Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
William Ruto rais aliyethibitishwa na mahakama baada ya mpinzani wake kugomea matokeo yuko hatarini kuangushwa kabla hata ya kumaliza kipindi chake cha kwanza. Ameanza na papara huku akijua fika kuna majeraha mengi ya kuponya kwanza.
Kwa haiba na hulka Ruto ni mbepari si mjamaa, tajiri mkubwa Kenya na pengine Afrika, anamiliki mali nyingi mpaka unajiuliza kwanini akautaka urais.. Ila kwa hulka za bidanamu keshapata kila kitu sasa anachosaka ni ukuu na mamlaka.
Ushindi wake ni mwembamba kwahiyo kuna nusu nzima ya wapiga kura wanaowawakilisha Wakenya mamilioni ambao hawakumchagua ama hawampendi.. Hawa ndio wa kupetipeti kwa sasa.. Asikomaze shingo! Itavunjika mara.
Huku kwetu mwendazake alishinda kwa taabu sana kiuhalisia ukiachana na ule wizi mkubwa wa kura, na inasemwa kama uchaguzi ungekuwa huru na haki angeangukia pua parefu sana! Ni katika panic na,hasira ya kugundua kutokubalika alifanya ambayo aliyafanya ya kuudhibiti upinzani kwa mkono wa chuma.. Kilichotokea baada ya hapo kimebaki kwenye vitabu vya kumbukumbu.
Ruto ana vinasaba vingi vya mwendazake lakini sasa Kenya sio Tanzania, kule hakuna wapole,waoga na makondoo kams huku kwetu na kila kinachofanyika kule kinaangaliwa kwa macho haya matatu.
Jicho na mtazamo wa kisheria
Jicho na mtazamo wa kiimani/kidini
Jicho na mtazamo wa kikanda na kikabila
Jinsia haina nguvu sana Kenya kuliko hayo matatu, Chochote atakachofanya kitajengewa hoja zenye nguvu sana kwenye hayo mambo matatu.
Chaguzi hasa hizi za kiafrika zina gharama kubwa na mara nyingi hufilisi hifadhi ya pesa za nchi. Kenya sio exclusive. Uchaguzi umeisha nchi haina hela na matarajio ni makubwa huku wa kuwashukuru ni wengi.
Katika hali tete kama hiyo inahitaji bongo yenye utulivu na werevu mkubwa kuweza kudhibiti bila tafrani mpaka pale mambo yatakapotulia! Je Ruto ana uwezo wa kufanya hivyo? Tuupe muda wakati! Utasema kwa sauti!