RUTALAKA: Sasa tumefikia robo ya uchumi Wa Marekani

RUTALAKA: Sasa tumefikia robo ya uchumi Wa Marekani

sishangai maana ukiwa CCM akili zako huwa zinawekwa mfukoni. halafu unatumia uji kuongea na kutoa hoja

Hahaaa wapi daud mchambuzi , analijua hili vizuri!
Yaani lazima uondoe ufahamu ndio uitetee ccm!
 
Huyu ni kada mkongwe wa CCM. Hiki ni kipimo kizuri cha fikra na upeo wa mambo ndani ya CCM. Huyu mzee, kada wa CCM hana taarifa sahihi, ana tatizo la kutumia uzoefu! Mawazo mgando! Ndugu yangu, huna haja ya kulinganisha tanzania na marekani. Marekani ni taifa kubwa mno kupita maelezo lilianza zaidi ya miaka 200 iliyopita hivyo ni kutokuwa makini na inawezekana ndiyo mtindo wa CCM kuwapumbaza watanzania. Huwezi kulinganisha Mike Tyson na Rashid Matumla! Kuna nchi kama Indonesia, Malaysia au Korea ya Kusini na kasikazini zilikuwa na uchumi sawa na tanzania wakati tunapata uhuru. Sasa hivi mataifa haya ukilinganisha na tanzania unaweza kutokwa na majozi na kukata tamaa ya maisha. Nchi hizi sasa zinakimbizana na mataifa makubwa ya ulaya ya europa na marekani! Ni CCM yenye mawazo mgando inayojua kushinda kwa kishindo tu kama mzee Rutalaka waliotufikisha hapa pomoja na utitili ya rasilimali tulizojariwa na mwenyezi mungu. Taifa letu limekwama kwa kuongozwa na chama wasio na mawazo mapya na badala yake wametumbukia katika shimo la kila mwenye madaraka ndani ya CCM na serikali yake wanashindana kujilimbikizia utajiri wao na washirika wao. Tanzania ilipofikia na viongozi tuliona nakumbuka usemi wa mwanafalsafa bora dunia Albert Einsten alisema hivi: "We can't solve problems by using the same kind of thinking (CCM) we used when we created them". Taifa hili lipende lisipende ili lipate mwelekeo sahihi kutoka hapa tulipo linahitaji mawazo mapya, new kind of thinking to solve the existing and future challenges. CCM MUST STEP DOWN IN 2015!!!!!

Aiseee!!! Ndg Butungo, ebu skiliza hii hotuba ya Rev Msigwa ikupe changa moto:

Last edited by a moderator:
yani hata Mimi nawashangaa Hawa Star tv huyu mzee wanampenda sana, maana anapata sana mialiko Yao.

Inawezekana mialiko ikamkithiri mzee Rutalaka shauri tu ya uhaba wa wachambuzi wa masuala ya siasa jijini Mwanza, hebu ninyi Star nitupieni mialiko muone umahiri wa mambo uwavyo.
 
Km mwigulu ndo naibu katbu mkuu ccm,unategemea logical&factual speech?!magamba kwisha kazi!
 
(Mwana ccm mkongwe, Rutalaka) amesisitiza kuwa uchumi Wa Tanzania sasa ni robo ya uchumi Wa marekani.
Mwenyekiti wake alishatamka hajui ni kwanini sisi ni maskini..kwa lugha nyepesi tunaye mtegemea atufikishe kwenye hiyo robo hajui ni wapi pakuanzia
 
Huyu ni kada mkongwe wa CCM. Hiki ni kipimo kizuri cha fikra na upeo wa mambo ndani ya CCM. Huyu mzee, kada wa CCM hana taarifa sahihi, ana tatizo la kutumia uzoefu! Mawazo mgando! Ndugu yangu, huna haja ya kulinganisha tanzania na marekani.
hili ni tatizo kubwa zaidi ya tunavyodhani maana tayari kuna mawazo kuwa tuwaheshimu wakongwe, wazoefu, wanausalama na mengine kama hayo. Tunachosahau ni kuwa hawa watu wana uzoefu wa kuharibu ambao kimsingi umetufikisha hapa tulipo na kwa bahati mbaya hawataki kuambiwa lolote kwa vile wanaelewa kila kitu ati!
Juzi nilikuwa sehemu na alikuwepo mzee mmoja ambapo kimuonekano ni dizaini ya mzee Rutaraka, alipita bibi mmoja na watu wakawa wanabiishana juu ya umri wake basi ndio huyo mzee akaanza kuelezea jinsi alivyokuwa Ros Angels mwaka 2003 na akaona kwenye tv mtu mmoja aliyeishi wakati wa Abraham Lincoln akiendesha baiskeli. Basi watu waliposikia ndio wakabisha na kukataa kuwa ulikuwa uongo maana mtu huyo atakuwa ameishi zaidi ya miaka 200.
Natoa huo mfano huu maana hawa wazee mwishoni mwa siku ndio huwa wanaamua mustakabali wa maisha yetu na hizo akili zao za kinyume nyume badala ya kutuachia sisi kuamua huku wakitushauri.

GDP ya USA ni aprox $15 Trillion (2011)

GDP ya Tanzania aprox $23 billion (2011)

Tanzania hatujafika hata $1 trillion! Hiyo robo anayoongelea ni ipi?

Ni muhimu CCM na Makada wake watambue kuwa mapato ya Kampuni moja tu ya Marekani ya amazon.com kwa mwaka 2011 ni USD 48.08 bn. Hii ni zaidi ya mara mbili ya GDP yetu kwa mwaka 2011.
 
hili ni tatizo kubwa zaidi ya tunavyodhani maana tayari kuna mawazo kuwa tuwaheshimu wakongwe, wazoefu, wanausalama na mengine kama hayo. Tunachosahau ni kuwa hawa watu wana uzoefu wa kuharibu ambao kimsingi umetufikisha hapa tulipo na kwa bahati mbaya hawataki kuambiwa lolote kwa vile wanaelewa kila kitu ati!
Juzi nilikuwa sehemu na alikuwepo mzee mmoja ambapo kimuonekano ni dizaini ya mzee Rutaraka, alipita bibi mmoja na watu wakawa wanabiishana juu ya umri wake basi ndio huyo mzee akaanza kuelezea jinsi alivyokuwa Ros Angels mwaka 2003 na akaona kwenye tv mtu mmoja aliyeishi wakati wa Abraham Lincoln akiendesha baiskeli. Basi watu waliposikia ndio wakabisha na kukataa kuwa ulikuwa uongo maana mtu huyo atakuwa ameishi zaidi ya miaka 200.
Natoa huo mfano huu maana hawa wazee mwishoni mwa siku ndio huwa wanaamua mustakabali wa maisha yetu na hizo akili zao za kinyume nyume badala ya kutuachia sisi kuamua huku wakitushauri.

Nina wasiwasi na uwezo wa kuchambua mambo kwa wazee kama Rutaraka kwa sababu ya kuishi kwa muda mrefu ndani ya mfumo wa chama kimoja. Sio kosa lao ni uelewa mdogo ndani mfuko mpya wa siasa za vyama vingi.
 
Pamoja na TV za kibongo kutangaza wanakwenda Digital bado sana, BBC wao watu wana enda hewani kwa tweety na FB live sasa kama mtu anaongea utumbo watu wanamchana live akiwa hewani siku nyingine akialikwa hawezi kwenda.
 
~~ unaweza kumwona mzee mkubwa, ana afya njema, kavaa kiafisa, na nywele nyeupe kuashiria japo busara, na anajua kakingereza.......

KUMBE HUKO KICHWANI NI MASABURI TU..... NA VIMA KIBAO..... wake 3 na UCHAFU MTUPU.....

So mm sinaga heshima na mzee au mtu yeyote akiongea KI MASABURI.....

Biblia inasema, mjinga mwelekeze na usimfanyie heshima kwani hata heshima hajui..... UKIMPA HESHIMA ANAONA WW MJINGA NA NDIO ATAKUWA ANAKUPUUZA....!!
 
Ni muhimu CCM na Makada wake watambue kuwa mapato ya Kampuni moja tu ya Marekani ya amazon.com kwa mwaka 2011 ni USD 48.08 bn. Hii ni zaidi ya mara mbili ya GDP yetu kwa mwaka 2011.
Mkuu safi sana kwa mfano huu! Najua tu tutafika tu lakini tukiwa hoi bin taaban, yaani hatujitambui kabisa!
 
Namkumbuka mzee huyu enzi hizo kichwa kikubwa lakini mbumbumbu hata ubunge ulimshinda ..chezeya S.Kinyondo.. R.I.P!!
 
Namkumbuka mzee huyu enzi hizo kichwa kikubwa lakini mbumbumbu hata ubunge ulimshinda ..chezeya S.Kinyondo.. R.I.P!!

Tatizo lake anafikiri bado ni enzi zile za zidumu fikra sahihi za mwenyekiti. Ukimsikiliza kwa makini utagundua kama vile hatambui huwepo wa vyama vya upinzani hapa nchini! Binafsi sina tatizo na mwenendo wa sasa Startv wa kushiriki kwa makusudi kuwaficha watz ukweli na taarifa sahihi eti kwa sababu mmiliki wake ni kada wa ccm. Lakini startv pamoja na waandishi wake wa habari watambue kuwa watahukumiwa na mungu kwa kutosema ukweli na kutumika kama chombo cha uzushi na propaganda ilimradi watawala wa ccm waendelee kuitawala nchi japo ni dhahiri chama hiki kimeleta madhira makubwa kwa watz. Chama kimeua elimu ya watoto wetu, chama kimeua mshikamano miongoni mwa watz kwa kuruhusu watu kushabikia mambo ya kidini, makabila, ukanda tofauti na miaka ya 80. Huu ni wakati wa watz wenye kupenda nchi yao kushikamana na kutetea nchi yao. Imekuwa dhahiri sasa baadhi ya watawala na watu wenye mapesa na hasa wamiliki ya vyombo vya habari wameamua kujiunga pamoja ili kulinda masilahi ya wachache na kuwaficha watz ukweli wa mambo.
 
labda anajua dola moja ni sawa shilingi 400
hawa watawala wamefikiri na kuongea sana uongo mpaka vichwa vyao sasa vimejaa uongo na hawaweza hata kutofautisha pale unapotakiwa uongo au ukweli maana wanajua uongo ndio 'chakula' ya watanzania!
Na ndio maana wamekuwa waki-inflate gharama za miradi wakijua hakuna atakayejua mpaka sasa Wamakonde/Watanzania wameamua kuamka juu ya gesi. Ngoja tuone kama hawajafutika kwenye historia kama waongo wengine

Back
Top Bottom