Rupia: Hazina ya Mjerumani

Kwanza soma historia vizuri usituletee hadithi za kubuni hapa. Wajerumani waliondoka baada ya WW I. Wakati huo mwalimu Nyerere alikuwa bado hajazaliwa.

Ni kweli Wajerumani waliondolewa ghafla baada ya kushindwa vita na League of Nations ambayo ndiyo Umoja wa Mataifa wa sasa ilikabidhi Tanganyika katika utawala wa Mwingereza kama guardian.
 
Watu wametapeliwa sana Mpwapwa, Lushoto na Tanga kwa hizi stori za wajerumani. Sasa hata kama waliacha rupia, hizo pesa zitakuwa na thamani gani wakati nchi yenyewe siyo ile ya wakati ule?
 
Sky eclat anachosema huyu jamaa kipo kuna watu wanakesha milimani kutafuta hizo mali
 
WEWE NYERERE ALIWATIMUA WAJERUMANI MWAKA GANI? SI BORA HATA UNGEMTAJA KINJEKITILE NGWALE?

UJERUMANI WALITIMULIWA 1919 BAADA YA KUSHNDWA VITA YA KWANZA YA DUNIA NA KUONEKANA NDIYE CHANZO CHA VITA, BASI LEAGUE OF NATIONS PAMOJA NA MAMBO MENGNE IKAAMURU MJERUMANI KUACHIA MAKOLONI YAKE YOTE YAWE CHINI YA UANGALIZI WA LEAGUE OF NATIONS, AMBAPO MWINGEREZA ALIKABIDHIWA JUKUMU HILO KWA UPANDE WA TANGANYIKA NA MAKOLONI MENGINE.

NYERERE AMEZALIWA 1922.

NYERERE ALIWAFUKUZA WAHINDI BAADA YA UHURU.
 
AmekalilishwA halafu na yy anapanda jukwaani anaanza kutupa habari za uongo mwambie asome kwanza huyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi ni issue za utapeli mtupu! Nakumbuka kuna kipindi nilikuwa wilaya ya Liwale akanijia mtu mmoja ambaye kwa sasa ni ni muigizaji ktk FUTUHI akanieleza kuhusu sanduku lililopo milimani na lina amana hizo. Aliniomba nitoe pesa kwa ajili ya kwenda kufanya kafara ili waweze kulifikia sanduku, machale yakanicheza nikawa mgumu kutoa pesa akasepa!
 
upo vizuri upstairs..... yaani kuanzia elimu ya sayansi... historia... na maisha kwa ujumla congrats
 
Niliwahi shuhudia jamaa mmoja aliyesanukia kaburi lenye mali za wajerumani mkoa fulani hapa Tanzania akifa na kukauka kama mti wa mpingo..ama kwa hakika ilinisikitisha sana! Inasemekana jamaa wameacha kafara za kufa mtu katika mali hizo kiasi kwamba kama huna nguvu huwezi chukua! Hii ndio tofauti kati ya uchawi mweupe na mweusi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…