Pre GE2025 Ruvuma: Mwenyekiti CCM, viongozi wa chama acheni kuanzisha migogoro inayochonganisha wananchi na serikali

Pre GE2025 Ruvuma: Mwenyekiti CCM, viongozi wa chama acheni kuanzisha migogoro inayochonganisha wananchi na serikali

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Ruvuma ndugu Oddo Mwisho amewataka viongozi wa chama hicho ngazi ya kata,tawi mpaka shina kuacha tabia za kuanzisha migogoro katika jamii ambayo inawachonganisha viongozi wa serikali pamoja na wananchi.

Hayo ameyasema wakati anaongea na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wa kata ya Kilagano iliyopo halmashauri ya wilaya ya Songea mkoani Ruvuma ambapo kuna mgogoro ambao umedumu miaka 30 na unatokana na wananchi wa kata hiyo wamevamia na kufanya shughuli za kilimo katika hifadhi ya mlima Lihanje.

Pia soma: Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Kutokana na kuwepo kwa mgogoro huo serikali imeamua kutenga eneo la mlima huo na kuwagawia wananchi ili waweze kuendelea na kilimo ambapo kila mwananchi amegawiwa heka tatu.

Baada ya wananchi kugawiwa heka tutu kila mmoja lakini bado mgogoro huo unaendelea baada ya baadhi ya wananchi kukosa eneo la kulima huku wakitoa shutuma za baadhi ya viongozi wa serikali na chama wameshindwa kutenda haki katika zoezi la ugawaji wa ardhi hiyo huku wakieleza baadhi ya viongozi wamewanyang'anya mashamba yao.
 
Back
Top Bottom