England itawashangaza wengi itakapomtoa croatia.
Halafu sielewi kwa nini watu wengi duniani hawaipendi england
Ndugu yangu nikupongeze kwa kutupa burdani tofauti kabisa na mada mbili nilizozisoma kabla. Kumbe England wakitolewa ni kilio na fujo. Ubingwa wa kujitangazia wazi namna hiyo! Sijui Wafaransa huko waliko mambo yakoje? Presha kama hii iliwatoa Brazil fainali WC 1998. Huenda wanaitumia kwa vita ya Kisaikolojia kabla ya mechi kuwatisha Ufaransa, Croatia na Ubelgiji. Watakuwa wamepata ushauri kwa wataalamu.Tuombe isitokee hii, dunia itasimama kwa mda
England ni nchi yenye mashabiki vichaa wa sokaView attachment 806452
Hahahaa. Ndioooo. [emoji85] [emoji85]Anhaaa, nishajua kidonda kingine kilipo kumbe sio jangwani tu!
Duuh! Rafiki.France nipo na nyieeee
Kwa hyo unataka kuniambia ile ahadi niliyopewa leo yakutunikiwa saa tatu usiku na mwanamke niliepambana nae kwa miaka miwili niipotezee?[emoji35] [emoji35] [emoji35]Leo ndio Leo Mtoto Hatumwi Gengeni, Ni Nusu Fainali ya kwanza ya WORLD CUP ambapo FRANCE anakipiga na BELGIUM. VARANE, na UMTITI wataweza Kuwazuia HAZARD na DE BRUYNE? Au ALDERWEIRD na KOMPANY wataweza Kuzima Moto wa MBAPPE? Nani Atashinda nani atarudi nyumbani?
Uchambuzi maridadi kabisa mkuu, na vile Cassamiro alikua hayupo kuharibu mipango ya Belgium basi dimba la katikati likatawaliwa vyema na kina Fellain kiungo cha Brazil kikafunikwa kabisaaFellain.... Yes. Belgium dhidi ya Brazil, Fellain ndiye aliyekuwa mzizi wa kwanza wa kuizuia Brazil kabla ya Hazard kuiogopesha. Martinez alianzia hapo, na Tite akafia hapo. Pengine msaada mkubwa kwa Munier ulianzia kwa Fellain. Hapa Fellain alianza kwanza kwenye miguu ya Neymar ndio mpira umfikie Munier.
Leo Mungu kawajaalia tena kawapa Klyane Mbappe upande huo. Bahati nzuri kwa Munier ni kukutana na wachezaji ambao anafanya nao mazoezi katika klabu ya PSG.......
Kama Chadli atakosa mchezo huu basi hapo panaweza kuwa sehemu yenye kidonda kwa Martinez. Carrasco alishindwa kabisa kupanda na kushuka kama wingback na sijui kama Vermaleen kama anaweza kuwa msaada katika hilo.
Leo kuna utamu wake ....kante sijajua mpaka leo ameamukia ubavu upi kabla ya kumuwaza Pogba .....Paul Pogba, Ng'olo Kante na Matuidi..... Wakianza kwa pamoja wanaweza kuwa na uchachu sana mbele ya KDB, Witsol na Mkubwa Fellain..... Role ya kiungo cha ufaransa inanguvu sana katika kuzuia wapinzani haswa wanaopitia katikati. Ila pia wamekuwa wakisapoti mashambulizi kupitia katikati pia na kutupa mipira mirafu.Uchambuzi maridadi kabisa mkuu, na vile Cassamiro alikua hayupo kuharibu mipango ya Belgium basi dimba la katikati likatawaliwa vyema na kina Fellain kiungo cha Brazil kikafunikwa kabisaa
Ntakua nakitonesha mara kwa mara, shauri zakoHahahaa. Ndioooo. [emoji85] [emoji85]
Ha ha halukaku anabeba kombe
You are one of the best soccer analysts mkuu, najikuta nafuatilia kwa umakini uchambuzi wako...Leo kuna utamu wake ....kante sijajua mpaka leo ameamukia ubavu upi kabla ya kumuwaza Pogba .....Paul Pogba, Ng'olo Kante na Matuidi..... Wakianza kwa pamoja wanaweza kuwa na uchachu sana mbele ya KDB, Witsol na Mkubwa Fellain..... Role ya kiungo cha ufaransa inanguvu sana katika kuzuia wapinzani haswa wanaopitia katikati. Ila pia wamekuwa wakisapoti mashambulizi kupitia katikati pia na kutupa mipira mirafu.
Kama Mbappe atacheza kama alivyocheza dhidi ya Uruguay basi nawaona wafaransa wakitokwa machozi baada ya dk za VAR. Kuna haja ya yeye kujitambua na kutambua umuhimu wa mchezo. Dhidi ya Uruguay kuna utoto mwingi ulitawala kwenye ule ubora wake na kumfanya awe mchezaji wa kawaida sana.
Silaha ya kwanza kwa Ufaransa ni gloves za Hugo Lyoris kabla ya njumu za Antonio Greizman..... Umbile lake jumlisha na janja janja yake, weka na ubora wake vinaweza kuwa sumu kwa Defensive zone ya Belgium.