Rushwa za uchaguzi ujao makanisani zimeanza. Watumishi wa Mungu chukueni tahadhali

tripof

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2024
Posts
829
Reaction score
1,120
Askofu Dr Shoo amenena ukweli kuwa Rushwa za uchaguzi zimeanza kupenyezwa kwenye makanisa na misikitini, bila aibu watumishi wa Mungu na waumini chukueni tahadhali za kutosha ili msije mkajidhalilisha kwa umma wa Tanzania.

Wananchi wanaona yanayotendeka kipindi hiki kwa viongozi wetu. Zingatieni kuwa rushwa na hongo vilimsaliti Yesu na kumsababishia maumivu mjitenge navyo.

Jehenamu haibagui Padre, shehe au Askofu zingatieni maadili ya kanisa na misikiti na nadhili zenu mlizofunga na Mwenyezi Mungu. Nyinyi ni njia ya Haki na Upendo.

Tumeona Rushwa ikitolewa kwa misaada, zawadi,pongezi kwenye makanisa na misikitini hususani kwa wakatoliki na KKKT nk
 
lakin rushwa ilitembea sana kanisani kwako baba askofu wakati wa Uchaguzi wa mkuu wa kanisa, hukukemea ama ile ilikua nini?🐒
 
Watumishi wapi unaowazungumzia?

Maana hata huko makanisani watoaji wakubwa wa sadaka kubwakubwa na kujenga ndio hao hao tuwaowalalamikia kwa ufisadi na huoni hao watumishi na wachungaji kuwakemea na hata kukataa hizo hela.
 
Ni jambo la hovyo sana
 
Vyeo vimekuwa dili hadi kwenye Taasisi za kiroho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…