Rwanda, Kenya na Uganda zajipanga kuwa na umeme wa nyuklia, Tanzania tumejipangaje?

davedas

Senior Member
Joined
Feb 18, 2015
Posts
163
Reaction score
123
Rwanda wanampango mpaka 2026 wawe wanafua umeme kupitia nyuklia, Uganda pia wanampango mpaka mwaka 2040 wawe wana uwezo wa kuzalisha umeme kupitia nyuklia, Kenya wao ni mpaka 2035. Sisi tumejipanga vipi?

Ukweli ni kwamba umeme wa nyuklia huwa ni bei rahisi sana kuuendesha na pia unatoa umeme mwingi ukilinganisha na vyanzo vingine vya umeme.. hii upelekea unafuu wa bei kwa mtumiaji wa mwisho ikiwemo viwanda.

Sote tunajua jinsi ilivyo ngumu kwa mwekezaji kuwekeza Tanzania kutokana na sheria zilipo bado tena uko kwenye urahisi wa kuwekeza wanajiongezea advantage nyingine ya kuwa na nishati nafuu ambayo inapelekea uendeshaji wa viwanda kuwa nafuu zaidi.

Serikali haioni kuwa tutakosa wawekezaji hasa hasa viwanda, Serikali imejipange bhasi kwa Tanzania kuwa na nishati nafuu kuliko majirani hivyo kupelekea ukuwaji na mapinduzi ya viwanda au ndo ile tumeshachagua kuwa soko la bidhaa la majirani?

Naona tupo kwenye mchakato wa kutengeneza Dira ya tanzania..Najua kuna wanao husika humu, tunaomba wafikilie pia kuhusu uzalishaji wa umeme wa nyuklia au kama tunaona hatuwezi bhasi waje na alternative ya nishati ambayo haitaathiliwa na mabadiliko ya hali ya hewa na yenye kutoa nishati ya bei rahisi.

Uzuri kila kitu tunacho, madini ya uranium tunayo, ardhi kubwa ya kutenga kwa ajili ya vinu vya nyuklia ambayo hata majanga yakitokea hayawezi kuathiri watu tunayo.

Hivyo ni sisi tu kuamua Tanzania yetu tunataka iwaje miaka kumi ijayo.​
 
Hatuna sababu ya kuwa na umeme wa nuclear wakati tuna vyanzo vingine vingi,hao hawana vyanzo mbadala.

Kenya wanategenea geothermal,jua na maji kidogo

Rwanda NJ maji tuu

Tanzania tuna vyanzo vya Maji Lukuki,Makaa ya Mawe ya kumwaga,gesi kama yote, geothermal hata hatujagusa,upepo na jua kazi inaendelea Shinyanga Bado Makambako nk nk
 
Sahihi nyukilia ya kuzalisha umeme wala hatuhitaji watanzania hata tupewe bure
 
Huo tulio nao sasa hivi ni zaidi ya mahitaji yetu kwa miaka 10 ijayo.

Hatuigi fulani anafanya hivi na sisi tufanye hivyo.
 
Uko Sahihi hatuhitaji umeme wa Nyuklia tunao wa kutosha usio wa Nyuklia kuzidi matumizi yetu labda wao watuombe wao tuwauzie umeme extra tusiouhitaji
 
Huo tulio nao sasa hivi ni zaidi ya mahitaji yetu kwa miaka 10 ijayo.

Hatuigi fulani anafanya hivi na sisi tufanye hivyo.
Lakini huo tulio nao mwingi unatoka kwenye Nyerere hydro power mabadiliko ya hali ya hewa kidogo tu tunarudi kwenye mgao
 
Hatuna sababu ya kuwa na umeme wa nuclear wakati tuna vyanzo vingine vingi,hao hawana vyanzo mbadala.

Kenya wanategenea geothermal,jua na maji kidogo

Rwanda NJ maji tuu

Tanzania tuna vyanzo vya Maji Lukuki,Makaa ya Mawe ya kumwaga,gesi kama yote, geothermal hata hatujagusa,upepo na jua kazi inaendelea Shinyanga Bado Makambako nk nk
Katika vyanzo vingi na nyuklia iwepo muhimu ni kuangalia cost na bei kwa mtumiaji wa mwisho.
Pia ni advantage kuwa na vyanzo vingi hata kukiwa na mabadiliko yoyote mfano ukame vingine vinatumika
 
Huo tulio nao sasa hivi ni zaidi ya mahitaji yetu kwa miaka 10 ijayo.

Hatuigi fulani anafanya hivi na sisi tufanye hivyo.
Ndiyo maana tunawauwa uwa na kuwabambikia case kwanza tunaohisi wanatuchelewesha ili ikifika hiyo miaka kumi tuzidi kuwapiga gap hao wanaojifanya kuwa na umeme wa nyuklia.

Unaongea kama kasuku huo umeme wa kutosha uko wapi nchi hii!
 
Huo tulio nao sasa hivi ni zaidi ya mahitaji yetu kwa miaka 10 ijayo.

Hatuigi fulani anafanya hivi na sisi tufanye hivyo.
Halafu hatuigi..!
Ukisoma vinzuri utaona kuwa maoni ni tunajipangaje kuwa na vyanzo vyenye kupunguza bei ya umeme kwa watumiaji
 
Katika vyanzo vingi na nyuklia iwepo muhimu ni kuangalia cost na bei kwa mtumiaji wa mwisho.
Pia ni advantage kuwa na vyanzo vingi hata kukiwa na mabadiliko yoyote mfano ukame vingine vinatumika
Nyumlia ni too expensive
 
Uranium yetu ina kazi gani?? Inamaana migodi yetu yote ya uranium nitaendelea kuwanufaisha mabepari tu??
 
Attachments

  • Screenshot_20240919_224206_Chrome.jpg
    Screenshot_20240919_224206_Chrome.jpg
    217.5 KB · Views: 5
Rwanda wanampango mpaka 2026 wawe wanafua umeme kupitia nyuklia, Uganda pia wanampango mpaka mwaka 2040 wawe wana uwezo wa kuzalisha umeme kupitia nyuklia, Kenya wao ni mpaka 2035. Sisi tumejipanga vipi?

Ukweli ni kwamba umeme wa nyuklia huwa ni bei rahisi sana kuuendesha na pia unatoa umeme mwingi ukilinganisha na vyanzo vingine vya umeme.. hii upelekea unafuu wa bei kwa mtumiaji wa mwisho ikiwemo viwanda.

Sote tunajua jinsi ilivyo ngumu kwa mwekezaji kuwekeza Tanzania kutokana na sheria zilipo bado tena uko kwenye urahisi wa kuwekeza wanajiongezea advantage nyingine ya kuwa na nishati nafuu ambayo inapelekea uendeshaji wa viwanda kuwa nafuu zaidi.

Serikali haioni kuwa tutakosa wawekezaji hasa hasa viwanda, Serikali imejipange bhasi kwa Tanzania kuwa na nishati nafuu kuliko majirani hivyo kupelekea ukuwaji na mapinduzi ya viwanda au ndo ile tumeshachagua kuwa soko la bidhaa la majirani?

Naona tupo kwenye mchakato wa kutengeneza Dira ya tanzania..Najua kuna wanao husika humu, tunaomba wafikilie pia kuhusu uzalishaji wa umeme wa nyuklia au kama tunaona hatuwezi bhasi waje na alternative ya nishati ambayo haitaathiliwa na mabadiliko ya hali ya hewa na yenye kutoa nishati ya bei rahisi.

Uzuri kila kitu tunacho, madini ya uranium tunayo, ardhi kubwa ya kutenga kwa ajili ya vinu vya nyuklia ambayo hata majanga yakitokea hayawezi kuathiri watu tunayo.

Hivyo ni sisi tu kuamua Tanzania yetu tunataka iwaje miaka kumi ijayo.​
Vitu vingine msiwe mnashadadia tu mmesikia habari mnapayuka.
Hivi bro unajua thamani na gharama ya kusimamisha kinu cha nuclear ki generate energy!??
Kwanza hizo nchi hayo madini ya uranium wanayo!?
Hiyo Kenya kukarabati uwanja wa ndege tu imewashinda waje kusimamisha kinu cha nuclear energy??
Embu acheni kushadadia habari mfu.
 
Umeme ulitakiwa kuwa mwingi mnoo kwasasa baada ya kukamilika kwa Stigglers na hilo lingesaidia kuinua uchumi mtu akijenga kiwanda asijiulize habari ya majenerator.

Umeme bado unakatika sana maeneo mengi tu
 
Vitu vingine msiwe mnashadadia tu mmesikia habari mnapayuka.
Hivi bro unajua thamani na gharama ya kusimamisha kinu cha nuclear ki generate energy!??
Kwanza hizo nchi hayo madini ya uranium wanayo!?
Hiyo Kenya kukarabati uwanja wa ndege tu imewashinda waje kusimamisha kinu cha nuclear energy??
Embu acheni kushadadia habari mfu.
75 M usd cha Rwanda
Sasa hyo itatushindwa?
 
Back
Top Bottom