storyteller ungetupa kidogo uzoefu wako
Kiukweli mm bado sina uhakika kama yapo kwasababu BINAFSI sijafuatilia kiundani na sikutilia maanani kwa kuwa kuna mengine kama hayakuniingia akilini(niliona ni mepesi sana), ILA ninachofahamu hadi sasa kuna eneo nilienda kulingana na maelezo niliyopewa nikakuta kuna dalili za hiyo kitu.
ILIKUWAJE:
Nilivoulizia zile alama ktk mawe kule mwanza(mawe mengi yana alama za michoro km chokaa, mfano alama ya jiwe ambalo maji yalikua yakitiririka kupitia hapo kisha yakakauka)..... Maelezo nlopewa yaliendana na hicho
mshana jr alichosema, ila jamaa alikua na ushahidi zaidi, kwa kuwa alinifundisha maana ya alama zote kuanzia hiyo michoro ya chokaa, aina ya miti, mchanga.... na alinipitisha ktk maeneo yote yaliyo karibu ili kuona mifano halisi.
Kwa ufukunyunyu wangu siku moja nikaenda mbali sana huko nyegezi af unapanda huko ndani ndani. Nikachagua moja ya alama na kuanza kufatilia kadri alivyonieleza..... nikakuta kuna mahali kuna jiwe(ama zege hivi) kama limeegeshwa...... nilipologonga.... ulitoka mlio mithili kuna uwazi kwa chini....sikufatilia zaidi ya hapo kwa kuwa nilijawa hofu........ ila ipo siku nitakwenda na team tukafanye mambo.
Maeneo yenye hizi mambo mengine unakuta ni kambi za jeshi, na kwa maelezo ya jamaa waliofanikiwa kupata hazina hii ni wajeda wakubwa tu(haiwekwi wazi) ingawa wao walitumia njia rahisi ya kununua maji(au mafuta) toka kwa familia za kijerumani zinazojua maswala haya(hii ni kwa mujibu wa maelezo ya jamaa).
Masharti ya kuingia maeneo haya.
1. Usisex wala kujielekeza sana na mawazo ya sex kwa muda usiopungua miezi6(maana yake uwe masafi(pure), kuna uwezekano ukiwa bikra unafanikiwa zaidi) pia usiwe na mawazo ya chuki, hasira.
2. Ukiwa eneo hili hamtakiwi kula kula(kama ni kula mkalie mbali huko)
3. Usiende kwa mganga kwa nia ya kudhuru(wapo waganga wanaoelewa hilo na wanajua namna ya kuwashauri)
4. Mnapoenda, msiwe na mawazo ya kidhuluma(yani km ni mgawo, uwe sawa sawa kama mlivokubaliana)
5. Uwe jasiri, vile vitu unapokutana navyo ni vitisho tu, havidhuru, mtu anadhurika kwa woga wake na panic, na pia utakapoogopa na kupiga kelele ndo mauza uza yanapozidi.
6.Msiwe waropokaji, hapa jamaa alisema utakaposema sema habar hizo kwa wasiohusika(kwamba mna mzigo) utakua unapotea potea....
7. Haitakiwi kelele, msiongee ongee, mnatakiwa kuweka akili yote katika jambo mnalofanya(ikiwezekana mjifunze kuwasiliana kwa ishara kabla hamjaingia)
Kikubwa hapa ni kuwa waangalifu kwa mazingira yanayokuzunguka, kuchunga hali ya hatari ili usidhurike na vitu halisi mfano nyoka, wanyama, wadudu na mawe kuporomoka.