Russia yavurugana na Wagner Group, waanza kutuhumiana kwa Uasi

Russia yavurugana na Wagner Group, waanza kutuhumiana kwa Uasi

Mrusi wa Block E, Kigamboni Yericko Nyerere anasema

Mvutano wa muda mrefu kati ya Waziri wa Ulinzi wa Urusi na Mkuu wa Wagner PMC ulichukua sura nyingine 23/6/2023 pale kiongozi wa Wagner Yevgen Prigozhin alipotangaza kutotii amri ya Wizara ya Ulinzi akisisitiza ni wakati sasa wakubadili safu za uongozi wa jeshi. Tangazo hilo lilifuata baada ya muda mrefu tangu Wagner PMC imalize Oparesheni kule Bakhmut ambapo imekuwa ikinyimwa tenda huku Wizara ya Ulinzi ikiwapatia Akhmat kikosi cha Chechinia kilicho chini ya Ramzan Kadryov. Wagner wanalalamika kuwa Waziri wa Ulinzi wa Urusi Jenerali Shoigu hawapendi anaona wanafaidika sana wakifanikiwa misheni wanazopewa, na kwamba kule Bakhmut aliwahujumu sana kwakuchelewesha kuwapatia silaha hali iliyofanya mji ule kukombolewa kwa gharama kubwa ya damu ya mamluki wengi.

Tangu Wagner wamalize kazi kule Bakhmut, Kiongozi wao Yevgen amekuwa akifuatilia mkataba mwingine bila mafanikio, na hivi karibuni tarehe 18/6/2023 alipewa mkataba ambao atatakiwa kuanza kazi mwezi wa 8, 2023 hali iliyomkwaza akitoa sababu kwamba jeshi lake la watu zaidi ya 30,000 walio katika ajira rasmi na vibarua zaidi ya 50,000 wako tu wanasubiri kazi, huku akishuhudia Ukraine ikianzisha mashambulizi katika milki ya Urusi. Hilo anaona kama ni dharau kubwa kwake. Alianza ukosozi wa kijeshi, ambapo Mkuu huyo wa Wagner tarehe 20/6/2023 alisema Jeshi na waziri wa Ulizi wa urusi wanamdanganya Rais juu ya maendeleo ya Oparesheni ya Urusi,

Tangazo hili la Yevgen Prigozhin lilikuwa kama uasi dhidi ya Jeshi, ambapo Huduma ya Usalama ya Shirikisho la Urusi ilifungua kesi ya jinai dhidi ya mkuu wa Wagner PMC, Yevgeny Prigozhin, Kamati ya Kitaifa ya Kupambana na Ugaidi (NAC) iliripoti. Kwamjibu wa sheria ya Jinai ya Urusi kuna kifungu cha 279 "Uasi wa Silaha", inasema: "Kupanga uasi wa kutumia silaha au kushiriki kikamilifu ndani yake kwa madhumuni ya kupindua au kubadilisha kwa nguvu utaratibu wa kikatiba wa Shirikisho la Urusi au kukiuka uadilifu wa eneo la Shirikisho la Urusi, mtu/watu hao wataadhibiwa kwa kifungo jela cha miaka 12 hadi 20 na kizuizi cha uhuru kwa muda wa hadi miaka miwili."

Idara hiyo ilisisitiza kuwa madai yote yaliyoenezwa kwa niaba ya mwanzilishi huyo wa Wagner hayana msingi. wowote. Wizara ya Ulinzi iliripoti kwamba habari iliyochapishwa na Yevgeny Prigozhin kuhusu "mgomo" kwenye kambi za nyuma za kikundi cha Wagner sio kweli. Wizara ilizitaja tuhuma hizo kuwa ni uchochezi. Pia walibaini kuwa wanajeshi wa Urusi wanaendelea kutekeleza misheni ya mapigano kwenye mstari wa ulinzi katika eneo la operesheni maalum. Msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov alisema kuwa, Rais Putin anafahamu kwa karibu hali inayoendelea ya Mkuu wa Wagner Yevgen Prigozhin na Waziri wa Ulinzi Shoigu, hatua zote muhimu zinachukuliwa. Asubuhi ya 24/6/2023 kundi la Wagner lilirusha Video iliyonyesha Mkuu wa Wagner Yevgeny Prigozhin akikutana na Kanali Jenerali Yunus-Bek, Naibu Waziri wa Ulinzi wa Wilaya ya Kijeshi ya Kusini ya jeshi la Urusi huko Rostov wakizungumza. Prigozhin aliripotiwa kufanya mazungumzo na Yunus-Bek. Hili halikuthibitishwa na Wuzara ya Ulinzi ya Urusi.

Rais Putin wa Urusi alizungumza na vyombo vya habari asubihi ya tarehe 24/6/2023 kuelezea na kufafanua kilichojiri 23/6/2023. Putin alianza kwakusema kwamba usiku alizungumza na makamanda wa pande zote: askari wanapigana kishujaa. Putin aliendelea kusema, "Ninatoa wito kwa Warusi, jeshi na vyombo vya kutekeleza sheria na kwa wale ambao walisukumwa kwenye njia ya uasi wa kutumia silaha kwa udanganyifu na vitisho kuzingatia umoja, uimarishaji na uwajibikaji".

Akaendelea kusema, "Migogoro yoyote inapaswa kutupiliwa mbali wakati wa operesheni maalumu, hatima ya watu wetu sasa inaamuliwa", Putin aliita vitendo vya kugawanya umoja ni ukengeufu. Akasema, "Tunachokabiliana nacho ni usaliti, Viongozi hawataruhusu mgawanyiko nchini Urusi ujirudie, tutalinda watu, Kila mtu ambaye alianza kwa makusudi njia ya usaliti atapata adhabu isiyoepukika, Vikosi vya jeshi vitapokea maagizo yanayofaa, Hatua zitachukuliwa ili kuleta utulivu huko Rostov-on-Don, wanajeshi walipokea amri ya kudhibiti viongozi wa uasi.

Kwa upande mwingine, Oparesheni ya ulinzi wa maeneo yaliyotwaliwa na Urusi iliendelea chini ya vikosi vya Akhmat, Vikosi vya Urusi vimekikomboa kijiji cha Sinkovka katika Mkoa wa Kharkov na sasa vinapigana huko Petropavlovka. Wapiganaji wa Urusi wanasonga mbele kwenye viunga vya jiji la Kupyansk, na kutengeneza daraja la shambulio dhidi ya jiji hilo. Hii inaweza kuwa hasara kubwa kwa Ukraine katika mkesha wa mkutano wa kilele wa NATO, ndiyo maana jeshi la Ukraine lilianza haraka kuhamisha akiba kuelekea Kupyansk kutumia katika kile kinachoitwa 'kukabiliana na mashambulizi'. Na Vikosi vya Anga vya Urusi viliendelea na mashambulizi ndani ya Jiji la Kyiv na mikoa mingine likilenga kambi za kijeshi na miundombinu ya kijeshi, maghala ya silaha za kimagharibi nk.

Kwa undani zaidi utapata katika kitabu kipya cha MOSCOW: Oparesheni Ukraine kinachokujia hivi karibuni.

Na Yericko Nyerere
Murusi wa Mbutu Kigamboni anaendekea kuishiwa pumzi haamini masikio na macho yske....shwain Nyerere
 
Nchi utavurugika Ile, ht km hili litapita madhara yake yataishi mda mrefu na yatakuwa na madhara sana kwa stability ya nchi
 
Wanajeshi wa Chechnya wa Kadyrov wamejiunga na jeshi la nchi kupambana na Wagner

Kadyrov mr showoff, since hii vita imeanza ni side mbili tu zimekuwa realy commited RF na wagner only
 
Urusi tuliwa over rate! Wameshindwa kupigana objectively na kuishia kupigana vita isiyo na mwisho ambayo inawateketeza.

Wangetafuta exit way then wapige propaganda waachane na vita.

Wakiondoka Ukraine wataipa nafasi NATO kujitanua zaidi na kuwa tishio kwa usalama wao.
Hawana option nyingine zaidi ya kuendelea na mapambano
 
Nasikia askari wa mamluki katika vita ya Urusi na Ukraine wakiitwa Wagner. Hawa ni watu gani hasa na motive yao ni nini katika vita hii?
 
Hicho kikundi kitajuta kuundwa, russia atakifyagilia mbali hakina utii ni waasi tu
 
Back
Top Bottom