Milesmontego
New Member
- Jul 16, 2023
- 2
- 0
Katika miaka michache niliyowahi kufanya kazi katika jamii, nimegundua na kushuhudia namna WATENDAJI wa serikali wanavoihujumu serikali na nchi yao kwa kupokea rushwa.
Hili linajidhihirisha katika mikoa ya Tabora, Shinyanga na Simiyu ambapo watoto wengi huachishwa shule kwaajili ya kuchunga ng'ombe, kuoa au kuolewa na wakati huo mtendaji akipelekewa malamiko na walimu anagiza apelekewe majina ya wanafunzi watoro na kuwatoza wazazi wao faini ambayo haipo kweny maandishi na kuwaambia wazazi hamtosumbuliwa tena.
Wale ambao tunaishi mikoa hii tumeona wanafunzi wakianza 170 kidato cha kwanza na kumaliza 30, pia hata wale ambao wanapewa ujauzito suala hili likifika kwa mtendaji kata basi ni rushwa na kesi hufutwa katika matokeo ya mitihan katika mikoa hii unaweza ona wamefanya vizuri kumbe ni kwasababu wanafunzi wengi hawakufanya mitihani ,mifano mizuri kwenye hili ni shule nyingi za wilaya ya igunga na nzega katika wilaya hizi kila mtendaji wa kata naeletwa malengo yake makubwa ni kufatilia watoro kwa lengo la kujipatia kipato kwa njia ya rushwa.
Kwa hali hii wanafunzi wengi wa jamii ya kisuma hukosa haki yao ya elimu huku wazazi wakiwaambia siku hizi hakuna ajira ili kuwashawishi waache shule na wakati mwingine wakiwatishia kuwatenga kabisa lakini cha kushangaza wataalamu wetu wa usalama wakiongozwa na watendaji kata na madiwani wamekua wakiwa saidia wananchi ili wasikutane na sheria ,mfano diwani wa kata ya BUKOKO wilaya ya Igunga kuna siku alimgombeza mkuu wa shule ya BUKOKO SEKONDARI kwamba kwanini anapeleka majina mengi ya wanafunzi walioacha shule katika kikao cha kata huku akisema mimi nilishawaambia halmashauri sina watoro katika kata yangu huku mtendaji akisema wanafunzi ambao utoro wao ni kuanzia mwaka jana usiwajumuishe hivo abakishe wale watoro wa rejareja lakini wanafunzi walioacha wakiulizwa wanasema baba alishalipa kwenye ofisi ya kata. Uchafu huu unajidhihirisha pale ambapo mtu atafanikiwa kuangalia mfumo wa usajili wa wanafunzi kwenye shule husika ambapo wanafunzi wote walioacha shule majina yao yamesalia kidato cha pili na yamejilundika ya miaka mitatu, hivyo ni vigumu utawala wa serikali yetu kufikia malengo na maendeleo kama ndani ya serikali yenyewe kuna watendaji ambao hawana lengo zuri na wananchi wake. HEbu mtu afikiri tu mtoto akiwa nyumbani anaambiwa hakuna umuhimu wa kusoma wala hakuna ajira na anathibitishiwa kwamba ata viongozi tutaongea nao afu mwalimu amwambie mwanafunzi elimu ni ufunguo wa maisha na mwanafunzi anaona watoto wenzake wapo mtaani hakuna shida ni wazi kwamba siku mwanafunzi huyu akipata ugumu wowote atarudi mtaani ambako wazazi wanafurahi mtoto wao akiwepo.
Madiwani wao wamekua wakitetea utoro huu kwasababu ya kulinda kura kwa wananchi hii ni changamoto ambayo inatupasa kuitatua ili kuweza kujenga taifa la kesho lililo imara, huru na haki.
Kwangu mimi nadhani rushwa ni changamoto kubwa saana ambayo inaliyumbisha taifa la Tanzania kuanzia kwenye vijiji mpaka serikali kuu,hili ni tatzo ambalo kwanza kabisa TAKUKURU iajiri watumishi wenye weledi na serikali iwe yenye kufatilia mtiriko wa pesa kwa watumishi wake pia elimu yakutosha itolewe na sheria nzito na kali ipitishe kwa atakaekutwa hatia ya kula na kutoa rushwa ili kuwapatia haki zao hawa watoto.
Nimezungumzia saana rushwa hii ambayo inawanyima watoto haki yao ya msingi kwasababu vijana wa leo ndio taifa la kesho, natamani ningeambatanisha na video za watoto hawa wanavolamika kuwa wazazi wengine wanakataa hata kuwanunulia vifaa vya shule ili kuwafanya wakate tamaa na kuendelea na shule.Kiukweli kabisa ili kuwe na utawala bora ni lazima kwanza tutokomeze rushwa na tujenge kesho uliyo bora na ya haki.
Nashauri madiwani na matendaji kata wahimizwe kuwahimiza watoto kufika shuleni na kuwaeleza umuhimu wa shule, pia kuwaeleza wazazi umuhimu wa elimu na pia hawa viongozi wa serikali ndio wanatakiwa wawe mstari wa mbele kupinga rushwa katika jamii zao kwasababu wao pia ni vioo ambavyo jamii wanaitaza.
Kama serikali ingekua inafuatilia kwamba watoto hawa wanapotelea wapi nadhani wangekuja kugundua huu uozo ambao umeshamiri kwa kiasi kikubwa kwasababu wazazi wanajua nikiongea na mtendaji vizuri basi hata barua ya walimu ikifika hata nisipoitikia wito hakuna tatizo.
Pamoja na watendaji kuongoza kwenye rushwa inayowanyima watoto elimu pia kuna wakuu wa shule wanaokula njama na wazazi kuwakatisha watoto masomo ambapo mzazi anamfuata mkuu wa wa shule ili amuhamishe mtoto wake katika shule nyingine ambayo ipo mbali na mkuu wa shule anapokubali basi anawasiliana na mkuu wa shule mtoto anapotakiwa aende anampatia fedha kidogo na kumuambia huyu mkuu huku akikupigia simu muambie nafasi ipo hivo ahamishwe na baadae uhamisho ukikamilika yule mwanafunzi anaambiwa asiripoti shule husika hivyo mwanafunzi anakatisha masomo.
Kwa maelezo haya inaonyesha ni namna gani kunahitajika nguvu ya ziada kuleta mabadiliko ya kielimu katika mikoa ya Tabora Shinyanga na Simiyu, hii habari nimeandika kwa yale niliyoyashuhudia baada yakufika kwenye mikoa hii ambapo mzazi anatoa rushwa ili mtoto aache shule, anamshauri mtoto afanye vibaya kwenye mitihani hakika hiki ni kitu cha ajabu saana lakini ukweli ni kwamba kipo na bado kinaendelea kuwepo .
Mwisho kabisa ili kutokomeza hili serikali iajiri watumishi ambao wanapenda maendeleo ya Taifa sio ya ubinasi, watumishi ambao watatanguliza mbele maslahi mapana ya Taifa la leo na kesho.

Upvote
0