Rushwa ya cheo ni sawa na Rushwa nyingine

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
3,197
Reaction score
7,677
Katika shauri dhidi ya Mbowe, mlalamikaji ni Serikali, na Serikali kiongozi wake mkuu ni Rais. Hivyo mlalamikaji katika kesi hii, ni Rais.

Wakati kesi inasubiriwa kutolewa hukumu, mlalamikaji anatoa cheo kwa hakimu anayeendesha kesi ambayo yeye ni mlalamikaji.

Katika mfumo wa utoaji haki, hii siyo rushwa ya wazi?

Hukumu aliyoitoa huyu jaji ambaye amepewa cheo na mlalamikaji, itaaminiwa vipi kuwa haijaathiriwa na rushwa ya kupandishwa cheo?

Wataalam wa masuala ya sheria na masula ya rushwa, mnalionaje hili? Tupeni elimu.
 
Mmmm,sawa inatafakarisha Sana kwa kweli. Na Hilo linaweza kutokea Tanzania tu.
 
Ni kosa, lakini kisheria Rais hashtakiwi akiwa madarakani au akimaliza muda wake kwa mambo aliyofanya kwenye utawala wake, tumefungwa pingu mikononi na miguuni.
 
Kumpandisha mtu cheo wakati yupo katikati ya key project ni rushwa. Tunaona shauri hili lipo arranged na Mh. Mbowe watamfunga miaka watakayo wao wenyewe.

Kwa sasa cha kufanya ni kujikusanya na kuendelea kudai katiba mpya kwa nguvu zaidi, this is the only thing we can do right now.. hawa CCM si watu wazuri.
 
Kesi ya Mbowe mbona imekua yamoto kiasi hiki[emoji23][emoji23]. Kila mtu anaikimbia. Wazee wanaogopa kuwaudhi CCM!
 
Niliwaambia ni geresha Ila watu hawaelewi sabaya kahukumiwa Miaka 30 na walewale Leo mnnapiga makofi hamjui ni mtego wanakuja kumfunga mbowe walewale tuone kama hamjapiga makofi

Kipindi cha nyuma kumbukeni hata kibiti ilisifika Kwa lipi kubomolewa na kuchukuliwa Kwa siraha kwenye vituo vya polisi msidhani ilikuwa inshu ndogo

Yanayokuja yashaandaliwa
 
Kumpandisha mtu cheo wakati yupo katikati ya key project ni rushwa. Tunaona shauri hili lipo arranged na Mh. Mbowe watamfunga miaka watakayo wao wenyewe.

Kwa sasa cha kufanya ni kujikusanya na kuendelea kudai katiba mpya kwa nguvu zaidi, this is the only thing we can do right now.. hawa CCM si watu wazuri.
Rais anapokuwa mtoa rushwa, ataweza kuipiga vita rushwa? Watu waovu kupindukia, mara nyingi hupenda kujificha nyuma ya alama za nje za uchamungu.
 
Rushwa ni adui wa haki,sitapokea wala kutoa rushwa. Mtu kapewa rushwa ya cheo na leo kaitendea haki rushwa hiyo. Aliyetoa na aliyepokea wote ni wahalifu na wahujumu uchumi. Ewe Mwenyezi Mungu ingilia kati utoe hukumu wote hawa wawili,wapige hata kwa Corona.
 
Ni kosa, lakini kisheria Rais hashtakiwi akiwa madarakani au akimaliza muda wake kwa mambo aliyofanya kwenye itawala wake, tumefungwa pingu mikono na miguu.
Huyu ni kumshtakia kwa Mungu tu.
 
Niliwaambia ni geresha Ila watu hawaelewi sabaya kahukumiwa Miaka 30 na walewale Leo mnnapiga makofi hamjui ni mtego wanakuja kumfunga mbowe walewale tuone kama hamjapiga makofi

Kipindi cha nyuma kumbukeni hata kibiti ilisifika Kwa lipi kubomolewa na kuchukuliwa Kwa siraha kwenye vituo vya polisi msidhani ilikuwa inshu ndogo

Yanayokuja yashaandaliwa

Naona mnalazimisha kuchanganya maamuzi ya kesi ya Mbowe na Sabaya, mkiamini kabisa hatujui tofauti yake. Kesi ya Sabaya ni mashitaka ya dhahiri tena na mashahidi wa unyama ule wasiotiliwa shaka. Kesi ya Mbowe na ya kubambikizia mmoja wapo wa waliotengeneza hiyo kesi ni Sabaya ambaye leo hii ni mfungwa kwa ushahidi usioacha shaka. Ndio maana unaona kila jaji sasa anaikimbia kesi hiyo ya Mbowe maana serikali inalazimisha hukumu isiyoendana na ushahidi.
 
Katika shauri dhidi ya Mbowe, mlalamikaji ni Serikali, na Serikali kiongozi wake mkuu ni Rais. Hivyo mlalamikaji katika kesi hii, ni Rais.

Wakati kesi inasubiriwa kutolewa hukumu, mlalamikaji anatoa cheo kwa hakimu anayeendesha kesi ambayo yeye ni mlalamikaji.

Katika mfumo wa utoaji haki, hii siyo rushwa ya wazi?

Hukumu aliyoitoa huyu jaji ambaye amepewa cheo na mlalamikaji, itaaminiwa vipi kuwa haijaathiriwa na rushwa ya kupandishwa cheo?

Wataalam wa masuala ya sheria na masula ya rushwa, mnalionaje hili? Tupeni elimu.
Hivi tunaposema Katiba iliyopo haifai huwa hamtuelewi? Tunaishi kwa huruma na kudra za Mungu tu. Mkuu wa Mhimili ulioleta kesi katikati ya kesi anampangisha cheo hakimu. Unategemea huyo hakimu atoe hukumu inayoegemea kwenye haki kweli? Jamani, mambo mengine muwe mnaelewa hata kama mmeishia darasa la Pili
 
Naona mnalazimisha kuchanganya maamuzi ya kesi ya Mbowe na Sabaya, mkiamini kabisa hatujui tofauti yake. Kesi ya Sabaya ni mashitaka ya dhahiri tena na mashahidi wa unyama ule wasiotiliwa shaka. Kesi ya Mbowe na ya kubambikizia mmoja wapo wa waliotengeneza hiyo kesi ni Sabaya ambaye leo hii ni mfungwa kwa ushahidi usioacha shaka. Ndio maana unaona kila jaji sasa anaikimbia kesi hiyo ya Mbowe maana serikali inalazimisha hukumu isiyoendana na ushahidi.
Sitetei uhalifu wa Sabaya ila nalaani uharibifu wa mfumo wa utoaji haki.

Wasiojulikana kuwafanya kuwa majaji ili kuipa Serikali ushindi ni kosa kubwa. Aliyepewa kesi ya Mbowe mwanzoni na aliyemhukumu Sabaya, wote ni wasiojulikana wanaojulikana.

Sabaya alistahili kuhukumiwa na jaji halisi, sawa kama ilivyo kwa Mbowe na washtakiwa wengine wote. Hakuna namna ya kuwaondoa wasiojulikana ndani ya mahakama bila ya kuwa na katiba mpya.
 
Katika shauri dhidi ya Mbowe, mlalamikaji ni Serikali, na Serikali kiongozi wake mkuu ni Rais. Hivyo mlalamikaji katika kesi hii, ni Rais.

Wakati kesi inasubiriwa kutolewa hukumu, mlalamikaji anatoa cheo kwa hakimu anayeendesha kesi ambayo yeye ni mlalamikaji.

Katika mfumo wa utoaji haki, hii siyo rushwa ya wazi?

Hukumu aliyoitoa huyu jaji ambaye amepewa cheo na mlalamikaji, itaaminiwa vipi kuwa haijaathiriwa na rushwa ya kupandishwa cheo?

Wataalam wa masuala ya sheria na masula ya rushwa, mnalionaje hili? Tupeni elimu.
Hapa ni Mungu tu ndio atakayeingilia kati
 
Rushwa ya Cheo kwa Jaji ambaye anasikiliza shauri la UGAIDI, kapandishwa cheo wakati bado anasikiliza hilo kauli kinalofuatiliwa na watanzania na dunia nzima...kwa aibu kajitoa.

Way forward:

CDM kumbukeni mnapambana na
DOLA yaani muhimuli wa utawala (executives) hapa kuna Police, Usalama wa Taifa, Jeshi nk
BUNGE hapa bado mna mapambano matakatifu na Spika mamoja na hila ya wale Covid 19
MAHAKAMA, leo mmeshuhudia hukumu ambayo haijafuata misingi ya kisheria ya mchi yetu

Mapambano haya yamefikia patamu mno, ni wakati sasa wa kila mwana CDM kusimama kidete ili kuhesabiwa, huu mziki si wa kitoto huu, so far so good kwao, lengo lao bado miezi kadhaa tu litimie.
 
Back
Top Bottom