Kwani uongo? England siyo timu ya magazeti? Unafuatilia mpira kweli? Halafu Hamna mtu mwenye chuki na England, wanachozungumzia watu ndiyo uhalisia huo England hajui mpira. Unajua kwenye mpira ili ufanikiwe kwenye hatua ya makundi kuna haya, uwezo wako, uwezo wa timu pinzani na kundi ulipo likoje? Unajua ni kwa nini Portugal ilipotoka 3-3 na Hispania walishangilia akina Ronaldo? Ni kwa sababu ya kundi walilopo in kundi lenye upinzani mkubwa. Hiyo hali linganisha kwa England majibu utayapata mwenyewe.
Kwanza kuna baadhi ya match zikichezwa unasema kabisa dahhh!!! Leo shughuli ipo. Hiyo hali ilitokea kwa England leo shughuli ipo? Kundi alilipo England ndilo lililombeba akafikia hii hatua tunayozungumzia. Hata Mpira wao ukiutizama unajua kabisa hawa England wakikutana na timu heavy watapoteana uwanjani.
Hujui mpira hata kidogo.
Mimi tangu utoto wangu nasapot England. Unaposema England ni team ya magazeti unamaanisha nini ? Niambie ni team ipi duniani haiandikwi na magazeti yao. Issue ni nyie kufuatilia vyombo vya habari vya england. Kwanini msifuatilie magazeti ya spain au france anadhani huko hakuna magazeti?? Spain kuna gazeti kuna la michezo linaita Macca, France lipo pia linaloitwa Le Elquipe na German lipo Bild. Sasa si muende kuyasoma hayo magazeti na mtuachie Daily Mail,The Sun na magazeti mengine mengi kutoka kisiwani kwetu.
Issue ni kwamba kwenye mpira wa miguu vyombo vya habari vyenye nguvu duniani vipo uingereza ndio maana hata hawa wakina edo na shaffih dauda taarifa zao ni copy and paste kutoka sky sports,BT sports, BBC au Magazeti lukuki ya huko.
Halafu suala la sisi kuwa kundi jepesi huo ni ujinga. German alitolewa na Korea kusini ambae alikuwa ameshaaga mashindano.
Naona mnazidi kuhamisha magoli. Mlianza timu haitavuka makundi, ikavuka. Mkaja kusema haitafuzu 16 bora,ikafuzu. Mkasema haifika robo, ikafika. Mkasema haigusi nusu , imetusua. Hivi hamuoni aibu nyie wanafiki na wazandiki,wachawi wakubwa????
Mtu mzima unakuja na hoja eti england alikuwa kundi jepesi, ila hamsemi Belgium kuwa na yeye alikuwa kundi hilohilo. Belgium wala hamumzungumzii.
Halafu wengi wenu ni wajinga na hamna exposure ya mpira. Mwaka 2002 unajua kuwa brazili alikuwa kundi moja na china?? Mbona hamsemi alikuwa kundi bovu. Acheni utaahaira. Mpira wa sasa hauna mambo ya historia na majina. Mlitegemea timu zenu za Brazil, Argentina,ureno, Spain au German zingefuzu na kutamalaki hatua ya nane bora. Mambo hayakp hivyo.
Hakuna mtu alidhani urusi ingefika hapo ilipo kwa kiwango ilichokuwa nacho kwenye friend matches zake zote lakini naona umeona walipofika.
Kwa taarifa yako england kwa sasa ndio ina mafanikio kwa mashindano ya vikombe vya timu za vijana. Kama wewe ni shabiki wa mpira unaelewa ninachomaanisha. Na unajua engr mwaka jana kabeba kombe lipi na lipi.
Ifike muda muache unafiki na mkubali tumewaprove wrong kwa team hiyo ambayo goli kipa wake tu Jordan Pickford anakipiga Everton wakati kocha alipomuacha Joe Hart mashabiki maandazi kama nyie mnaoangalia majina mlifikiri pickford ni shati.
Mashabiki viazi kama nyie alipoanza kuchezeshwa Harry Maguire (Leicester city) na kumpigisha Benchi Beki kisiki na experienced wa chelsea mlijua Maguire ni shati. Wengi hawaamini. Mifano ni mingi mno.
Kocha Southgate Alipomuacha Wilshere sio wewe tu hata pale Viunga vya jiji la london maneno ya chini kwa chini yaliibuka kuhusu kuachwa kwake. Nyie hamuijui England kaeni kimya.
Mchezaji aliechwa England nikaumia ni Jonjo Shelvely na Towvosk. Sijui kama unawafahamu.
KamA umefuatilia Bundesliga mwaka huu nina vijana wawili wa kiingereza wameuwasha moto balaaaaaaa. Kwa kukusaidia tu wote walikuwa kwenye kikosi cha England under17 kilichotwaa kombe la dunia mwaka jana chini ya captain Andre Gomes anaekipiga pale Manchester United. Sijui shabiki ukwaju kama wewe unayajua haya.
Tukutane nusu fainali.