bongo dili
JF-Expert Member
- Feb 13, 2015
- 12,350
- 25,180
Kesi ni biashara Sasa umekula buku 5 hata rim paper tu ya kuandikia kesi yako upati kwann usifungwe miaka Kama mfano wa kuonyesha tunafanya kazi.Jela ni kwa ajili ya watu masikini.Inasemekana, wala rushwa wanaofungwa kwa kosa la rushwa ni wale tu wenye ",tuhela twa dagaa". Wenye mihela hawafungwi.
Kwa kweli inatia uchungu sana!!Vyote kwa pamoja.
Na mazoea pia mkuu mtu unaenda ofisi fulani kufuata stahiki zako kama wewe ivo, unamkuta huyo afisa anakunywa supu, pembeni ana pepsi big huku kashanunua korosho za 5000 kwenye foleni anazo hapo.
Na bado kahawa ya ofisi inamsubiri lakini bado ataitaka hiyo elfu 5 au 10 yako wewe ambae kimuonekano tu umeitamani ile supu.
Ni njaa iliyopelekea kuundwa kwa tabia.
Aisee!Nilikuwa niandike kama hiki. Mbaya zaid imeanzia kwenye jamii ngazi ya familia
Mkuu huna habari? Hata wabunge wanakula rushwa!Chanzo kikubwa cha rushwa nchi hii ni wanasiasa kujipendelea mafao makubwa na kuwaacha watumishi wa umma wengi wao wakiwa na njaa kali. Mbunge analipwa Tsh15m kwa mwezi na marupurupu kibao. Akimaliza muda wake wa miaka mitano mafao ni Tsh300m na ushee. Sasa njoo kwa watumishi miaka 30 halafu mafao na pensheni ni upuuzi mtupu.
Tena siku hizi Rushwa Watu wanapatana Kama biashara,tena wazi wazi kabisa bila kificho, zamani Rushwa ndiyo ilikua inafanywa siri sana,hata mpokeaji hana muda wa kupatana,anapokea anachopewa tu na hakuna kulalamika Kama siku hizi mpokeaji kila anapokea Rushwa ndiyo anazidi taka Rushwa kubwa!!Tanzania Rushwa ni FURSA ya kutoka kimaisha. Hayupo anaeweza kusita kuchukua Rushwa anapopata nafasi, kwanza nafsi yake itamsuta na kumlaumu sana akilazia damu fursa hiyo pekee na muhimu sana ya kutoka na kutoboa maisha. Kwanza akiacha kuchukua atachekwa na jamii [emoji851]
Wanyonge Mahakamani na haki zao sijui inakuwaje!? Naona wengi lazima watakua wanapoteza haki zao kwa kukosa kutoa Rushwa!!Bila kutoa rushwa hii nchi utangoja Sana kupata haki Yako utakuja kupata ukiwa kaburini