Rushwa kushinikiza Bandari ya Bagamoyo: Nani anatoa Pesa?

Mnayemuongelea ni mtu amefanya kazi mpaka mashirika ya kimataifa ukiacha kwamba amekuwa Waziri wa serikali yetu kwa muda plus Makamu wa Rais.

Ukiongelea hizi ishu za uwekezaji ana exposure kubwa kushinda wote humu mnaojinasibu kama wataalamu sana.

Nadhani yupo sahihi sana acheni wawekezaji waje, terms tutazinegotiate vizuri sababu mifano tumeshaona. Tusiwe na mawazo mgando
 
Tatizo liko private sekta kumiliki sehemu nyeti kama bandari ya nchi. Hizo sheria na taratibu unazosema ni changa la macho kwa sababu zinatu

Kumbe hakuna hata kitu kimoja unachokifahamu juu ya ujenzi wa bandari hiyo!!zaidi ya kumezeshwa hayo matango poli!!
Kwanza hiyo bandari sio kama ni bandari tu kama hizi zilizopo ukanda huu wote wa Africa, hivyo huwezi ijenga wewe kama wewe!!wachina wakijenga hiyo bandari na viwanda vingi hapo, mi jimeli mikubwa itakuwa inatoka china na kuleta bidhaa hadi hapo hapo sasa zinakuja meli ndogo ndio zinachukua mizigo hiyo hapo na kupeleka kwenye nchi zao badala ya kuzifuata china.sasa hapo ile hoja kuwa hutakiwi kuendeleza bandarini yoyote kwenye ukanda huo inatoka wapi?kwani majukumu ni tofauti.
Mkataba wake wa kuiendesha ni miaka 40, sasa hoja ya kuwa asipopata pesa yake ataichukua inatoka wapi?
Wakati huo kodi za serikali zote zinakusanywa.
Ukiwasikia wataalam wa mambo ya majini(marine) hiyo bandari ina manufaa sana, achana na wana siasa.na Kenya wanasubiria tu lishindikane hapa waitumie nafasi hiyo , halafu kama kawaida yetu (wazee wa nongwa)tuanze kuwaona wachawi wetu!!!
 
Hiyo bandari sio kama bandari hizi nyingine mkuu, elewa hilo kwanza, hii itakuwa ni EPZ, ambayo wachina watakuwa wanatengeneza baadhi ya bidhaa zao , na kuziuza duniani, na nyingine mi meli mikubwa itakuwa inaleta mizigo toka china, inashusha hapo wafanyabiashara wengine afrika ndio wanachukulia mizigo yao hapo , kwa sasa mchina karibia soko lote la afrika amelishika yeye, sasa ukimpa mrusi/mturuki hilo lengo litafikiwa?!!na hapa wazungu ndio watia fitina wakubwa!!
Serikali yetu ingekuwa na desturi za kuweka mambo hadharani, ingeweka tu wataalam wauchambue, then tuamue kuliko , hizi kila mtu ana lake.
 
Stupidity start with the concern of not knowing which direction to follow , then comes with the concept which concern to follow
 
Mifano ya China iko mingi sana si Afrika tu bali nchi nyingi za njaa njaa, wao lazima kwanza watangulize rushwa ya maana kwa watia signature hizo contracts zenyewe. Usitegemee yatakayokuwa hadharani na kudaiwa ndiyo terms yatakuwa halisia.
Bora Wazungu au Japanese au South Korea, hizo ni nchi zenye makampuni yenye uwezo kitaaluma na vifaa na mabenki makubwa yanaweza kuwekeza kwao(kwa companies zenye financial records nzuri).
Kuna nchi 'zinalia' kuingia 'cha kike' kwa Mchina mifano halisi ni jirani zetu wa Kenya na Zambia, si kwamba nchi hizo hazina wataalam wa kukagua mikataba bali wakati mnatiwa ndimu kunakuwa na watu wenu ambao inakuwa wameshadakishwa chao na hao ndiyo wanatumika 'kuwakarabati' nyinyi(sisi) na taifa kwa ujumla. Mchina haaminiki,ana rekodi chafu.
 
Mnasumbuliwa kukosa exposure!

Miradi mingi ya bandari za kisasa duniani inajengwa kwa utaratibu wa PPP na mafanikio ni makubwa!
Issue sio exposure hapa, muhimu hiyo mikataba iwekwe wazi, huko unamosema huyo PPP ilifanikiwa hawafichi mikataba kama mnavyofanya nyie.
 
We nani alikwambia kuwa kazi ya serikali ni kodi tu? Ulikaririshwa na mabeberu na naomba uende kwao uone kama beberu ka binafsi sha kila kitu .RIP jembe letu
 
Hizi fix zako umezitoa wapi?
 
Bandari ya Dar ni kama roho ya uchumi wa nchi, tukichomeka muwekezaji humo tunaweza kuja kujuta siku za usoni, tumeona madhara ya uwekezaji kwenye madini na viwanda tulivyo vibinafisha.

Tungejikita kujitegemeza wenyewe kwenye baadhi ya mambo hii ingetujengea kujiamini zaidi, hakuna kitu kibaya kama kujihisi hauwezi. Wantanzania tulishaanza kujiamini kwamba tunaweza, ila taratibu naona imani inaanza kutupungua.
 
Nawahakikishia..tunaweza tuka binafisisha reli zote, barabara zote, bandari zote n.k na nchi ikawa na mapato ya kutosha zaidi na ika imarika zaidi.
Tulijaribu kwa kubinafsisha reli (na mashirika mengine fulani) matokeo yake ikafa kabisa!
Asante Magufuli kwa kuifufua reli yetu.
 
Wenye mawazo mgando ya ujamaa hawawezi kuelewa kabisa haya mambo
 
Legacy ya ujamaa imeiganda nchi
 
Usichanganye Bandari,TRA na Benki kuu katika kapu moja.
 
Uko sahihi kabisa
 
Washamba wa kijamaa wanairudisha nyuma sana hii nchi
 
Serikali haitakiwi ishindane na wananchi wake katika biashara
We nani alikwambia kuwa kazi ya serikali ni kodi tu? Ulikaririshwa na mabeberu na naomba uende kwao uone kama beberu ka binafsi sha kila kitu .RIP jembe letu
 
Tutafute roho nyingine sita tuwe kama paka badala ya kutegemea roho moja tu.
 
Pesa ya rushwa itakuwa inatolewa na Kikwete na wabia wake wachina. Huo mradi ulikuwa ni white elephant yake aliyowaahidi wachina baada ya mtoto wa mfalme kudabwa na sembe, lazima atakuwa anafight ili kutimiza ahadi.
 
Reli haijawahi kubinafsishwa, UDA walipewa makada wa chama na viwanda vingi vilibinafsishwa kwa makada wakati vilikua vinaelekea kufa vikiwa mikononi mwa serikali
Tulijaribu kwa kubinafsisha reli (na mashirika mengine fulani) matokeo yake ikafa kabisa!
Asante Magufuli kwa kuifufua reli yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…