Kikwete aliwezaje!!?
Hayati magufuli ndio muasisi wa siasa zisizotumia akili zaidi ya mkono wa chuma!
Leo risasi na kipotea ndio umekua mbadala wa siasa za kistaarabu na tumeua taifa letu na sasa tumekua vituko huko majuu!!
Hawa Gen z ni rahisi sana kuwa spin rahisi sana!
Tumia mfumo mpya wa ajira za mikataba,tengeneza bunge active lenye upinzani active wa kimfumo!
Wajibisha wanasiasa wezi hata kwa kesi za kimahakama liposha faini funga,filisi n.k
Wanasiasa walipe Kodi lazima watende wanachokihubiri kwenye majukwaa!!
Uone kama gen z wataleta kelele!!
Tunataka siasa tendaji zenye meno sio siasa za wapiga domo tu hata Kodi hawalipi halafu wanapiga makelele tu bila uwajibikaji!!
Kikwete?. Katiba mpya ilifeli kipindi cha nani?. Kwa huo umahiri wake wa kufanya spinning hebu niambie 2005 alishinda kwa kiasi gani na 2010 alishinda kwa kiasi gani?.
Magufuli aliiona hali halisi ya kisiasa hususani kupitia matokeo ya uchaguzi ya 2015 ndio maana 2019 na 2020 akaona aukwapue uchaguzi wenyewe (hii ndio ilikuwa njia pekee ya yeye kubaki madarakani vinginevyo angeng'oka!). Propaganda zake za kupumbaza wananchi kwamba yeye ni Rais wa wanyonge zilifeli kwa kiasi kikubwa. Uhalisia wa maisha ya hao wanyonge wenyewe ulimkataa licha ya ukali wake dhidi ya 'ufisadi'(ingawa ana kesi ya kujibu kuhusu CAG-Profesa Assad).
Magufuli aliposema tu kwamba Katiba mpya sio kipaumbele chake,mtu kama mimi pale pale nilimuona kwamba nae ndio wale wale tu. Sio mzalendo kama tulivyoaminishwa!
Kwa maoni yangu,kipimo cha uzalendo wa kweli wa kiongozi wa kisiasa ni nia yake ya dhati ya kushughulikia mzizi wa matatizo nchini na sio kupumbaza wananchi kwa kujifanya anakata matawi.
Katiba ambayo inampa Rais umungu mtu wa kufanya chochote anachotaka na akishafanya hashtakiwi akitoka madarakani ya kazi gani hiyo?
Mkuu,CCM wamshukuru sana Mbowe. Huyu amewasaidia sana kuchelewesha mabadiliko halisi nchini kupitia spinning ya maridhiano. Cheki mtiti wa Lissu na Heche!
Mkuu,hebu toa mbinu hata moja tu ya kuspin suala la Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi. Yaani hiyo mbinu iwapumbaze watanzania wengi waone hakuna haja ya kuwa na Katiba mpya wala Tume huru ya uchaguzi.
Wakati huo huo usisahau kwamba kwa muda mrefu, CCM kiliwekeza sana kwenye UJINGA na UFUKARA kwenye maisha ya watu vikiwa kama mtaji wake muhimu wa kuendelea kubaki madarakani. Tafsiri yake ni kwamba kadiri UJINGA au UFUKARA unavyopungua ndivyo CCM inakuwa hatarini zaidi kutoka madarakani.
Kwa sababu wananchi wanazidi kufunguka akili,imefikia hatua kila ambacho CCM watafanya kitakuwa kinaharakisha ANGUKO lao.Fanya maendeleo,unang'oka, usifanye maendeleo unang'oka vile vile!. Imarisha demokrasia unang'oka,zorotesha demokrasia unang'oka!
Karibu kwa Mawazo kinzani. Nipo tayari kukosolewa!