Sasa kama unakiri Uruguay, Russia, na sweden hawakucheza vizuri na walipata matokeo mazuri kwa nini na waingereza usiwaweke kwenye hilo kundi kuwa walicheza vibaya na wamepata matokeo. Kipi kinakufanya uwatoe kwenye kundi la waliecheza vibaya ila matokeo wamepata.
Kinachowasumbua nyie ni kuangalia mechi kimazoea. Mpira wa sasa ni matokeo na kuwa resilient kwa aggressiveness ya opponent wako, ndicho walichofanya England jana, licha ya ukali wa colombia waliambulia kona mbili tu ndani ya dakika 120 na kuvurumishwa nje ya mashindano kwa mikwaju ya penati.
Mmezoea kuangalia mechi kimazoea. Katika team nane zilizosalia ukitoa Brazil na Uruguay zingine zilizobaki kufika robo fainal miaka ya hivi karibuni ilikuwa ni ngumu sana (urusi,croatia,sweden,France,England na belgium) na hapo ndipo mnapopata mawazo kuwa hizi team zimefikaje wakati mateam yenu kama Germany, Ureno,Argentina na Spain zipo nyumbani.
Tukutane kesho kutwa.