Mathanzua
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 17,251
- 22,929
- Thread starter
- #21
Source ya hii habari ni ipi?
Anyway, it’s interesting. Nasubiri kuona madikteta wa dunia kama Putin & the oligarchs, Xi & Chinese tycoons, Kim wa NK na wengineo wakihamisha utajiri wao wa kifisadi toka US na EU region. Bila shaka unafahamu kuwa US wanamiliki deni kubwa sana la China kupitia federal treasury bonds. Yaani Wachina wanajua ili utajiri wao usipoteze thamani lazima uhifadhiwe US in dollars.
Thamani ya pesa haiimarishwi na vitu pekee. Bali zaidi na mifumo imara ya pesa iliyojengwa kule New York, London, Brussels, Frankfurt, n.k. Usalama wa pesa ni wa hali ya juu sana. Imagine, matajiri wa dunia wakiwemo mafisadi papa hata wa kwetu, wauza madawa ya kulevya, wote wanafanya kila janja kuhifadhi pesa zao huko.
Huko ni kwenye nchi zenye demokrasia ambako systems zinafanya kazi badala ya maamuzi ya mtu mmoja. Political systems and processes ziko stable. Uchumi unafuata sera zinazokubalika na wengi. Maamuzi muhimu yanachakatwa kiundani na vyombo shirikishi vya maamuzi vyenye kauli ya mwisho.
Sioni uwezekano wa watu kuhifadhi utajiri wao kwenye rubuli (roubles) ilhali haijulikani kesho Putin ataamka vipi. Au kwenye yuan na kuishi na wasiwasi kuhusu mipango na maamuzi ya Xi huko South China Sea! Ni kama ilivyokuwa hapa bongo nyakati zile unaweza amka na kukuta visenti vyako benki vimekaushwa vyote kwa “amri toka juu”. Sasa imagine tungekuwa super power.
BOOM! RUSSIA RETURNS TO THE GOLD STANDARD FOR ITS CURRENCY!!!!!
Russia Returns to Gold Standard - Government to Remove VAT (Tax) on Bullion. This bill will be submitted to the State Duma on March 4. . . .