KERO Rushwa na utapeli wa baadhi ya wafanyakazi wa Ardhi Halmashauri ya Bagamoyo

KERO Rushwa na utapeli wa baadhi ya wafanyakazi wa Ardhi Halmashauri ya Bagamoyo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Nimekutana na kadhia kubwa ambayo nilinunua viwanja kadhaa kwenye mfumo wa tausi eneo la bagamoyo. Na mwaka huu mwanzoni nilitaka kufatilia kupata hati ya viwanja vyangu. Ila nilishangaa kila mfanyakazi wa halmashauri ili akufanyie kitu flani ni anahitaji umlipe.

Nilikaa siku mbili nafatilia mpaka nikakamilisha mahitaji yote yanayotakiwa na kumkabidhi mfanyakazi wa pale mafaili yangu kwaajiri ya kupata hati. Ilikua january 2026 mwishoni.

Nilichukua mawasiliano ya mfanyakazi aliyechukua mafaili yangu ili niwe napata update kama hati imetoka na kila nilikua nikimpigia ananiambia iko wizarani.

Nilielekea wizarani mwezi wa 5 naambiwa mbona hakuna document zilizowahi kuletwa hapa zinazohusiana na viwanja hivyo.

Niliamua kufunga safari kufika halmashauri ya bagamoyo. Naambiwa aliyechukua files zangu hakuzipeleka na pale ofisini hazipo. Simu zangu hapokei na naambiwa haji kazini na hakuna anayejua sababu.

Sasa najiuliza files za ofisi kazipeleka wapi toka january mpaka may. Nilijaribu kwenda kwa mkubwa wake wa kazi na inaonekana anajua anayoyafanya mfanyakazi wake. Ila hakuna hatua inayo chukuliwa.

Nimepoteza gharama kufunga safari za kwenda huko na kulala kwani natokea mbali. Ila huduma ni mbayaa na kila mtu ofisini ukifika anakuona fursa. Mamlaka iangalie swala hili kwakweli. Sasa tunaanza kuona hakuna umuhimu wa kuwa na ofisi maana huduma za haki na maendeleo ila watendaji wanaotakiwa kuwa msaada ndo wanakua kero kwa wananchi.

Ninashindwa hata nifanye nini maana nimekosa msaada wowote juu ya hatua hii ya mfanyakazi kupotea na documents zangu zote.
 
Documaa zimepoteaje ofisini, Afisa ardhi wilaya anasemaje? Mkuu wa wilaya Bi H anasemaje nae?
 
Serikali ya CCM chini ya uyo SAMUYA ni familia ya kambale Kila mtu anataka rushwa tu. Kwa kua eti mteule wao kauza ngorongoro,Bandari na wao wanachukua chao mapema tu.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Serikali ya CCM chini ya uyo SAMUYA ni familia ya kambale Kila mtu anataka rushwa tu. Kwa kua eti mteule wao kauza ngorongoro,Bandari na wao wanachukua chao mapema tu.
Kazi ni kipimo cha utu
Sure
 
Ingia kwenye mfumo, uwatolee nakala uwapelekee ofisini, waanzie hapo kutatua changamoto.
 
Kwenye mfumo unaingiaje?Na wewe huna akaunti!Na akaunti may be alikufungulia huyo mtu wa ardhi Kwa Siri bila wewe kujua?
''Nimekutana na kadhia kubwa ambayo nilinunua viwanja kadhaa kwenye mfumo wa tausi eneo la bagamoyo'' ina maana hapa alitengeneza akaunti.
 
Back
Top Bottom