Kenya 2022 Ruto: Nina miezi sijazungumza na Rais Kenyatta

Kenya 2022 General Election

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Rais mteule wa Kenya, William Ruto ameweka wazi kuwa hajazungumza na Rais Uhuru Kenyatta kwa miezi sasa huku akiahidi kuwa atampigia simu kuzungumza naye.

Ruto amesema hayo muda mfupi baada ya Mahakama ya Juu nchini Kenya kutupilia mbali maombi ya kikatiba yalifunguliwa wiki iliyopita na mgombea aliyeshindwa, Raila Odinga kupinga ushindi wa Ruto.

Akitoa uamuzi wa hukumu hiyo huo leo Jumatatu Septemba 5, 2022, Jaji Mkuu Martha Koome amesema Raila na waleta maombi wenzake wameshindwa kuthibitisha kuwa kulikuwa na udanganyifu na uchakachuaji wakati wa mchakato wa kuelekea uchaguzi, siku na baada ya kupiga kura.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya uamuzi huo wa mahakama, Ruto ameweka wazi kuwa hajazungumza na Rais Kenyatta kwa miezi sasa.

“Nina miezi sasa sijazungumza naye lakini nitampigia rafiki yangu Rais Uhuru Kenyatta tuzungumze” amesema Ruto huku akicheka.

Rais Kenyatta alikuwa anamuunga mkono Odinga katika kampeni za uchaguzi huo uliofanyika Agosti 9 mwaka huu.
 
Siasa sio uadui....teh teh teh 😂 😂😂
MK254 pingli-nywee Tony254

Ndio maana huwa naziepuka sana siasa, kitambo nilikua natokwa povu na kupandisha msukumo wa damu kwa mihemko ya siasa.
Utajikuta unazozana na watu kisa kumshabikia mtu anayetafuta uongozi ili akaupige mwingi, baadaye wanaungana huko juu juu kivyao.
Yaani mpaka huu uchaguzi umeisha bila ya mimi kuleta humu uzi wowote unaomshabikia yeyote.
 
Upo Kenya, Tanzania au Ukraine?
 
Hana jinsi ya kufanikiwa kama Rais wa 5 kama hatatafuta suluhu na Uhuru na Odinga. Huo ndio ukweli mchungu. Ataikumbuka hand shake anayoibeza leo. Uzuri Wanasiasa hawakuumbiwa haya muda si mrefu atafanya handshake kwa jina lingine ila maudhui yaleyale.
 
Hand shake haipoo
 
Huenda hawajawahi kuwa maadui.
 
Utajikuta unazozana na watu kisa kumshabikia mtu anayetafuta uongozi ili akaupige mwingi, baadaye wanaungana huko juu juu kivyao.
Hatari kweli kweli, hawa wanasiasa ni wapiga dili wanaofahamiana.
 
Bifu la Uhuru na Ruto ni real kabisa. Uhuru amegoma kumpongeza Ruto moja kwa moja .
 
Hand shake haipoo

Walibana na Uhuru wakaachia kwa Raila. Ruto akapigwa chini awamu ya pili ya Uongozi wa Uhuru. Akawa Naibu wa Rais koti tu. Narudia the 5th hawezi fanikiwa kama Rais wa Kenya kama hatatafuta namna ya kuyajenga na Kenyatta, Odinga na Moi families. Hawezi iendesha nchi ya Kenya kwa kumtegemea Gachaua ni kujidanganya na kujilisha/kujijaza upepo tu.
 
Aaah wapi!!! The 5th anatakiwa akae chonjo na ajue next move ya Uhuru itakuwa ipi?
Ile ni nchi siyo kikoba boss. Mambo hayatokei kama suprice yanapangwa kisha maigizo ya siasa yanafata. Machafuko hutokea pale wapangaji wanapotofautiana au kunapokosekana details za kutosha ambazo zinaweza tumika kuzuia machafuko.
 
Urais unaweza kuwa ndoano yenye chambo umeze ikukwamie kooni na biashara iishie hapo. Lolote lawezekana chini ya jua. RIP JPM.
 
Ndoano pale unapotaka kuunda kamfumo kako kapya na kakikundi kako kadogo ambacho si sehemu ya system inayokupa madaraka. Kuhamisha control system ya nchi si jambo rahisi. Wananchi wanakupa kura na uraisi, ila mfumo unakupa mamlaka. Wananchi wao wanaweza mpa yoyote uraisi ila madaraka ya uraisi kuna mfumo ambao unakuwezesha kuyapata. Kupigana na mfumo ni kutaka kuwa raisi jina au kutokuwepo.
 
Umesema vizuri. Kuna mfumo Kenya unaweza kupuuza familia ya Kenyatta, Odinga, Moi and the likes eti wawe replaced na watoto wa mama mbogamboga na bodaboda. Kama huo si ujinga utaita nini? The 5th mwenyewe si kasema jana isingekuwa juhudi za Raila kusingekuwa na Demokrasia ya yeye kuwa Rais. Ama atakataa hakushikwa mkono na Moi katika hatua flani ya maisha yake na ndio masna leo ni the 5th na kwa vile ni Kalenjii mwezake. Leo ajifanye kusahau hayo yote na kujidanganya na kauli ya hustula nation.
 
uhuru.jpeg

Hapongezwi mtu hapa. Kenya polarized like north pole and south pole - 7 million against a disgruntled 41 million.
 
Hata huyo mwanasheria aliyekengeuka nahisi alishauriwa na Uhuru.

Heko Ruto.
 
Umesma vizuri. Kuna mfumo Kenya unaweza kupuuza familia ya Kenyatta, Odinga, Moi and the likes eti wawe replaced na watoto wa mama mbogamboga na bodaboda. Kama huo si ujinga utaita nini? The 5th mwenyewe si kasema jana isingekuwa juhudi za Raila kusingekuwa na Demokrasia ya yeye kuwa Rais. Ama atakataa hakushikwa mkono na Moi katika hatua flani ya maisha yake na ndio masna leo ni the 5th na kwa vile ni Kalenjii mwezake. Leo ajifanye kusahau hayo yote na kujidanganya na kauli ya hustula nation.
Uhuru support for Raila ni genuine. Mambo yalivyo mkikuyu na mkalenjini wanatawala Kenya miaka mingine 20, jambo ambalo Uhuru hafikiani nalo: Ruto miaka 10,Gashagwa miaka 10. Jumla makabila mawili yanaelekea kutawala Kenya zaidi ya miaka 80 kwa staili ya kupokezena.
 
Principled Uhuru and Raila will make a formidable opposition- the battle line has been drawn.
 
Ndoano pale unapotaka kuunda kamfumo kako kapya na kakikundi kako kadogo ambacho si sehemu ya system inayokupa madaraka. Kuhamisha control system ya nchi si jambo rahisi. Wananchi wanakupa kura na uraisi, ila mfumo unakupa mamlaka. Wananchi wao wanaweza mpa yoyote uraisi ila madaraka ya uraisi kuna mfumo ambao unakuwezesha kuyapata. Kupigana na mfumo ni kutaka kuwa raisi jina au kutokuwepo.
Mfano JPM
 
Back
Top Bottom