RUWASA: Kata ya Nyaishozi na Kitongoji cha Akajiji (Kagera) wanapata maji, pampu ilikatika, imerekebishwa

RUWASA: Kata ya Nyaishozi na Kitongoji cha Akajiji (Kagera) wanapata maji, pampu ilikatika, imerekebishwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
WhatsApp Image 2026-04-17 at 15.07.50.jpeg
Kaimu Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), Wilaya ya Karagwe, Eng. Justo Mtabuzi amesema Kata ya Nyaishozi ina Vijiji vitatu ambavyo ni Nyaishozi, Lukale na Nyakayanja, miradi hii ipo chini ya Chombo cha Utoaji Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii kiitwacho LUNYANYABIRWA.

Vijiji hivyo vina huduma ya maji ya bomba ambayo imesambaa vijiji vyote isipokuwa Kitongoji cha Akajiji kilichopo Kijiji cha Nyakayanja ambacho kinatumia maji kutoka kwenye pampu.

Hoja ya awali ~ Afya za Wananchi Kata Nyaishozi-Karagwe zipo hatarini, wanatumia maji ya madimbwi

Pampu hiyo ya Wananchi hao ndio ilikuwa imeharibika na LUNYANYABIRWA imegharamikia matengenezo ya Pump hiyo kutoka kwenye miradi mingine na imeshatengemaa.

Baada ya kukamilisha matengenezo uliitishwa mkutano tarehe 14 Aprili 2026 ambapo Mkutano ulifanyika na mpango wa kuchangia huduma ukawekwa na huduma imerejea vizuri.

Pamoja na pump hii kitongoji hiki litapata Maji ya uhakika na toshelezi zaidi kupitia mradi wa Rwakajunju wenye thamani ya Shilingi Bilioni 64 wa Miji 28 unaotegemewa kukamilika Desemba 2026.
 
Back
Top Bottom