Rwanda kuanza kutumia nguruwe kama mlo mashuleni

Rwanda kuanza kutumia nguruwe kama mlo mashuleni

Hata waislam wenyekuifuata msaafu hawali ngamia kamweee
Maana zote sawa

Kwenye sheria za Wayahudi/Jews/Israel hawatumii vyote hivyo, Nguruwe na Ngamia na wao ndo wana sheria kali mno zingine hata namna ya kuchanganya vyakula ambavyo wanaruhusiwa kula kuna mpangilio wake

Mfano maziwa hayatakiwi kuchangamana na nyama inayoruhusiwa kuliwa wakati wa kula vinatakiwa kupishana masaa unaweza ona kwenye ‘ Koshar Laws’

Kumbuka Judaism ndo imewapa wengine miongozo mingi tu
 
Mijamaa itakuwa na akili sana.

Huwa watu wanaonyesha jamii ya Israel/Jews ni watu wenye akili mno lkn kwao Nguruwe ni katazo kubwa ni ‘forbidden’ kabisa sasa sijajua nguruwe na akili vina uhusiano upi?
 
Ukiona mtawala anaanza kuwalazimisha watu kwenda kinyume na dini zao elewa kuwa siku zake zinahesabika.

kwani wamelazimisha madam? Mbona kwenye shule zetu hapa tanzania siku ya nyama shuleni kuna vegetarian huwa hawatumii mboga hiyo na hakuna wakuwagusa. Shida iko wapi?
 
La haraka haraka kichwani ni "swine flu" Elewa kuwa siku hizi dunia kiganjani, unaweza kumtumia chatgpt:

Swine can carry a variety of diseases that can be transmitted to humans. Some of the diseases associated with swine include ringworm, erysipelas, leptospirosis, streptococcosis, campylobacterosis, salmonellosis, cryptosporidiosis, giardiasis, balantidiasis, infection with pathogenic E. coli, and brucellosis¹.
magonjwa mengi yamedhibitiwa kwa sasa hasa hayo Zoonotic.mimi si mlaji wa nguruwe ila nimemsoma na kwa tafiti zilizofanyika nyama yake ni nzuri na ina virutubisho vya kutosha bila kusahau anafaida chungu mzima kuanzia bandandani hadi mezani.ulaji wa nguruwe na tende waweza kuwa mwarobaini wa utapia mlo tukitazama kwa umakini
 
Binafsi kitimoto ilishanishinda, all the best kwa walaji.

Chakula ni utamaduni na siyo dini! Mimi naamini hivyo. Maeneno mengi duniani nguruwe ni rahisi kupatikana kuliko nyama nyinginezo. Pia uvunaji wa nyama ya nguruwe ni muda mfupi ukilinganisha na mifugo wengine.

Kaeni mkijua kuwa Kagame ni msabato ( ambao ndiyo wapinga kitimoto) lakini kaona mbali kuhusu lishe.
 
View attachment 2639065

Mipango inaendelea kuwezesha shule kujumuisha nyama ya nguruwe katika ratiba ya chakula nchini Rwanda kama njia ya kutokomeza utapiamlo, Olivier Kamana, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Rasilimali Wanyama amenukuliwa na gazeti la New Time nchini humo akisema.

"Tunaziomba shule kuanzisha miradi ya ufugaji wa nguruwe ili kuweza kumudu nyama ya nguruwe," alisema.

Mnamo mwaka wa 2019, mpango wa lishe shuleni ulitekelezwa katika shule za sekondari (zinazosaidiwa na serikali na za serikali) huku wanafunzi 680,000 wakipokea ruzuku ya Serikali ya chakula cha shule.

Takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuwa shule za msingi na sekondari ziliongezeka kutoka 2,877 mwaka 2017 hadi 2,963.

Mnamo 2021, Rwanda ilizalisha tani 185,989 za nyama. Idadi ya nguruwe imeongezeka kutoka 989,000 mnamo 2012 hadi takriban milioni 1.5 mnamo 2021.

Nchi hiyo iilizalisha wastani wa tani 23,000 za nyama ya nguruwe kwa katika mwaka 2019 na inalenga kuongeza uzalishaji wa nyama hiyo hadi kufikia tani 68,000 ifikapo 2024.

“Tunashughulikia mpango wa kutumia vyanzo mbadala vya protini kulisha mifugo badala ya mahindi. Hii itasaidia kuongeza idadi ya wafugaji wa nguruwe na uzalishaji wa nguruwe,” Kamana alisema.

---

NB. Afya haina dini
Safi sana bonge la plan , Tanzania tunafeli sababu ya Iman za watu wengine kwa Kagame anakuambia ukileta mambo ya Iman za kidini kwenye Mipango ya serikali , haraka katafute nchi yako
 
Safi sana bonge la plan , Tanzania tunafeli sababu ya Iman za watu wengine kwa Kagame anakuambia ukileta mambo ya Iman za kidini kwenye Mipango ya serikali , haraka katafute nchi yako
Ye ni mpitaji Hana hata miaka 15 ya kuwepo Duniani
 
Yaani huyu ni wale wanazi wa kidini. Yaani yeye anatumia nguvu zake kutetea dini badala ya kukubali kuwa wanadamu tunatofautiana.

Ajifunze kuishi na watu wa dini tofauti na yake pia.
shule ndogo ndio shida mimi nimeshuhudia dakitari wa mifugo wasilamu wengi tuh wana kagua nyama za nguruwe wanawakata meno, kuhasi na kuwatibu bila shida yoyote wala hawamchukii nguruwe tena wanafuga na nguruwe kabisa lakini sijda ziko usoni
 
Ye ni mpitaji Hana hata miaka 15 ya kuwepo Duniani
Hakuna haijuae kesho si yeye wala wewe , ila yeye ni mpitaji wa mipango sio kibwegebwege , juzi kafungia makanisa 78 yasio na usajili na wachungaji wasio na degree ya theolojia wote kawafuta na makanisa yao kayafungilia mbali.....
 
Hakuna haijuae kesho si yeye wala wewe , ila yeye ni mpitaji wa mipango sio kibwegebwege , juzi kafungia makanisa 78 yasio na usajili na wachungaji wasio na degree ya theolojia wote kawafuta na makanisa yao kayafungilia mbali.....
Akiondoka akija mwingine atayafungulia ili apate kura za wapigakura.Afrika mtawala ndie sheria Kila ajae huja na yake
 
shule ndogo ndio shida mimi nimeshuhudia dakitari wa mifugo wasilamu wengi tuh wana kagua nyama za nguruwe wanawakata meno, kuhasi na kuwatibu bila shida yoyote wala hawamchukii nguruwe tena wanafuga na nguruwe kabisa lakini sijda ziko usoni
Uislam umekataza kumla nguruwe ba wapo wenye kukufuru wanakula.
 
Back
Top Bottom