Wewe ni vipi, mbona unaficha wala rushwa?
Kuna Mwenyekiti anayeitwa Mdachi na Karani anayeitwa Kachenje ni wala rushwa mashuhuri pale Baraza la Ardhi na Nyumba - Arusha.
Mdachi alipata shida ya kupewa mkataba kwa miezi kadhaa, baada ya kupewa mkataba sasa anachukua rushwa kama njia ya kufidia mapengo aliyopata alipokuwa nje ya ofisi.
Kachenje anatumia uzoefu wake wa muda mrefu katika ofisi hiyo na sasa anakula rushwa mchana kweupe. Amekuwa na jeuri na kujibu vibaya wanaotaka huduma katika ofisi ile kama njia ya kutaka kupewa rushwa.
Baraza la Ardhi na Nyumba - Arusha ni kama halina uongozi kwa sababu kila mmoja pale anajifanyia kazi kama anavyotaka.
Ni wakati muafaka sasa kwa Mhe Lukuvi na Mhe Angelina Mabula kufuatilia na kuchukua hatua zinazostahili kwa watendaji hawa wala rushwa walio chini ya Wizara yao na kuharibu taswira nzuri ya Serikali ya awamu ya Tano.