Rushwa Ya Ngono Kutawala Vyuoni!!

Rushwa Ya Ngono Kutawala Vyuoni!!

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
20,834
Reaction score
26,217
Habari Wana Jamii Forums,..

Kuna hili suala la rushwa ya ngono ambalo limekithiri vyuoni.

Baadhi ya wahadhiri wa vyuo vikuu wanalazimisha mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi wao, inapotokea mwanafunzi kumkatalia mhadhiri basi anakuwa matatani kwani wahadhiri hao huwatamkia waziwazi wanafunzi hao kwamba watawafelisha katika mitihani yao.

Ikumbukwe kuna wanafunzi wanafaulu kwa jitihada zao binafsi na kuna wale wanaofaulu kwa kutoa rushwa ya ngono.

Hebu tutafakari basi, ni nini kifanyike maana suala hili lina changamoto kubwa.

Je mwanafunzi akatae kutoa rushwa ya ngono afeli au atoe rushwa ya ngono apate kufaulishwa!!

Pia nini kifanyike kwa baadhi ya wahadhiri wenye tabia hii chafu ya kutaka rushwa ya ngono ambayo inawaathiri wanafunzi katika taaluma!!

Nawasilisha,...
 
wavae vizuri wakiwa vyuoni na wasome pia....Ila ujue pia hawaathiriki kimasomo kamwe....
 
wavae vizuri kwa namna gani mkuu kabanga, mbona kuna ambao wanajisitiri vyema na mavazi ya heshima kabisa lakini bado wanasumbuliwa kingono na wahadhiri,..
 
Last edited by a moderator:
Dawa ya hao wanaotaka rushwa ya ngono ni kuwawekea mtego ili wakamatwe kwani hii tabia inarudisha nyuma maendeleo ya watoto zetu Pia kueneza maradhi vyuoni hasa ukimwi.
 
^^
Uzuri wake ni G.P.A yake...
Sexual violence is of historic culture, it changes appearance but will never easily come to an end
^^
 
Dawa ya hao wanaotaka rushwa ya ngono ni kuwawekea mtego ili wakamatwe kwani hii tabia inarudisha nyuma maendeleo ya watoto zetu Pia kueneza maradhi vyuoni hasa ukimwi.

Ngono na uzinzi umetawala kuanzia watoto hadi wazee,matajiri hadi maskini ,wanasiasa na wanachama wao,maamuma na wasomi .
Kila sekta ngono imetamalaki,hakuna tena anayeona kama hilo ni kosa.Na imekua ni fasheni kwa wanawake hasa akiombwa ngono na mtu mwenye mapesa au chei kikubwa kwake ni ufahari kwani ndugu zake ,wazazi na marafiki watatambulishwa na kujulishwa habari za uzinzi huo na itaonekana kama ni bahati nzuri kwa huyo mwanamke ,mara nyingine hata kama ana mume basi na mwanaume anaweza akajua na akajikausha kwani utajiri umeingia nyumbani.
Hapo nani wa kumvisha paka kengele.

Ukiwatega na kuwachukulia hatua basi wahadhiri wenzake watawafelisha wanafunzi kwa maksudi mpaka wakome. Assignment zote Total marks 12%;End exiam 22% -Total 34%-(Failed).

Kwani wahadhiri wa vyuo vikuu wanakozi za kufundishwa maadili ya kazi?
Au mtu akishaonekana jembe kwenye masomo yake basi akiomba nafasi ya uhadhiri anapewa?
Matokeo yake yatabaki kama tabia ya mtu binafsi.
 
Wanajipeleka wenyewe, yaani katika kundi la wanafunzi zaidi ya mia mbili huyo mhadhiri anaanzaje kukujua bila kujipeleka?

Halafu wengi wao hawajiamini, ni vilaza, hivi mtu course work inasoma 31 huyo mhadhiri anaanzaje kukutishia kukufelisha?

Kama wanapeana wapeane kiroho safi wasisingizie rushwa.
 
siyo kweli mkuu, wengi wanatongozwa na wahadhiri kwa kulazimishwa.
 
Ngono na uzinzi umetawala kuanzia watoto hadi wazee,matajiri hadi maskini ,wanasiasa na wanachama wao,maamuma na wasomi .
Kila sekta ngono imetamalaki,hakuna tena anayeona kama hilo ni kosa.Na imekua ni fasheni kwa wanawake hasa akiombwa ngono na mtu mwenye mapesa au chei kikubwa kwake ni ufahari kwani ndugu zake ,wazazi na marafiki watatambulishwa na kujulishwa habari za uzinzi huo na itaonekana kama ni bahati nzuri kwa huyo mwanamke ,mara nyingine hata kama ana mume basi na mwanaume anaweza akajua na akajikausha kwani utajiri umeingia nyumbani.
Hapo nani wa kumvisha paka kengele.

Ukiwatega na kuwachukulia hatua basi wahadhiri wenzake watawafelisha wanafunzi kwa maksudi mpaka wakome. Assignment zote Total marks 12%;End exiam 22% -Total 34%-(Failed).

Kwani wahadhiri wa vyuo vikuu wanakozi za kufundishwa maadili ya kazi?
Au mtu akishaonekana jembe kwenye masomo yake basi akiomba nafasi ya uhadhiri anapewa?
Matokeo yake yatabaki kama tabia ya mtu binafsi.

mbona wakikataa wanafelishwa mkuu?
 
Habari Wana Jamii Forums,..

Kuna hili suala la rushwa ya ngono ambalo limekithiri vyuoni.

Baadhi ya wahadhiri wa vyuo vikuu wanalazimisha mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi wao, inapotokea mwanafunzi kumkatalia mhadhiri basi anakuwa matatani kwani wahadhiri hao huwatamkia waziwazi wanafunzi hao kwamba watawafelisha katika mitihani yao.

Ikumbukwe kuna wanafunzi wanafaulu kwa jitihada zao binafsi na kuna wale wanaofaulu kwa kutoa rushwa ya ngono.

Hebu tutafakari basi, ni nini kifanyike maana suala hili lina changamoto kubwa.

Je mwanafunzi akatae kutoa rushwa ya ngono afeli au atoe rushwa ya ngono apate kufaulishwa!!

Pia nini kifanyike kwa baadhi ya wahadhiri wenye tabia hii chafu ya kutaka rushwa ya ngono ambayo inawaathiri wanafunzi katika taaluma!!

Nawasilisha,...

Serikali ya Chukua Chako Mapema iko bize na kuhamisha rasilimali za taifa na kuweka katika mifuko ya watu binafsi hao mafisadi, kwahi imekosa kuyaona wala kuyasikia haya hata watunga sheria ndo wanao ongoza kwa ufuska sio rahisi kukekmea hili, ninaamini hali hii itabadilika siku Tanzania ikija kukombolewa
 
Kwa kwel mkuu rushwa ya ngono ni tatizo kubwa katka ajira na vyuo vya elimu ya juu. Knowing the root causes problem is the first step in problem solving. Kwa mtazamo wangu kuna 7bu kuu 3 za kukithri kwa rushwa ya ngono nazo ni
1. Wanafunzi wenyewe-kuna baadhi yao mavaz yao na jins wanavyo behave inawafanya wahanga.
2. Wahadhiri-baadhi yao wanapenda michepuko na hawana dignity.
3.Mfumo mzma wa uwajibikaji wahadhir weng hu2mia vyeo vyao kama kinga ktk kutimiza matakwa yao, kutokana na bureaucracy na kulindana wanafunz wanaendelea kuwa wahanga kw kuwa hawana cha kufanya.

NINI KIFANYIKE?
1.Ili kukomesha rushwa ya ngono wanafunz lazma wajue vi kwa namna gan mavaz na matendo yao yanaweza kuwafanya wahanga.
2. Waadhiri wafuate maadil ya kaz zao," Professional ethics."
3.Lazma kuwa na uwajibikaji, urasimu na kulindana vikomeshwe
 
Kwa kwel mkuu rushwa ya ngono ni tatizo kubwa katka ajira na vyuo vya elimu ya juu. Knowing the root causes of the problem is the first step in problem solving. Kwa mtazamo wangu kuna sababu kuu 3 za kukithri kwa rushwa ya ngono vyuon nazo ni
1. Wanafunzi wenyewe-kuna baadhi yao mavaz yao na jins wanavyo behave inawafanya wahanga.
2. Wahadhiri-baadhi yao wanapenda michepuko na hawana dignity wala ethics.
3.Mfumo mzma wa uwajibikaji wahadhir weng hutumia vyeo vyao kama kinga ktk kutimiza matakwa yao, kutokana na bureaucracy na kulindana wanafunz wanaendelea kuwa wahanga kwa kuwa hawana cha kufanya.

NINI KIFANYIKE?
1.Ili kukomesha rushwa ya ngono wanafunz lazma wajue ni namna mavaz na matendo yao yanaweza kuwafanya wahanga.
2. Waadhiri wafuate maadil ya kaz zao," Professional ethics."
3.Kuwe na uwajibikaji, pia urasimu na kulindana vikomeshwe
 
wanafunzi wasome kwa bidii,ukifeli kwenye somo la huyo prof pekee ndiyo unaweza kufanya appeal,ukasahihishwa na lecturer mwingine
 
mimi naona na wenyewe midada inajipelekesha kwanini wasiliwe!!!!!
 
Rushwa ilikuwepo toka chuo kinaanza hadi leo.
 
Back
Top Bottom