Patriot
JF-Expert Member
- Feb 11, 2008
- 5,705
- 4,703
Nimeanza kuona watu wakitetea tatizo hili la rushwa kwa kusema lete ushahidi. Ukweli ni kwamba nafasi ya wajumbe wa CCM kuamua nani awe mgombea, inatumika vibaya sana!
Hawa ni watu ambao hawalipwi mshahara. Wakati wa uchaguzi hutegemea kipato toka kwa wgombea huu ni mtindo ambao umejionesha wazi kwamba, uchaguzi ndani ya chama hauleti mtu bora, bali ni sehemu ya kuchochea rushwa. Bahati mbaya sana baada ya wabunge, sasa tena madiwani wanapatikana kwa mtindo huo.
Viongoziwa kitaifa wanaweza kujifanya kutoona kwa kuwa tu tayari wanaowagombea ambao watatumika kuunda serikali, lakini hali ya Bungeni itakuweje? Ni salama kuamini siasa ni sehemu ya kupeana rushwa?
Kifuatacho, sisi ambao siyo wajumbe, nasi tutaomba kupewa chochote na bila hivyo, lazimisheni matokeo maana haiwezekani tupoteza muda kupitisha viongozi wenye uwezo mdogo kiasi hiki.