Kenya 2022 Ruto vs Odinga Agosti 9/2022

Kenya 2022 General Election
Huu ni upumbavu au kitu gani. Kumtusi Rais ni kipimo cha kukomaa kisiasa? Tangu lini matusi yakawa ukomavu kwenye tribalist shithole?
It may look stupid yes but it shows how our democratic space has grown in comparison to most African states, Tanzania included
 
Me nimeanza kufuatilia siasa za Kenya tangu 2007,nimegundua hili jukwaa watanzania hamjui siasa za kenya mnabahatisha tu.
Siasa za kenya ni siasa za Afrika mashariki na Aftika kwa ujumla.
Kenya sio kisiwa......lazima ufahamu kuwa Uchaguzi wa kenya ni muhimu pia kwa mustakbali wa Tanzania na Uganda..........
 
#VOTE YELLOW 🍌🍌🍌 for healthy and better life🍻Hustler ndio form!!!
 
Ruto anashinda hii Ngoma....dakika za Mwisho amempata mtu anaeitwa SONKO....Ile ni mashine hatari sana....jamaa ana ushawishi ni balaa....anakusa ya Kijiji kama chote....Mombasa, Nairobi, ukambani kote Sonko anasomba Kijiji kinampigia Ruto.Jamaa kaingia juzi upepo umebadilika gafla. Yule mzee hata bahati na mabaya zaidi mlima Kenya hauko upande wake na mbaya zaidi kamteua mtu ambae watu wa mlima Kenya ( wakuyu) hawaoni future.Wakikuyu wanaamini wao ndo tabaka linalozaa viongozi wa nchi na wako tayari kuzichapa ili mradi wasitawaliwe na mtu yoyote. So hili ndo kosa la uhuru kumteua Raila instead of another candidate kutoka mlima Kenya. Na anavozidi kumpigia debe Raila ndo anamharibia zaidi Bora anguchuna tu.
 
Kivip sas asimame
 
Miaka ya hapo awali nilikuwa shabiki mkubwa sana wa hizi siasa zetu. Ila kwenye uchaguzi huu sina habari, hata za wanaowania nafasi ya ubunge, achia mbali ugavana, useneta na MCA(diwani), kwenye eneo bunge/wodi/gatuzi ambalo nilijisajili zamani kupigia kura. Sasa hivi wakimuapisha hata ngendere kama rais sitojali, wala haitanipa presha.

Kwenye haya maisha kila kitu huwa kama ngazi fulani hivi, 'stage', moja baada ya nyingine. Ambazo sijui kwanini, lakini kwangu mimi, nikizipita huwa sina hamu kabisa ya kuzirudia rudia. Nakumbuka enzi hizo nikiwa fresh from campus, nikifanya 'tarmaking'. Huku part time nafanya 'volunteering' na NGO flani jijini Nairobi, kazi bila malipo. Sina hela mfukoni, zero savings kwenye acc. yangu benki, sina mali, sijaoa.

Kisha jamaa fulani hivi, tajiri mashuhuri maeneo ya Westands, akatupa kazi ya kumfanyia kampeni. Mimi na wenzangu kama 10 hivi, tulokuwa pamoja nao chuoni. Kila mara tukawa tunaketi kwenye 'vikao' naye, vya kumpa 'updates', tena ndani ya vilabu mbalimbali jijini. Baada ya kazi nzito ya kumfata fata kwenye mikutano, tukimpigia debe na kuwatusi wafuasi wa wapinzani wake.
Alafu 'Mheshimiwa' akiondoka anaacha hela kwenye counter, ili tuzidi kulewa na tusahau kabisa kumuitisha mishahara yetu. 😄😄😄
Yaani nikikumbuka enzi hizo huwa nakiri kwamba Mungu ni mwema sana.

Wakenya wenzangu timizeni wajibu wenu inavyostahili, ila nawasihi muifanye kwa amani. Kwenye sekta hiyo nakubali kwamba uchaguzi huu nimefeli na nimewaangusha sana, kama mwananchi mwenzenu. Ila hamna namna na nipo tayari kabisa kumkubali mtakayemchagua nyie, kwa niaba yangu.
 
Wewe bora unyamaze tu. The moment nimeona ukisema Sonko anacontrol kura za ukambani, Nairobi na Mombasa hapo ndio nikajua hujui unachosema. Siasa/kura za Ukambani yapo mikononi mwa Kalonzo na amekuwa akizincontrol kwa muda mrefu sana. Ndio maana Odinga na Ruto walijaribu sana kumsawishi Kalonzo ajiunge na timu zao ila mwishowe ni Odinga ndiye aliwezakumshawishi zaidi. Huo muda wote Ruto na Raila hawakushugulika na Sonko kwa sababu walijua mahali kifunguu ya kura ya ukambani ilipo!

Siasa za Nairobi nazo zimekuwa ni za Odinga tangu 2002. Kibaki hakuwahishinda Raila Nairobi 2007. Uhuru na Ruto pia hawakufaulu kumshinda Raila Nairobi kwa chaguzi zote mbili za 2013/17. Sasa Sonko ndio awe maarufu Nairobi kuwashinda Kibaki, Uhuru na Ruto ambao wote Raila amewalemea Nairobi?

Mombasa kwa sasa ipo chini ya Hassan Joho, na kabla yake alikuwa ni Balala. Sonko hana kura kule wala hatambuliki kule kwa hivyo usidanganywe na mtu

Nimegundua watanzania wengi sana hapa huvutiwa na siasa za Kenya ila wengi pia hawaielewi, ni kuongea tu.
 
Sonko pia ameenguliwa kwenye kinyang'anyiro cha ugavana huko Mombasa amebaki na biashara ya sembe tu. DEBE TUPU
 
Sonko pia ameenguliwa kwenye kinyang'anyiro cha ugavana huko Mombasa amebaki na biashara ya sembe tu. DEBE TUPU
Huyo jamaa amenifanya nicheke sana alipotaja Sonko. Yani kama kuna mtu hana influence yoyote iwe ni Mombasa, Nairobi ama ukambani ni yeye sasa. Ukambani ni ngome ya Kalonzo, Mombasa ni ya Joho nayo Nairobi kwa kiasi kikubwa ni Odinga
 
Huyo jamaa amenifanya nicheke sana alipotaja Sonko. Yani kama kuna mtu hana influence yoyote iwe ni Mombasa, Nairobi ama ukambani ni yeye sasa. Ukambani ni ngome ya Kalonzo, Mombasa ni ya Joho nayo Nairobi kwa kiasi kikubwa ni Odinga
Sure, Sonko labda influence imebaki kwa wanunuzi wa sembe lake. Na US wamemlima ban yeye na familia yake. Atulie tu aongeze mateja
 
Sure, Sonko labda influence imebaki kwa wanunuzi wa sembe lake. Na US wamemlima ban yeye na familia yake. Atulie tu aongeze mateja
Sonko rides on fame, nothing much. Hana constituency of voters he can claim is his. Hana kabisa. Yani Sonko hata Joho anamshinda mbali sana kwa wafuasi. Sarakasi ndio zake yule jamaa
 
Mleta mada nimegundua unaokota okota tu vihabari na kwakuwa umejikuta unampenda Ruto basi unaona kila kitu kwake kiko sawa[emoji3]
nipo kenya na ninafuatilia vyema siasa.

angalia umoja wa "Kenya kwanza" unataswira ya umoja wa Taifa la kenya, hiyo ni nguvu tosha ya ushindi.
 
Afadhari mmekuja wenyeji mnaozijua vizuri siasa za Nchi yenu Kenya,Wabongo walishaanza kutudanganya hapa.Asante sana Mkuu kwa ufafanuzi wako.
 
Umeandika vizuri sana katika uchambuzi;

Ruto yupo well informed, anaeleza jambo kwa ufasaha sana.

Nilimsikiliza alipohojiwa katika kituo kimoja cha habari; interview ya saa 1 na anaulizwa maswali na yote aliyajibu vizuri sana.

Umri wake pia ni added advantage hasa kupata kura za watu wa umri wa kati.

Lakini nikakaa na kuona siasa za Afrika, ni lini Waafrika walimchagua mtu kuwa Rais kwa uwezo wake wa kujieleza au kwa kutumia umri?!

Kwa siasa za Afrika na kenya in particular, Mtu hawi Rais kwa sababu ya Uwezo wa kujieleza au umri. Mara zote sababu ni 1. Kabila 2. Kabila na Kundi alilopo mgombea Urais( Party Alliances).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…