Rushwa hushamiri pale watu wanapocheleweshewa haki yao na kuanza kuitafuta kwa njia ya mkato

Rushwa hushamiri pale watu wanapocheleweshewa haki yao na kuanza kuitafuta kwa njia ya mkato

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Picha

JAJI Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma ameitaka Mahakama kuacha kuchelewesha haki kwani ndiyo chanzo kikubwa cha rushwa katika mhimili huo.

Profesa Juma alitoa kauli hiyo jijini hapa jana wakati akifungua Kongamano la Wadau wa Masuala Kupinga Rushwa Nchini lililoshirikisha vyombo mbalimbali vya utoaji haki nchini wakiwemo majaji, wasajili na mahakimu wa mahakama nchini.

Jaji Mkuu alisema rushwa hushamiri zaidi katika taasisi zinazochelewesha haki kwani watu wanaohitaji kupata haki zao kwa wakati unaokubaliwa wakikosa hulazimika kuitafuta haki hiyo kwa njia ya mkato.

Alisema rushwa inatajwa zaidi katika taasisi zinazohusika na utoaji wa haki hivyo akasema haipendezi na asingetamani kuwa chombo muhimu kama mhimili wa mahakamana ukiendelea kunyooshewa kidole kuhusu rushwa.

“Mapambano dhidi ya rushwa yanapaswa kuwa endelevu isiwe kwa sababu Takukuru yupo, bali yawe ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku katika taasisi zetu ili kuweza kufanikiwa kuishinda rushwa,”alisema.

Kwa mujibu Jaji Mkuu, uzoefu unaonesha kwamba rushwa haiwezi kumalizwa na mahakama pekee bali taasisi zote zinatakiwa kushirikiana ili kuongeza nguvu kwenye mapambano hayo.

Aliwaagiza watumishi wa mahakama waanze kujisafisha katika vita ya rushwa na lazima waanzie ndani ya mahakama wenyewe ndiyo wawe mstari wa mbele katika mapambano hayo na siyo kumtegemea mtu mwingine.

Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Wilbert Chuma alisema lengo la kongamano hilo ni kujadili hali ya rushwa katika vyombo vya utoaji haki nchini.

Wengine walioshiriki katika kongamano hilo ni pamoja na viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU) kwa pamoja wakilenga namna ya kuweka mfumo wa kuwasaidia wanyonge katika kupata haki zao
 
Back
Top Bottom