Miaka ya hapo awali nilikuwa shabiki mkubwa sana wa hizi siasa zetu. Ila kwenye uchaguzi huu sina habari, hata za wanaowania nafasi ya ubunge, achia mbali ugavana, useneta na MCA(diwani), kwenye eneo bunge/wodi/gatuzi ambalo nilijisajili zamani kupigia kura. Sasa hivi wakimuapisha hata ngendere kama rais sitojali, wala haitanipa presha.
Kwenye haya maisha kila kitu huwa kama ngazi fulani hivi, 'stage', moja baada ya nyingine. Ambazo sijui kwanini, lakini kwangu mimi, nikizipita huwa sina hamu kabisa ya kuzirudia rudia. Nakumbuka enzi hizo nikiwa fresh from campus, nikifanya 'tarmaking'. Huku part time nafanya 'volunteering' na NGO flani jijini Nairobi, kazi bila malipo. Sina hela mfukoni, zero savings kwenye acc. yangu benki, sina mali, sijaoa.
Kisha jamaa fulani hivi, tajiri mashuhuri maeneo ya Westands, akatupa kazi ya kumfanyia kampeni. Mimi na wenzangu kama 10 hivi, tulokuwa pamoja nao chuoni. Kila mara tukawa tunaketi kwenye 'vikao' naye, vya kumpa 'updates', tena ndani ya vilabu mbalimbali jijini. Baada ya kazi nzito ya kumfata fata kwenye mikutano, tukimpigia debe na kuwatusi wafuasi wa wapinzani wake.
Alafu 'Mheshimiwa' akiondoka anaacha hela kwenye counter, ili tuzidi kulewa na tusahau kabisa kumuitisha mishahara yetu. 😄😄😄
Yaani nikikumbuka enzi hizo huwa nakiri kwamba Mungu ni mwema sana.
Wakenya wenzangu timizeni wajibu wenu inavyostahili, ila nawasihi muifanye kwa amani. Kwenye sekta hiyo nakubali kwamba uchaguzi huu nimefeli na nimewaangusha sana, kama mwananchi mwenzenu. Ila hamna namna na nipo tayari kabisa kumkubali mtakayemchagua nyie, kwa niaba yangu.