Russia World Cup 2018: France crowned World Champions after defeating Croatia 4-2

Sababu wakoloni wanajisifu sana. Cheki tu UEFA liver ilipata upinzani kila kona.

Pia ule ubishi wa ligi bora duniani nao umechangia,England wamejaza kikosi toka EPL wakati la liga na wengineo (wachezaji wao wengi) wameshatoka world cup zaman
England itawashangaza wengi itakapomtoa croatia.
Halafu sielewi kwa nini watu wengi duniani hawaipendi england
 
Tuombe isitokee hii, dunia itasimama kwa mda

England ni nchi yenye mashabiki vichaa wa sokaView attachment 806452
Ndugu yangu nikupongeze kwa kutupa burdani tofauti kabisa na mada mbili nilizozisoma kabla. Kumbe England wakitolewa ni kilio na fujo. Ubingwa wa kujitangazia wazi namna hiyo! Sijui Wafaransa huko waliko mambo yakoje? Presha kama hii iliwatoa Brazil fainali WC 1998. Huenda wanaitumia kwa vita ya Kisaikolojia kabla ya mechi kuwatisha Ufaransa, Croatia na Ubelgiji. Watakuwa wamepata ushauri kwa wataalamu.
 
Fellain.... Yes. Belgium dhidi ya Brazil, Fellain ndiye aliyekuwa mzizi wa kwanza wa kuizuia Brazil kabla ya Hazard kuiogopesha. Martinez alianzia hapo, na Tite akafia hapo. Pengine msaada mkubwa kwa Munier ulianzia kwa Fellain. Hapa Fellain alianza kwanza kwenye miguu ya Neymar ndio mpira umfikie Munier.

Leo Mungu kawajaalia tena kawapa Klyane Mbappe upande huo. Bahati nzuri kwa Munier ni kukutana na wachezaji ambao anafanya nao mazoezi katika klabu ya PSG.......

Kama Chadli atakosa mchezo huu basi hapo panaweza kuwa sehemu yenye kidonda kwa Martinez. Carrasco alishindwa kabisa kupanda na kushuka kama wingback na sijui kama Vermaleen kama anaweza kuwa msaada katika hilo.
 
Mechi zimefika kiwango cha nusu fainali. Sina maslahi yeyote binafsi na nchi hizo nne za ulaya zilizo fikia hatua hiyo.

Lakini mimi binafsi kutokana na kumuhifadhi, kumtibu na kumpa usalama Mhe. Tundu Lissu nchini Ubeligiji najikuta NAIOMBEA HERI NCHI HIYO ipate furaha kushinda leo na ikiwezekana kubeba kombe kama zawadi kwao kwa wema wao kwa nchi yetu iliyo jaa chuki na ubaguzi sasa hivi.

Ukiniunga mkono nipe like nisikie raha nami! wale wenye chuki zao wapitilize tuu kwenda Airport kupiga selfie na mdude wetu mpya!
🙂🙂🙂
 
Leo ndio Leo Mtoto Hatumwi Gengeni, Ni Nusu Fainali ya kwanza ya WORLD CUP ambapo FRANCE anakipiga na BELGIUM. VARANE, na UMTITI wataweza Kuwazuia HAZARD na DE BRUYNE? Au ALDERWEIRD na KOMPANY wataweza Kuzima Moto wa MBAPPE? Nani Atashinda nani atarudi nyumbani?
Kwa hyo unataka kuniambia ile ahadi niliyopewa leo yakutunikiwa saa tatu usiku na mwanamke niliepambana nae kwa miaka miwili niipotezee?[emoji35] [emoji35] [emoji35]
 
Fellain.... Yes. Belgium dhidi ya Brazil, Fellain ndiye aliyekuwa mzizi wa kwanza wa kuizuia Brazil kabla ya Hazard kuiogopesha. Martinez alianzia hapo, na Tite akafia hapo. Pengine msaada mkubwa kwa Munier ulianzia kwa Fellain. Hapa Fellain alianza kwanza kwenye miguu ya Neymar ndio mpira umfikie Munier.

Leo Mungu kawajaalia tena kawapa Klyane Mbappe upande huo. Bahati nzuri kwa Munier ni kukutana na wachezaji ambao anafanya nao mazoezi katika klabu ya PSG.......

Kama Chadli atakosa mchezo huu basi hapo panaweza kuwa sehemu yenye kidonda kwa Martinez. Carrasco alishindwa kabisa kupanda na kushuka kama wingback na sijui kama Vermaleen kama anaweza kuwa msaada katika hilo.
Uchambuzi maridadi kabisa mkuu, na vile Cassamiro alikua hayupo kuharibu mipango ya Belgium basi dimba la katikati likatawaliwa vyema na kina Fellain kiungo cha Brazil kikafunikwa kabisaa
 
Leo kuna utamu wake ....kante sijajua mpaka leo ameamukia ubavu upi kabla ya kumuwaza Pogba .....Paul Pogba, Ng'olo Kante na Matuidi..... Wakianza kwa pamoja wanaweza kuwa na uchachu sana mbele ya KDB, Witsol na Mkubwa Fellain..... Role ya kiungo cha ufaransa inanguvu sana katika kuzuia wapinzani haswa wanaopitia katikati. Ila pia wamekuwa wakisapoti mashambulizi kupitia katikati pia na kutupa mipira mirafu.

Kama Mbappe atacheza kama alivyocheza dhidi ya Uruguay basi nawaona wafaransa wakitokwa machozi baada ya dk za VAR. Kuna haja ya yeye kujitambua na kutambua umuhimu wa mchezo. Dhidi ya Uruguay kuna utoto mwingi ulitawala kwenye ule ubora wake na kumfanya awe mchezaji wa kawaida sana.

Silaha ya kwanza kwa Ufaransa ni gloves za Hugo Lyoris kabla ya njumu za Antonio Greizman..... Umbile lake jumlisha na janja janja yake, weka na ubora wake vinaweza kuwa sumu kwa Defensive zone ya Belgium.
 
Salary Slip ukuje humu muzee! au nawe ume changanywa kwenye uhujumu uchumi? maana siku hizi hata ukiwaumbua wasio julikana unaitwa muhujumu uchumi
 
Leo kuna utamu wake ....kante sijajua mpaka leo ameamukia ubavu upi kabla ya kumuwaza Pogba .....Paul Pogba, Ng'olo Kante na Matuidi..... Wakianza kwa pamoja wanaweza kuwa na uchachu sana mbele ya KDB, Witsol na Mkubwa Fellain..... Role ya kiungo cha ufaransa inanguvu sana katika kuzuia wapinzani haswa wanaopitia katikati. Ila pia wamekuwa wakisapoti mashambulizi kupitia katikati pia na kutupa mipira mirafu.

Kama Mbappe atacheza kama alivyocheza dhidi ya Uruguay basi nawaona wafaransa wakitokwa machozi baada ya dk za VAR. Kuna haja ya yeye kujitambua na kutambua umuhimu wa mchezo. Dhidi ya Uruguay kuna utoto mwingi ulitawala kwenye ule ubora wake na kumfanya awe mchezaji wa kawaida sana.

Silaha ya kwanza kwa Ufaransa ni gloves za Hugo Lyoris kabla ya njumu za Antonio Greizman..... Umbile lake jumlisha na janja janja yake, weka na ubora wake vinaweza kuwa sumu kwa Defensive zone ya Belgium.
You are one of the best soccer analysts mkuu, najikuta nafuatilia kwa umakini uchambuzi wako...
 
Back
Top Bottom