Kutokana na mvua kubwa zinazonyesha ukanda wa Morogoro na Selous, daraja kubwa la Mto Muhuwesi lililoko hapa Tunduru limejaa maji hadi juu ya daraja na kwa hiyo tumechukua uamuzi wa haraka wa kufunga barabara kuu ya Mangaka - Tunduru Mjini kwa muda. Eneo la barabara linalofungwa ni eneo la mto lililo kati ya kata za Muhuwesi na Majimaji.
Magari yanayotokea Mbeya, Iringa, Songea na Mkoa wote wa Ruvuma kuelekea Mkoa wa Lindi, Mtwara, Pwani na Dar yanapovuka Tunduru Mjini yapaki na kupumzika kusubiri hali iwe sawa Mto Muhuwesi. Magari hayo yanaweza pia kusimama/kupaki na kusubiria Sisi kwa Sisi au Muhuwesi Kijijini.
Magari yanayotokea mkoa wa Lindi, Mtwara, Pwani na Dar Es Salaam kuja Tunduru, yanashauriwa kusimama na kupaki Nakapanya, Namiungo au Majimaji.
Madereva wasilazimishe kuvuka daraja hili kwa sababu wataleta madhara, lakini vyombo vyetu vya usalama vimechukua tahadhari zote, visikilizwe.
Nachingwea apa ni kama tumefungiwa kisiwani hakuna kutoka...kwenda masasi barabara haipitiki kwenda Liwale pia barabara haipitiki.
ni kutumia njia za porini na boda boda
Bora DC Mtatatiro (Zamani Naibu Katibu Mkuu-CUF) ameifunga hiyo barabra kwa sababu kuna madereva vichwa maji kama hayo maji wangelazimisha kupita hapo na kuhatarisha maisha ya raia.