JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Rais Mteule wa Kenya, William Ruto amesema watu wengi walijiunga na Umoja wa Azimio kutokana na kupewa vitisho na sio kwa kupenda.
Amesema anafahamu hali hiyo iliwafanya wahamie upande mwingine lakini kwa kuwa sasa Mahakama imetoa uamuzi, basi wana uhuru wa kurejea au kwenda wanapotaka kwa kuwa Nchi ni ya Kidemokrasi.
Ruto amesema “Waliowatisha nilishawahi kuwaambia kuwa ipo siku hawatakuwa na nguvu kama waliyokuwa nayo ya kuwatisha watu, na sasa muda umefika wa watu kuwa huru.”
Ameongeza “Maamuzi ya Mahakama yanaashiria mwisho wa siasa za ulaghai, usaliti na ujanja... Mfumo wa haki ya jinai hautatumika tena dhidi ya wale wenye maoni tofauti ya kisiasa.”