Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Haya ni maneno tofauti,ingawa hutumiwa na wasemaji wengi wa kiswahili kumaanisha hali moja. Hongo ni tozo sawasawa na kodi,kwa mfano watawala wa jadi waliwatoza au waliwasamehe wafanyabiashara waliopita au kufanya biashara kwenye himaya zao,kwa hiyo hongo lina uhalali unaendana na maadili ya jamii,rushwa haina uhalali wa tozo kimaadi,kwani ni uharifu. Tatizo lililetwa pale watemi walipoitumia hongo kama silaha ya kukomoa,na huo ndiyo ukawa mwanzo wa wadau kutozitofautisha dhana hizi.