Mimi si shabiki wa Brazil lakini laiti Brazil wangelipanga kikosi chao vizuri Belgium angelitoka. Kipindi cha kwanza watatu ndiyo waliisumbua Brazil, De broune, Lukaku na Hazard. Kati pale Brazil walikosa kabisa kiungo De broune akawa anapita tu na wakampa jina kiuzembe jamaa akawànyoa. Angalia second half Brazil ndipo wakaamka alipoingia Ferminho, Augasto na Costa. Costa kawa wings tena anayezunguka uwanja na mwenye control ya mpira hali iliyomfanya Courtnho alirudi kuwa namba 8, Neymar 10 na Costa 7. Mpira ulibadilika mbona, Kocha wao angelikuwa na utambuzi ule basi tungeliyaongelea mengine.
Lakini upo sahihi, Mpira wa sasa ni wa kukaza sana history hazisaidii kitu. Nina uhakika the next world cup south Americans teams watakuwa completely different.