoja tufanye mengine kwanza.

Ila mshana anaeza akakomaa apate "maji" sa cjui huwa ni maji ya nn?
 
Step ya kwanza: nenda kahakikishe kweli kuna pango lenye zege? kisha mlikague jinsi lilivyo, mlango ulipo, mandhari ikoje.

Step ya pili: Ukishajiridhisha rudini na team yako, anzeni kuchambua madhara ya sehemu hiyo kutokana na mazingira yake..... hii itawasaidia kujua namna mtakavoingia kwa kujilinda.

Step ya tatu: Mkishajua namna na kujipanga, hapa mnapanga kwenda kuchunguza ndani.... step hii mjiandae kisaikolojia zaidi mkiwa na vitu vya kujikinga na madhara, pia muwe tayari kurudi na chochote, hivyo jiandaeni na vibebeo kabisa(kumbuka step hii ni ukaguzi wandani)

Step ya nne: Mmeshajua ndani kuna nn(yawezekana hakuna kitu, vimeshabebwa) lakni kama vipo muwe mnajua kilichopo ni nini, hivyo mmejipanga kubeba, taa za chemli zinazowaka bila mafuta, pasi za dhahabu ambazo haziwekwi mkaa, vikombe vya dhahabu.... sarafu, manwe kukuta buti(sema hapa zitakuwa zimeshaharibika na kuwa km bigijii)au bunduki na masanduku ya unga wa baruti, hizi acganeni zazo kwa kuwa ni rahisi kukamatwa nazo..... lkn km una mtu unaeza muuzia, chukua.

Kwa step hizo, mko tayar kuwa matajiri.... pangeni safari fasta.

ANGALIZO: kuna mitego mingi sana, ukiachilia ya kichawi, kuna.mitego ya gesi chafu(wataalamu wanazijua kwa majina) hizi ni pale umekuta kikombe maridadi cha dhahabu( hasa mwanzoni mwanzoni mnapoingia) halafu ww unakibeba kwa pupa kumbe limetegeshwa na unapokitoa unategua kitu kinachoatoa hiyo gesi.... hivyo MNAKUFA MNAJIONA kabla ya kusonga mbele, inaweza kuwa sehem yamepangwa mawe, mkaondoa moja tu, lkn hilo ndo limebeba uzito wa mengine yaliyopangwa kiustadi yatakayopelekea kuporomosha mengine yatakayoziba njia mliyoingilia(MNAKUFA MNAJIONA)

Kwa hiyo mnapaswa kuwa makini sana kugusa vitu msvyovijua kwa kuwa mpo kwenye hatua ya uchunguzi, pia hakikisheni mna kamera yenye flash, taa zenye mwanga mweupe, na diary ili kunote kila mnachokiona.
Du unanikumbusha mtiririko wa Movie inaitwa THE MUMMY iliyochezwa Egypt kwenye pyramids za Giza!
 
Sawa mkuu Storyteller nimekuelewa ila nimemuelewa mshana jr zaidi kwa sababu miaka ya nyuma mapadre wa kizungu walikua hawakauki katika makanisa ya vijiji vya jirani vinavyo zunguka milima hii lakn sku hzi hawapo kabisa wameacha nyumba zao tu na masista hukaa humo,Hii inaniamisha kwamba wamekomba kila kitu .Ila nitajitahd nifke kilele cha huu mlima nipate hata picha na mandhar ya huko.
 
Ni kweli kuna baadhi ya maeneo, ila kwa Wazee watu na hata sie Vijan bado hatujaweza kupata njia ya kuzitoa kwa sababu si rahisi sana kufahamu kilichomo ndani ya Shimo, andaki au Kavazi!
ii) kulingana naMila zetu ni Vigumu sana kutambua na kuzindua "Zindiko" la Mtu aliyefariki!
 
Sawa mkuu Storyteller nimekuelewa ila nimemuelewa mshana jr zaidi kwa sababu miaka ya nyuma mapadre wa kizungu walikua hawakauki katika makanisa ya vijiji vya jirani vinavyo zunguka milima hii lakn sku hzi hawapo kabisa wameacha nyumba zao tu na masista hukaa humo,Hii inaniamisha kwamba wamekomba kila kitu .Ila nitajitahd nifke kilele cha huu mlima nipate hata picha na mandhar ya huko.
Kumbe walishabeba vyao vyote basi.
 
Hiki kitu kipo nawala sikwamba kunauongo wala nni?,utakuta maeneo hayo huwa kuna mawe mawili hadi matatu na katikati ya hayo mawe kuna kapango hapo ssa utakuta kuna cement kali sna pia katika hayo mawe utaona kuna michoro mitatu ya rangi hapa (wao wanajua inamaana gani),ila ssa mkisema mfukuwe pale mtafanikiwa kuondoa hiyo zege ya cement na mkimaliza mtaona shimo mkiingia ktk shimo hilo mtakuta tena michoro ambayo inaendana na ile ya awali na hapo ssa mtakutana na zege tena ya cement ila ssa hapo ndo mauza uza yapo ndo wengi wanawafata waganga na waganga wanachemka sna mpaka mnaona hii kazi ni ngumu mnapaacha kama ilivyo.watanielewa watu ambao wameona hizi mambo,ukitaka kuamini tunaanza mwanza,mahina,kangae,kuna watu walikufa kufatilia hizi mambo kalibu na msikiti,mpanda kuna mlima unaitwa ibhasa kutoka senta moja inaitwa center maria nyuma yake kuna mlima unaitwa mlima ibhasa.kwa maoni ushauri kalibuni sna
 
Mwaka 2009 nilipata kibarua ya mda pale ngorongoro, nikazoeana na mwenyeji mmoja wa pale ingawa yeye si mzaliwa wa hapo... Siku moja akanipa wazo tupande mlima moja mrefu ulio pembezoni mwa creta, akanipa data kidogo kuwa wakati wa vita vya pili wajerumani walitumia mlima huo km chimbo lao. Chini ya huo mlima kuna mashamba na majengo yao ambayo yapo hadi leo.... Tulipanda huo mlima tukiwa tumebeba lunch box zetu, tulipofika karibu na kilele tulipita kati ya miamba fulani tukaona maganda ya risasi na vichupa vidogo vya soda vikiwa vimepoteza sura. Tulifika mahali juu kidogo tukakuta kidimbwi ikiwa imezungukwa na miti mikubwa. Mojawapo ilikuwa na kitu kikiwa kimefungwa na mnyororo ambao umezama ndani ya mti yaani mti umekua nao ukameza mnyororo. Tulicheki tukaona ni kisanduku kina kofuli ilopata kutu na kuzeeka sana... Tuliamua tujaribu kuitoa ghafla ukaja upepo tukajikuta tuko chini ya mlima nyuma ya shule fulani ya msingi, hatukuwa na ujanja tukarudi kambini. Baada km wiki mbili tukaazimia kurudi na vifaa ili tushushe lile sanduku... Tulipofika hapo ile tumegusa ule mti mi nikajikuta niko barabara fulani inayoenda kijiji fulani inaitwa endulen, sikujua mwenzangu yuko wapi, nilijaribu kumpigia cm yake ikawa haipatikani. Nikarudi kambini jioni lakini jamaa bado hayupo hadi siku ya pili ndo akapatikana kwenye cm. Akanijibu amejikuta yuko wilaya jirani ya karatu ilimbidi apande basi ili arudi kazini... Tulikoma kwakweli. Miaka chache tena baadae 2014 kuna mzee fulani mwenyeji wa manyara akaniambia nimsaidie kutafuta soko la mali zake fulani ambazo alichimbua ktk pori kilomita kadhaa mashariki mwa hoteli ya ndutu kule Serengeti. Akaeleza kuwa aliona kitu km msingi wa nyumba kimesakafiwa ktk bonde waliamua kivunja ili waone kuna nini. Walifanikiwa kutoa sanduku lakini ghafla akatoka shimoni joka kubwa aina ya chatu akapanda juu ya hilo sanduku. Wakaamua wachukue kondoo moja km kafara kwa joka hilo, baadae likarudi shimoni na wao wakachukua sanduku hilo. Wakafika mahali ikabidi walivunje wakakuta bunduki 2, mawe yanayon'gaa km kilo 3, mikufu 2, binocular 2, nguo za khaki, pesa za rupia sarafu 52 imeandikwa tabora pound, na vitu vidogo vidogo. Bunduki waliamua wazichimbie ardhin, na vingine wakaweka ndani mfuko afu wakachimbia ndani ya boma la tajiri wao wa ngombe... Mwaka ukapita afu yeye akarudi kwao manyara. Baadae yule mwenye boma akawa amemtuma kijanake kumweleza huyu mzee aje aondoe vitu hivo kwake kwasababu vinaleta vitisho vya radi kila siku. Niliposikia hayo nikapatana nae aende mtu wangu moja ili walete, soko si tatizo. Baada ya wiki niliandaa safari yao walipokaribia ile nyumba ghafla mzee akawa km hajielewi anaongea mwenyewe hataki mtu karibu yake. Jamaa akanipigia cm, nikamwambia urudi nae, eti wakati wa kurudi ile wenge imepotea yuko sawa. Na yeye anashangaa mbona tunarudi walikotoka awali? Ikabidi tutemane na hiyo mambo coz kila utakalogusa lina mauzauza....... Simshauri mtu afuatilie hizi mali coz unaweza ukajikuta we ni mganga wa kienyeji au ni mchawi
 
Hayo mambo naweza sema kwamba cjui yapo au la!!! Ukienda morogoro kuna sehemu inaitwa kasanga milimani huko, kuna jamaa walifuatilia shimo moja hivi, kwanza walikutana na mabomu, wengi walikufa, na alama kubwa hawa jamaa inavyosemekana hutoboa tobo kwenye mti mkubwa, unaweza shangaaa ukaenda polini ukaona mti una tobo kubwa la majabu sana, na wao walichagua miti ambayo hata ikikauka huchukua miaka minginkuoza mfano mpingo, muanga na nk. Alama nyingine walitumia mianzi(bamboo) sasa ile bamboo huenea eneo kubwa sana watu wanashindwa kujua mali ipo wapi.
Mawe nayo yametumika sana, unaweza ukakatiza polini ukakuta jiwe km lina michoro, hapo ndipo tunaposemaga kuna mawe ya ajabu, kumbe mambo hayo yachorwa/kuchonga na mtu
 
Nakuja na hii kitu na ntawatafuta wanaojua hizo sehemu tukasake mali hizo
105cfbe0e5661a0e7e7396fb6b620a37.jpg
 
Back
Top Bottom