kwa hisani ya chakarikamkopo. ( huyu bwana mara ya mwisho kuonekana hapa JF ni tarehe 23 July 2013)
Binafsi nimeshiriki sana kwenye hiyo biashara......kuna ukweli fulani lakini sehemu kubwa ni utapeli kwasababu ya ujinga na kukosa elimu kwa watu wengi. Watu wengi wanangaika kutafuta hivyo vitu lakini ultimately hakuna mtu anayemtaja mnunuzi wa uhakika...wanunuzi wote ni wa kufikirika.
Uzoefu wangu: NI kweli kuna hazina nyingi sana ambayo Wajerumani waliaacha Tz....wakati ule Msuya akiwa Waziri Mkuu katika ziara yake moja Ujereumani aliomba apewe ramani za sehemu ambazo wajerumani waliacha hazina ili zifukuliwe na zigawanywe. Jibu alilopewa ni kuwa hazina nyingi zilikuwa za watu binafsi wanaweza kushirikiana kwenye hazina za nchi ambazo nyingi zina vitu vya serikali....silaha, nk.
Hazina ya serikali pale Mbeya Tukuyu ipo jengo la mkuu wa wilaya...hata kwa macho ukiangalia ile ofisi imejengwa juu ya mlima wa kutengenezwa kule chini ni shimo kubwa sana. Mlango wa kuingilia upo ofisi ya afisa utamaduni wa wilaya. hata ukitembea kwenye ofisi utaona kuna hali ya kuonyesha chini kuna mtikisiko wa uwazi. Mlango mwingine nadhani uko nyumba aliyokuwa akiishi OCD. Miaka kumi iliyopita shirika la moja la Ujerumani waliomba kukarabati boma la mkuu wa wilaya na waliomba ukarabati uanzie ofisi ya utamaduni. Watu wakamshtua aliyekuwa RAS wa mkoa Mbeya (name withheld) akazuia ukarabati huo
Kule kijiji kwa akina Kapteni Komba kuna wageni wajerumani walichimba mashimbo kanisani na kwenye baadhi ya majengo ya kanisa hayo mashimo yalikuwepo hadi mwaka 2006 nilipopita hapo
Kuna kijiji kimoja cha akina Joyce Mhaville (wa ITV) nimekisahau kule Njombe baada ya Isoliwaya kabla hujafika Mfriga kuna binti wa kizungu alikuja kama kama volunteer akakaa baada ya miezi kadhaa akawaita wanakijiji wamsaidie kuchimba shimo fulani akawaambia mkifika sehemu ngumu muache ili nililete vifaa vingine usiku huo akaenda peke yake akachukua cha kuchukua asubuhi wakakuta shimo tupu na binti akatoweka hadi kesho.....sehemu inaitwa Lupembe
Kuna sehemu Mbeya inaitwa Ileya....pale kuna mzungu alikuwa tajiri sana yeye pia alificha mali zake jirani kabis na kanisa la Moravian hata alama za mawe alizoweka kuelekeza alipoficha mali zipo sema vile ni muda mfupi alama hizo zinapotea unapoingia kwenye vichaka. Baada ya kanisa la RC chini ya ''mtafutaji'' mashuhuri retired Afisa Usalama (name withheld) kushtukia hiyo dili waliamua kununua eneo lote hilo ili baadaye waanze kutafuta hizo mali wenyewe.
Kifupi ni kuwa Nyerere aliamua kujenga magereza, JKT, Shule sehemu zote ambazo alihisi kuna hazina ya madini au wajerumani waliaacha mali zao
The story goes on and on.................................