Aliyekuwa waziri mkuu nchini Kenya Raila Odinga ametangaza kwamba atagombea urais katika uchaguzi mkuu ujao nchini humo mwaka wa 2022. Alitoa tangazo hilo katika kongamano la Azimio la Umoja siku ya Ijumaa. "Ninatangaza kwamba ninakubali kujiwasilisha kama mgombeaji urais," Raila alisema...