SoC04 Rushwa ni adui wa haki kwa Mtanzania mpenda maendeleo

SoC04 Rushwa ni adui wa haki kwa Mtanzania mpenda maendeleo

Tanzania Tuitakayo competition threads

hauleibrahim

Senior Member
Joined
May 17, 2024
Posts
183
Reaction score
125
Rushwa ni adui wa haki Kwa mtanzania yeyote yule mwenye uzalendo na kuipenda nchi yake Kwa moyo wake wote.

Rushwa inaweza kuzibitiwa Kwa njia mbali Kwa kila mtanzania mpenda maendeleo ndani ya nchi yake.

Tukisema rushwa ni adui wa haki Kwa mtanzania hatukosei hata kidogo walio wahi kutana na hizo adha wanafahamu vizuri tukisema kwamba rushwa ni adui wa haki Kwa mtanzania mwenye kupenda maendeleo ya mtu mmoja mmoja au Kwa nchi kiujumla.

Mambo muhimu yanayo weza kudhibiti rushwa ndani ya nchi na kila mwananchi mpenda maendeleo ni kama ifuatavyo.

1.elimu ya uadilifu itolewe maeneo yote Kwa kila mtanzania.elimu hii ijikite kutolewa Kwa kila mtanzania mpenda maendeleo Kwa jamii na nchi yake kiujumla pasipo kuchagua huyu ni mtumishi wa serikali na huyu sio mtumishi wa serikali kiufupi elimu hii itolewe Kwa kila mtu mwenye sifa ya kuitwa mtanzania.

2.vyanzo vya rushwa vifuatiliwe Kwa umakini popote penye harufu ya rushwa ni vizuri pakafuatiliwa Kwa ukaribu mkubwa ili kuikomesha rushwa ndani ya taifa Kwa walio husika katika hilo jambo la rushwa.

3.wawajibishwe Wala rushwa:Kuna njia nyingi ila mm sipendi njia ya kunyonga na haitokuja kutokea nikaipenda ila tutumie njia ya kuwafilisi Mali zao zote yani wabaki o ili Mali zile zirudi Kwa wnanchi walio kosa maendeleo mfano maji mashule n.k njia ya kuwa filisi itakuwa njia Bora na nzuri.

4.kila mtu awe mlinzi wa mwenzake khusu rushwa kama ilivyo madawa ukikutwa nayo tu mtu akitoa taarifa ww umeishia ndani pia iwe hivyo hivyo Kwa mtoa taaarifa ya rushwa yenye vithibitisho kamili ili wahusika wa rushwa wachukuliwe hatua stahiki kabla hawaja ivunja jamii na nchi kiu jumla.

5.iwepo elimu ya usisi Kwa kila mtanzania na sio umimi:umimi mwingi ndio ulio tufikisha hapa tulipo kuhusu rushwa kukua na kuenea na kushindwa kuzibitiwa hiyo hali imechangiwa na watanzania wengi kukaa umimi kuliko usisi matokeo yake mtu hata akiiba hamuonei huruma yule bibi pale kijijini asie pata dawa kila afikapo hospitali ikiwa sababu ni kukubali kwake kupokea rushwa dawa zisifike eneo lake la kazi ya ki nchi ila zifike kwenye ofisi binafsi zao.

6.taaarifa zisipuuzwe za maswala ya rushwa zitolewapo.taaarifa yoyote itakayo husu rushwa vyombo husika vichukue hatua mapema kuwa dhibiti hao wachukua rushwa bila kujali vyeo na nguvu ya wahusika ikoje.

Nchi inaweza komesha rushwa kiujumla kila mtanzania akiwajibika ipasavyo kwenye kuikomesha rushwa.

Miaka 5 mpka kumi 15 nchi bila rushwa inawezekana Kwa kila mtu kuwajibika impasavyo.
 
Upvote 3
Back
Top Bottom