Ruto anaunga mkono busara za Magufuli

Ruto anaunga mkono busara za Magufuli

Ni kweli hajapiga marufuku lakini mtazamo wake ndo unaoendana na Magufuli. Mtazamo wa kwamba kuna wakati wa siasa na wakati wa kazi. Na kwamba wakati siasa ukiisha siasa inatakiwa zikome ili waliochaguliwa wafanye kazi.
Ukisema siasa zikome inamaanisha na wanasiasa wakome. Rais mwenyewe ni kiongozi wa kisiasa. Shughuli za siasa haimaanishi mikutano pekee yake.

Chama kilichopo madarakani kitawezaje kuipima Serikali yake inavyofanya kazi kama shughuli za kisiasa zikisimama? Vyama vya siasa vitawezaje kuikosoa Serikali iliyopo madarakani kama shughuli za siasa zikisimama?

Usahihi ni kwamba, Serikali ifanye shughuli zake, vyama vya siasa vifanye shughuli zao, watendaji wa Serikali wafanye kazi zao. Wanasiasa nao wafanye kazi zao. Shuguli za siasa zinapofanywa kwa mujibu wa sheria, hazizuii Serikali iliyopo madarakani kufanya kazi zake. Niambie ni kwa namna gani mkutano wa hadhara unaofanyika leo na CUF Mtwara au Dodoma, uramzuia Rais asitimize wajibu wake, au mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam au Dodoma ashindwe kufanya kazi.

Mara nyingi viongozi wale wasiotimiza wajibu wao au wanaofanya maovu, ili mapungufu yao yasionekana na wala kusiwepo na wa kuyasema, ndio ambao huwa wanazuia shughuli za vyama vya siasa, uhuru wa vyombo vya habari, na hugandamiza demokrasia.
 
Ndiyo bado tupo tunaojiuliza Mh Mbowe kama mbunge kwanini alishindwa kufanya mikutano katika jimbo lake, ambako kuna wananchi wake waliomchagua ila akawa anang'ang'ana na Dar? Je! Hakukuwa na haja ya kuwasikiliza wananchi wake? Wapiga kura wake hawakuwa na changamoto zozote?
Ndugu yangu, nadhani kuna kitu hakipo sawa upande wako. Ina maana huelewi kama Mh. Mbowe ni kiongozi mkuu wa kitaifa wa CHADEMA, na eneo lake la kazi ni eneo lote la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Uliskia alitaka kufanya mkutano Dar kama mbunge wa Hai? Panua uelewa wako.
 
Sababu ulizoweka hapa hazijitoshelezi kueleza kwanini katika jimbo lake hakutaka kufanya mikutano na wananchi wake waliomchagua! Labda uniambie wapigakura wake hawakuitaji mikutano cos walishajutosheleza na hawakuwa na changamoto zozote
Panua uelewa wako.

Uliwahi kumsikia Mbowe anataka kufanya mkutano Dar kama mbunge wa Hai?

Una uhakika Mbowe kama mbunge hakuwa anafanya mikutano kwenye eneo la jimbo lake?

Jambo la muhimu ni Katiba na Sheria.

Aliyezuia mikutano ya vyama vya siasa alikiuka katiba hakukiuka? Aliyezuia mikutano ya hadhara kwa vyama vya upinzani, hayo mamlaka aliyatoa kwenye eneo gani la katiba? Vyama vya siasa vilivyotaka kufanya mikutano ya hadhara, wana haki hiyo kisheria na kikatiba au hawana haki?

Mengine yote ni porojo.
 
Ndugu yangu, nadhani kuna kitu hakipo sawa upande wako. Ina maana huelewi kama Mh. Mbowe ni kiongozi mkuu wa kitaifa wa CHADEMA, na eneo lake la kazi ni eneo lote la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Uliskia alitaka kufanya mkutano Dar kama mbunge wa Hai? Panua uelewa wako.
May be ila kitendo chawewe pia kutojali mahitaji ya wapiga kura wake wa Hai kinatia warakini maana wao ndiyo waliokampa dhamana yakwenda huko Bungeni.

Mara ngapi sisi wananchi tumelalamikia wabunge wetu kwenda kuishi Dar huku wakitulekeza wapiga kura wao? Leo hii iweje kwa Mh Mbowe ionekane ni sawa? Kwa style hii basi Rasimu ya 2 ya Warioba itapingea na wote! Sio wanaCCM sio Wapinzani wote hamuitaki.
 
Kutoka tovuti ya Nation:

Huku kwetu bahati mbaya busara hii ya kutenga muda wa siasa na muda wa kazi imeonekana haina maana. Kampeni zisizokwisha zinaungwa mkono sasa.

View attachment 2497913
Nimelazimika kuweka hizi Paragraph chache ili wale Chadema wanasema wanaiga mambo ya demokrasia ya Kenya...kwamba waige na hii....

President William Ruto has rubbished comments by opposition leader Raila Odinga that he does not recognise his government, saying he is Kenya’s only Head of State and is focused on developing the country.

"Let me inform those who still want to take us back to politics that the time for politicking is over. They should allow me to plan this job because they were defeated and could not do it (win the elections),” he said.

He wondered why opposition chiefs were asking suffering Kenyans to attend their rallies and demonstrations.

Poor Kenyans

“Your children are in parliaments in Arusha yet you want the children of the poor Kenyans to come for riots in Kamukunji and Jacaranda grounds? We will follow the path of development and not that of exchanging words,” said President Rutto"
 
Sio Ruto tu, Afrika yote itafuata busara za JPM. Bara la Afrika litainuka kiuchumi kwa kufuata alichoanzisha mwamba JPM. Pumzika kwa amani BABA JPM.
 
Kuna kitu bado najiuliza!
2016 ni kweli Rais Magufuli aliweka zuio la kufanya mikutano ya siasa kiholela! Kwa maana kila mbunge afanye kwenye eneo lake la utawala sio nje ya eneo lake, ila sasa ilikuwaje mtu kama Mh Mbowe asifanye ata mikutano mi10 tu pae Hai kwenye jimbo lake ila mwisho wa siku ndani ya miaka 5 alifanya mikutano miwili tu ila akawa anataka kuja Dar kufanya mikutano ya kisiasa?

Kwanini Dar na sio Hai? Mbona Msigwa alifanya sana mikutano katika jimbo lake?
Ndivyo katiba inavyosema !?! Au ni katiba ya mzirankende inavyosema !!!?? Je vyama visivyo na wabunge na madiwani vitafanyeje mikutano yake??! Yaani mambo mengine ni ushamba na ulimbukeni wa kimadaraka tu . .. katiba inasema hv lkn kwakuwa amepakia makasi kichwani yy anakuja na Sheria za kikamasi kamasi
 
Ndivyo katiba inavyosema !?! Au ni katiba ya mzirankende inavyosema !!!?? Je vyama visivyo na wabunge na madiwani vitafanyeje mikutano yake??! Yaani mambo mengine ni ushamba na ulimbukeni wa kimadaraka tu . .. katiba inasema hv lkn kwakuwa amepakia makasi kichwani yy anakuja na Sheria za kikamasi kamasi
Hiyo mliyokapewa mlifanya? Si mlikumbia kwenye majimbo yenu kutwa mko Dar ndo mnawahamasisha waandamane!
 
Ndivyo katiba inavyosema !?! Au ni katiba ya mzirankende inavyosema !!!?? Je vyama visivyo na wabunge na madiwani vitafanyeje mikutano yake??! Yaani mambo mengine ni ushamba na ulimbukeni wa kimadaraka tu . .. katiba inasema hv lkn kwakuwa amepakia makasi kichwani yy anakuja na Sheria za kikamasi kamasi
Katiba unaijua, au unasimuliwa tu?

Hakuna ibara ya katiba inayoongelea mikutano ya vyama vya siasa.

Mambo mengine ni busara tu. Uchaguzi umeisha, ulikuwa wa moto sana, watu wameshambuliana kwa kila namna... halafu unataka mikutano ya siasa iendelee baada ya uchaguzi ili ugundue nini haswa?
 
Magufuli hakuwahi kuwa na Busara yoyote
On the contrary Magufuli was a mentally deranged person. Mwaka 2015 TISS walifanya kazi yao vizuri ila Waziri wa Utawala Bora Chikawe alificha faili linaloonyesha kuwa Magufuli alikuwa na kichaa, hakulifikisha Kamati Kuu ya CCM. Na zawadi ya Chikawe ilikuwa ni kupewa Ubalozi
 
Back
Top Bottom