Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Katika muendelezo wa kinachoonekana ni uasi kwa serikali ya Urusi Wagner group wanaripotiwa kutekea na kutwaa makao makuu ya jeshi katika mji wa Rostov. Misururu ya wapiganaji wa Wagner katika maeneo mbalimbali inazidi kuoenkea ndani ya Urusi, kwa sasa wapo Voronezh na kuna taarifa wanataka kuelekea Moscow.
Katika upande mwingine, vyombo vya Usalama vya Urusi vimevamia makao makuu ya Wagner huko St. Petersburg.
Prigozhin alikutana na manaibu wa waziri wa Ulinzi na GRU akiwasilisha madai yake ya kukabidhiwa Waziri wa Ulinzi, Shoigu na mkuu wa majeshi, Gerasimov ili Wagner wasitishe operation yao ndani ya Urusi.
Helicopter kadha zimeshambuliwa na kuangushwa maeneo mbalimbali ndani ya Urusi ila hazijajulikana ni za upande gani. Kuna video nyingi pia zilizogaa zikidaiwa na Wagner ni jeshi la Urusi linashambulia kambi za Wagner ndani ya Ukraine na misafara yake ya wapiganaji ndani ya Urusi.
Putin anatarajiwa kutoa kauli muda mfupi ujao kuhusu hali inavyoendelea ndani ya Urusi. Utawala wa Biden umetoa taarifa unafuatilia kwa karibu yanayoendelea ndani ya Urusi.
---
Rais Vladimir Putin amemtuhumu Mmiliki wa Jeshi Binafsi la Wagner, Yevgeny Prigozhin, juu ya jaribio la mapinduzi dhidi ya Majeshi ya Urusi baada ya Wagner kudai Serikali inahusika na mauaji ya Wapiganaji wa Wagner
Kwa mujibu wa ABCNews, Rais Putin amejulishwa rasmi kuwa Vikosi vya Wagner vimetangaza kuuteka Mji wa Rostov-on-Don pamoja na kushikilia kambi zote za Majeshi ya Urusi zilizopo eneo hilo
Kupitia taarifa ya Video, Prigozhin amekaririwa akiitaka Ikulu ya Urusi (Kremlin) kumkabidhi kwake Mkuu wa Vikosi vya Kijeshi vya Urusi vinginevyo wataingia Jijini #Moscow na kufanya mashambulizi kwa yeyote anayewaingilia
Ikumbukwe Russia na Wagner Group walikuwa na makubaliano ya ushirika katika Vita dhidi ya Ukraine ambapo Wagner walikuwa msaada mkubwa kwa Serikali ya Rais Putin tangu kuanza kwa Vita hiyo.