Wakuu heshima mbele!
Leo katika mdahalo Wa kisiasa kupitia STAR TV, uliokwenda kwa mada ya "kumbukumbu miaka 49 mapinduzi ya Zanzibar"; katika kupangua hoja zilizotolewa na wachangiaji wengine, kuwa japo umri Wa Uhuru (miaka 50) wetu ni robo ya umri Wa Uhuru Wa marekani (miaka 200),Lakini bado tupo gizani kiuchumi. huyu Bwana (Mwana ccm mkongwe, Rutalaka) amesisitiza kuwa uchumi Wa Tanzania sasa ni robo ya uchumi Wa marekani.
Sasa wakuu wenye idea na mambo ya uchumi kimataifa watujuze undani Wa hii hoja! Nawasilisha.

GDP ya USA ni aprox $15 Trillion (2011)
GDP ya Tanzania aprox $23 billion (2011)
Tanzania hatujafika hata $1 trillion! Hiyo robo anayoongelea ni ipi?
well stated mkuu! Na alikuwa akisisitiza kuwa yeye ni mkongwe na ameshikaTatatizo ni kuwa wapo pia watu hawana kazi wanawasikiliza wanjika kama hawa. Hata china ambayo second largest economy in the world is yet to reach half of the American Economy, sasa mtu ana amka asubuhi anaaga kwenda kwenye kipindi na akitoka anawaambia watu mumeona nilivyomwaka nondo kwenye TV. Poor Tanzania.
Wakuu heshima mbele!
Leo katika mdahalo Wa kisiasa kupitia STAR TV, uliokwenda kwa mada ya "kumbukumbu miaka 49 mapinduzi ya Zanzibar"; katika kupangua hoja zilizotolewa na wachangiaji wengine, kuwa japo umri Wa Uhuru (miaka 50) wetu ni robo ya umri Wa Uhuru Wa marekani (miaka 200),Lakini bado tupo gizani kiuchumi. huyu Bwana (Mwana ccm mkongwe, Rutalaka) amesisitiza kuwa uchumi Wa Tanzania sasa ni robo ya uchumi Wa marekani.
Sasa wakuu wenye idea na mambo ya uchumi kimataifa watujuze undani Wa hii hoja! Nawasilisha.
yule mzee ni mchumia tumbo na mvuta bangi kama silinde yaani mimacho imemtoka kusema upuuzi ule ajui kuwa pato la mtu mmoja tu kama hayati michael lilikuwa linaendesha wizara moja wapo hapa tanzania kwa miaka hawa star tv watafute watu wa maana tunapojadili facts issues za taifa letu yaani yule mzee ovyo kabisa
Huyu ni kada mkongwe wa CCM. Hiki ni kipimo kizuri cha fikra na upeo wa mambo ndani ya CCM. Huyu mzee, kada wa CCM hana taarifa sahihi, ana tatizo la kutumia uzoefu! Mawazo mgando! Ndugu yangu, huna haja ya kulinganisha tanzania na marekani. Marekani ni taifa kubwa mno kupita maelezo lilianza zaidi ya miaka 200 iliyopita hivyo ni kutokuwa makini na inawezekana ndiyo mtindo wa CCM kuwapumbaza watanzania. Huwezi kulinganisha Mike Tyson na Rashid Matumla! Kuna nchi kama Indonesia, Malaysia au Korea ya Kusini na kasikazini zilikuwa na uchumi sawa na tanzania wakati tunapata uhuru. Sasa hivi mataifa haya ukilinganisha na tanzania unaweza kutokwa na majozi na kukata tamaa ya maisha. Nchi hizi sasa zinakimbizana na mataifa makubwa ya ulaya ya europa na marekani! Ni CCM yenye mawazo mgando inayojua kushinda kwa kishindo tu kama mzee Rutalaka waliotufikisha hapa pomoja na utitili ya rasilimali tulizojariwa na mwenyezi mungu. Taifa letu limekwama kwa kuongozwa na chama wasio na mawazo mapya na badala yake wametumbukia katika shimo la kila mwenye madaraka ndani ya CCM na serikali yake wanashindana kujilimbikizia utajiri wao na washirika wao. Tanzania ilipofikia na viongozi tuliona nakumbuka usemi wa mwanafalsafa bora dunia Albert Einsten alisema hivi: "We can't solve problems by using the same kind of thinking (CCM) we used when we created them". Taifa hili lipende lisipende ili lipate mwelekeo sahihi kutoka hapa tulipo linahitaji mawazo mapya, new kind of thinking to solve the existing and future challenges. CCM MUST STEP DOWN IN 2015!!!!!