Rwanda katuzidi wapi kwenye kutangaza utalii?

Rwanda katuzidi wapi kwenye kutangaza utalii?

The Genius

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
822
Reaction score
2,095
Huyu ni Lionel Messi wakati akiwa anawasili kwenye viunga vya Paris Saint Germain (PSG).

Hii video imepostiwa kwenye official page ya PSG yenye mamillion ya followers, video hii hii imetazamwa na wapenzi wa kandanda wengi sana duniani na media kubwa duniani za football kama skysport,bt, supersport n.k wame repost hii video.

Kilichonivutia ni hilo neno hapo nyuma kwenye jezi ya MESSI.

Hakuna jina lake wala maandishi mengine zaidi ya VISIT RWANDA.

Nimewaza sana hivi RWANDA kuna kivutio gani kikubwa cha kushawishi hadi waende kuitangaza kwenye jezi ya club kubwa namna hii kwenye mgongo wa mtu maarufu hivi ulimwenguni.Wanavitu gani ambavyo Tanzania hatuna hadi waende kufanya promo kubwa kama hii?

Hapo nikakumbuka ile kauli ya Yericko Nyerere kuwa wenzetu wamewekeza kwenye ujajusi wa KIUCHUMI sisi tumewekeza kwenye ujajusi wa kumkamata mbowe na wafuasi wa Chadema.

Peter Msigwa aliwahi kusema kuliko kuwachukua kundi kuuubwaa la kina pierre liquid,babalevo,manara,steve nyerere nk watu ambao ni maarufu ndani ya Tanzania tu eti unaenda kufanya nao promo ya kuutangaza mlima Kilimanjaro kwa kupanda ule mlima,ni bora kuleta watu maarufu wachache duniani waje kuupanda bure au kwa bei nafuu zaidi, wetu wenye ushawishi kubwa kwenye soka,music au tasnia nyingine pendwa sana duniani.

Watu kama kina Messi, CR7, Tiger Woods, Maria Sharapova, Drake n.k watu ambao wakija Tanzania dunia itaangalia wamekuja kufanya nini na ulimwenguni utakuwa na attention kwa kiasi fulani.

Wanyarwanda wametuzidi wapi aisee? Ile nchi na mkoa wa kagea ni kama sawa tu, ila wapo intelligent sana kuliko sisi.Wapi tunafeli au intelligence yetu ndio ina shauri kuweka Tozo ili kupata hela na sio kutangaza utalii kama Rwanda?

#Nawaza Tu.

Didas Tumaini
shaffihdauda__20210811_152542_0.jpg
 
Wenzetu Rwanda wanabambikia wapinzani wa serikali kesi huku wakiumiza vichwa jinsi ya kujenga nchi yao. Watendaji wa serikali ya kwetu,Bongo zao zimejaa makamasi
Viongozi wetu wa Kibongo wanawaza tu namna ya kuongeza tozo kwenye mitandao ya simu
 
Sisi kigwangala alishafanya Sana hayo mambo mpaka akamtafuna poshy queen alafu akawalipa dabliusibii wakawa wanatalii huku wanakula pesa maana CAG alisema Yale malipo hayakua na viambatanisho 🤣🤣 Tanzania ukiwa CCM ukapewa kauwaziri unakula maisha🤣🤣
 
Visit Rwanda[emoji123][emoji123][emoji123][emoji91][emoji91][emoji119][emoji119]
 
Tz inadili zaidi na wapinzani. Na kuwabambikizia kesi!!! Umeshawahi kumuona au kuwasikia mawaziri wa Rwanda hata wakiongea kwenye luninga!?? Veeeery decent!!! Tooooofauti na hawa wa huku!! Amboa wengi ni PhD feki
 
Tapeli la kike liliahidi ajira 40,000. Sasa hivi limejikausha kweri kweri
 
Wanauhakika wa kuhudumiwa mpaka wanakufa wao na familia zao, mawaziri, wabunge na wakuu wa taasisi wote hao ni Club moja kupeana madili huku uhakika wa mshahara mnono + posho + V8. Hakuna mwenye muda kuhusu Taifa, zaidi wanahubiri tuwe na Amani ili tusiwahoji.
 
Wanauhakika wa kuhudumiwa mpaka wanakufa wao na familia zao, mawaziri, wabunge na wakuu wa taasisi wote hao ni Club moja kupeana madili huku uhakika wa mshahara mnono + posho + V8. Hakuna mwenye muda kuhusu Taifa, zaidi wanahubiri tuwe na Amani ili tusiwahoji.
Apo kwenye amani ndo wanataka kula bila kubuguziwa.
 
Alipotuzidi ni malengo tu.

Wakati wenzetu wanalenga kupata soko la ulaya kwa kutangaza chapa yao kupitia soka kwenye vilabu vikubwa

Sisi Tz tukawa busy kusaka soko la ulaya kwa kutangaza utalii kwa kuwatumia mastaa wa Bongo movie mfano...sitivu na ile chapa yetu ya unforgetable Tanzania

Tuna waza kupata watalii mil 2+ bila kutangaza utalii wetu ktk njia stahiki
 
Back
Top Bottom