Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyu ni kada mkongwe wa CCM. Hiki ni kipimo kizuri cha fikra na upeo wa mambo ndani ya CCM. Huyu mzee, kada wa CCM hana taarifa sahihi, ana tatizo la kutumia uzoefu! Mawazo mgando! Ndugu yangu, huna haja ya kulinganisha tanzania na marekani. Marekani ni taifa kubwa mno kupita maelezo lilianza zaidi ya miaka 200 iliyopita hivyo ni kutokuwa makini na inawezekana ndiyo mtindo wa CCM kuwapumbaza watanzania. Huwezi kulinganisha Mike Tyson na Rashid Matumla! Kuna nchi kama Indonesia, Malaysia au Korea ya Kusini na kasikazini zilikuwa na uchumi sawa na tanzania wakati tunapata uhuru. Sasa hivi mataifa haya ukilinganisha na tanzania unaweza kutokwa na majozi na kukata tamaa ya maisha. Nchi hizi sasa zinakimbizana na mataifa makubwa ya ulaya ya europa na marekani! Ni CCM yenye mawazo mgando inayojua kushinda kwa kishindo tu kama mzee Rutalaka waliotufikisha hapa pomoja na utitili ya rasilimali tulizojariwa na mwenyezi mungu. Taifa letu limekwama kwa kuongozwa na chama wasio na mawazo mapya na badala yake wametumbukia katika shimo la kila mwenye madaraka ndani ya CCM na serikali yake wanashindana kujilimbikizia utajiri wao na washirika wao. Tanzania ilipofikia na viongozi tuliona nakumbuka usemi wa mwanafalsafa bora dunia Albert Einsten alisema hivi: "We can't solve problems by using the same kind of thinking (CCM) we used when we created them". Taifa hili lipende lisipende ili lipate mwelekeo sahihi kutoka hapa tulipo linahitaji mawazo mapya, new kind of thinking to solve the existing and future challenges. CCM MUST STEP DOWN IN 2015!!!!!
mkuu hii comment yako imenifanya nicheke sana, lakini baada ya kuitafakari imebidi nisikitike sana hasa kujikuta nikiwa bado ndani ya hii nchi!
GreenCity tuna matatizo kweli.........
nimeipenda sana analysis yako
yani hata Mimi nawashangaa Hawa Star tv huyu mzee wanampenda sana, maana anapata sana mialiko Yao.
Mwenyekiti wake alishatamka hajui ni kwanini sisi ni maskini..kwa lugha nyepesi tunaye mtegemea atufikishe kwenye hiyo robo hajui ni wapi pakuanzia(Mwana ccm mkongwe, Rutalaka) amesisitiza kuwa uchumi Wa Tanzania sasa ni robo ya uchumi Wa marekani.
hili ni tatizo kubwa zaidi ya tunavyodhani maana tayari kuna mawazo kuwa tuwaheshimu wakongwe, wazoefu, wanausalama na mengine kama hayo. Tunachosahau ni kuwa hawa watu wana uzoefu wa kuharibu ambao kimsingi umetufikisha hapa tulipo na kwa bahati mbaya hawataki kuambiwa lolote kwa vile wanaelewa kila kitu ati!Huyu ni kada mkongwe wa CCM. Hiki ni kipimo kizuri cha fikra na upeo wa mambo ndani ya CCM. Huyu mzee, kada wa CCM hana taarifa sahihi, ana tatizo la kutumia uzoefu! Mawazo mgando! Ndugu yangu, huna haja ya kulinganisha tanzania na marekani.
GDP ya USA ni aprox $15 Trillion (2011)
GDP ya Tanzania aprox $23 billion (2011)
Tanzania hatujafika hata $1 trillion! Hiyo robo anayoongelea ni ipi?
hili ni tatizo kubwa zaidi ya tunavyodhani maana tayari kuna mawazo kuwa tuwaheshimu wakongwe, wazoefu, wanausalama na mengine kama hayo. Tunachosahau ni kuwa hawa watu wana uzoefu wa kuharibu ambao kimsingi umetufikisha hapa tulipo na kwa bahati mbaya hawataki kuambiwa lolote kwa vile wanaelewa kila kitu ati!
Juzi nilikuwa sehemu na alikuwepo mzee mmoja ambapo kimuonekano ni dizaini ya mzee Rutaraka, alipita bibi mmoja na watu wakawa wanabiishana juu ya umri wake basi ndio huyo mzee akaanza kuelezea jinsi alivyokuwa Ros Angels mwaka 2003 na akaona kwenye tv mtu mmoja aliyeishi wakati wa Abraham Lincoln akiendesha baiskeli. Basi watu waliposikia ndio wakabisha na kukataa kuwa ulikuwa uongo maana mtu huyo atakuwa ameishi zaidi ya miaka 200.
Natoa huo mfano huu maana hawa wazee mwishoni mwa siku ndio huwa wanaamua mustakabali wa maisha yetu na hizo akili zao za kinyume nyume badala ya kutuachia sisi kuamua huku wakitushauri.
amesisitiza kuwa uchumi Wa Tanzania sasa ni robo ya uchumi Wa marekani.
Mkuu safi sana kwa mfano huu! Najua tu tutafika tu lakini tukiwa hoi bin taaban, yaani hatujitambui kabisa!Ni muhimu CCM na Makada wake watambue kuwa mapato ya Kampuni moja tu ya Marekani ya amazon.com kwa mwaka 2011 ni USD 48.08 bn. Hii ni zaidi ya mara mbili ya GDP yetu kwa mwaka 2011.
Namkumbuka mzee huyu enzi hizo kichwa kikubwa lakini mbumbumbu hata ubunge ulimshinda ..chezeya S.Kinyondo.. R.I.P!!
hawa watawala wamefikiri na kuongea sana uongo mpaka vichwa vyao sasa vimejaa uongo na hawaweza hata kutofautisha pale unapotakiwa uongo au ukweli maana wanajua uongo ndio 'chakula' ya watanzania!labda anajua dola moja ni sawa shilingi 400