Kenya 2022 Rutto wa Kenya anatumia mbinu za Hayati Magufuli katika kampeni za Urais, atashinda hakika

Kenya 2022 Rutto wa Kenya anatumia mbinu za Hayati Magufuli katika kampeni za Urais, atashinda hakika

Kenya 2022 General Election
Mbona huo ndio utamaduni wakati wa kampeni nchini Kenya? Yaani 'impromptu stops' za kuongea na wapiga kura sanasana kwenye miji midogo midogo na vijijini? Nilipoingia kwenye uzi huu nilitegemea kuona picha za DP Ruto akipiga zile push-up ndomboloo za mwendazake.
 
Hao wakenya ndio hovyo kabisa katika siasa na uchaguzi, wewe umeona wapi kiongozi wa siasa ni makamo mwenyekiti wa chama lakini ameanzisha chama kingine na ndiye mgombea wa hicho chama kipya, huku bado ni makamo mwenyekiti wa chama kingine?, Kenya hakuna siasa ila ni kila mtu kujitafutia maisha
Endelea kuwadanganya mapimbi wenzako. Huelewi chochote kuhusu sheria za vyama na miungano ya kisiasa nchini Kenya. Alichofanya DP Ruto ni kujihusisha tu na chama kipya. Bila ya kutangaza rasmi uanachama wake wala kwamba atakuwa mgombea urais wa chama hicho. Alafu DP Ruto alishafurushwa kwenye chama cha Jubilee. Kisa aliendeleza sera na maadili ya chama kingine.

Anaendelea kushikilia nafasi yake kama makamu kwasababu nafasi hiyo pamoja na ya bosi wake imelindwa kikatiba. Kumaanisha ili apokonywe nafasi hiyo ni lazima mswada wa 'impeachment' dhidi yake upitishwe bungeni na uungwe mkono na 2/3 ya wabunge wote. Kuwa na mazoea ya kufanya risechi kwanza, sio unaingiza tu ujuaji wako wa peni mbili kwenye masuala ambayo huyaelewi hata kidogo.
 
Back
Top Bottom