Ruth Zaipuna: Mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa juu kwenye benki Tanzania

Ruth Zaipuna: Mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa juu kwenye benki Tanzania

Kuna mama mmoja alishawahi kuwa CEO wa EXIM Bank some years back! Kwahiyo, huyu sio wa kwanza
Kuna mwingine anaitwa Sabetha Mwambenja, ni mwanzilishi na CEO wa Covenant Bank. Labda Ruth ni mwanamama wa kwanza kuwa mkurugenzi mkuu wa NMB, sio wa benki kama benki.
 
Wakurugenzi watendaji wanawake wa benki walikuwepo huyu sio wa kwanza.
Sabetha Mwambenja Exim nadhani kutoka 2001 to 2010,Magrareth Chacha Tanzania Women Bank 2013 to 2016 na Jacquiline Woiso Bank M nadhani 2015 to 2017 au 18. Labda hapa issue ni kuwa CEO wa benki kubwa kuliko zote kwa mali,mikopo,faida etc. Ila hongera zake maana Rabobank wanahisa wakubwa wa nmb always walikuwa wanataka MD awe Mholanzi. Tumuombee afanye kazi nzuri nadhani anaweza.

Mwanahiba Mohammed amewahi kua MD Ecobank Tanzania. (2017 - 2020)
 
mkuu mshahara milioni 60 na malupulupu kibao so kwa mwezi hakosi milioni 100 ila matumizi yanakua makubwa so mshahara unakua bado hautoshi manake kama watoto walikua wanasoma feza atataka awapeleke london huko

Ofisi inawalipia fees kwenye taasis yeyote hapa duniani mkuu. CEO NMB ni level nyingine mkuu!
 
Mwenyekiti wa bodi ya NMB Bank, Dkt. Edwin Mhede, amemteua Ruth Zaipuna kuwa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB kuanzia leo, Agosti 18.

Ruth anakuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi kubwa katika taasisi za kibenki nchini. Awali Ruth aliikaimu nafasi ya Ukurugenzi Mkuu tangu Oktoba 2019.

Ruth ana Shahada ya kwanza ya Biashara ya Uhasibu na pia ana Masters of Business Administration (MBA) katika Fedha na zote alizipata Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam. Pia ana CPA (T)

Ruth amewahi kufanya kazi na mashirika mbalimbali ikiwemo Price Waterhouse Coopers Limited (PwC), aliwahi kuwa Mkurungenzi mkuu wa Standard Chartered kabla ya kujiunga NMB Bank

====

View attachment 1540990
Beaultiful and by appearance, very smart as well. Utadhani ni Air Hostess wa KLM. Muonekano wa nje tu unatosha kukupa hint kwamba the lady must be very smart upstarirs! Mungu azidi kumbariki sana pamoja na wajukuu zangu wote alionao nyumbani kwake
 
Back
Top Bottom