Nchi zote tatu zinasuasua kwa maandalizi hayo, labda ungesema mojawapo ya nchi inaweza kupokonywa uenyeji na kupewa Rwanda. Kenya nako maandalizi si ya kuridhisha, sawa na Uganda tu. Hizi nchi zimekurupushwa kuandaa uenyeji wakati zenyewe hazikuwa na mpango huo tangu awali. Unaandaaje uenyeji wakati huna miundombinu yake ndio kwanza unajenga harakaharaka na muda hautoshi. Nchi kama Tanzania ingejenga viwanja visivyopungua vitano tayari ndio iombe kuandaa. Mwanza, dar, arusha, mbeya, dom, tanga, moshi, musoma kungejengwa viwanja siku nyingi tayari kusubiri kutumika kwenye mashindano makubwa ya kimataifa