Rwanda kuanza kutumia nguruwe kama mlo mashuleni

View attachment 2639065

Mipango inaendelea kuwezesha shule kujumuisha nyama ya nguruwe katika ratiba ya chakula nchini Rwanda kama njia ya kutokomeza utapiamlo, Olivier Kamana, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Rasilimali Wanyama amenukuliwa na gazeti la New Time nchini humo akisema.

"Tunaziomba shule kuanzisha miradi ya ufugaji wa nguruwe ili kuweza kumudu nyama ya nguruwe," alisema.

Mnamo mwaka wa 2019, mpango wa lishe shuleni ulitekelezwa katika shule za sekondari (zinazosaidiwa na serikali na za serikali) huku wanafunzi 680,000 wakipokea ruzuku ya Serikali ya chakula cha shule.

Takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuwa shule za msingi na sekondari ziliongezeka kutoka 2,877 mwaka 2017 hadi 2,963.

Mnamo 2021, Rwanda ilizalisha tani 185,989 za nyama. Idadi ya nguruwe imeongezeka kutoka 989,000 mnamo 2012 hadi takriban milioni 1.5 mnamo 2021.

Nchi hiyo iilizalisha wastani wa tani 23,000 za nyama ya nguruwe kwa katika mwaka 2019 na inalenga kuongeza uzalishaji wa nyama hiyo hadi kufikia tani 68,000 ifikapo 2024.

“Tunashughulikia mpango wa kutumia vyanzo mbadala vya protini kulisha mifugo badala ya mahindi. Hii itasaidia kuongeza idadi ya wafugaji wa nguruwe na uzalishaji wa nguruwe,” Kamana alisema.

---

NB. Afya haina dini
Saafi sana aisee yaani umenifanya hadi mesikia njaa ghafla

OP.jpg
 
Hata wakristo wenye kuifata biblia hawali nguruwe.

Ukiiona mijitu inakula nguruwre ujuwe hiyo ni mikafiri tu.
Usitupangie Biblia ilishatutaarifu kwamba

Matendo ua Mitume 10:
11 Akaona mbingu zimefunguka na kitu kama nguo kubwa kikishushwa duniani kwa ncha zake nne. 12Ndani yake walikuwepo aina zote za wanyama wenye miguu minne, nao watambaao nchini, na ndege wa angani. 13Ndipo sauti ikamwambia “Petro, ondoka, uchinje na ule.”
14 Petro akajibu, “La hasha Bwana! Sijawahi kamwe kula kitu chochote kilicho najisi.”
15 Ile sauti ikasema naye mara ya pili, “Usikiite najisi kitu chochote Mungu alichokitakasa.”
 
Kwa ule utamu wa kitimoto itoshe tu kusema dikteta Kagame anaupiga mwingi. Lishe bora itafanya vijana wawe na akili mingi. Hata hapa Tanzania waanzishe hiyo kitu.
Hata hapo Tanzania wewe uko wapi? Ulaya Nguruwe hana thamani, ni nyama yenye bei ya chini kuliko zote upo Malawi nini??? Umaskini tu ndio unamfanya mbongo afiklie kuwa nguluwe ni mtamu.
 
Hata wakristo wenye kuifata biblia hawali nguruwe.

Ukiiona mijitu inakula nguruwre ujuwe hiyo ni mikafiri tu.
Acha habari zako Dada wewe,mimi muislamu pure,swala tano kabisa ila huniambii kitu juu ya kitimoto
 
Usitupangie Biblia ilishatutaarifu kwamba

Matendo ua Mitume 10:
11 Akaona mbingu zimefunguka na kitu kama nguo kubwa kikishushwa duniani kwa ncha zake nne. 12Ndani yake walikuwepo aina zote za wanyama wenye miguu minne, nao watambaao nchini, na ndege wa angani. 13Ndipo sauti ikamwambia “Petro, ondoka, uchinje na ule.”
14 Petro akajibu, “La hasha Bwana! Sijawahi kamwe kula kitu chochote kilicho najisi.”
15 Ile sauti ikasema naye mara ya pili, “Usikiite najisi kitu chochote Mungu alichokitakasa.”
Hapo ushajijibu mwenyewe "" ulichokitakasa",

Nguruwe wapi katakaswa? Au huku ndiko kutakaswa kwenyewe:

Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu.
8 Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao; hao ni najisi kwenu.
 
Usitupangie Biblia ilishatutaarifu kwamba

Matendo ua Mitume 10:
11 Akaona mbingu zimefunguka na kitu kama nguo kubwa kikishushwa duniani kwa ncha zake nne. 12Ndani yake walikuwepo aina zote za wanyama wenye miguu minne, nao watambaao nchini, na ndege wa angani. 13Ndipo sauti ikamwambia “Petro, ondoka, uchinje na ule.”
14 Petro akajibu, “La hasha Bwana! Sijawahi kamwe kula kitu chochote kilicho najisi.”
15 Ile sauti ikasema naye mara ya pili, “Usikiite najisi kitu chochote Mungu alichokitakasa.”
Hakika, wewe umejawa na Roho Mtakatifu, kwa mamlaka yangu, nakuagiza ukapate safari lager kumi hapo kwenye duka la mangi
 
View attachment 2639065

Mipango inaendelea kuwezesha shule kujumuisha nyama ya nguruwe katika ratiba ya chakula nchini Rwanda kama njia ya kutokomeza utapiamlo, Olivier Kamana, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Rasilimali Wanyama amenukuliwa na gazeti la New Time nchini humo akisema.

"Tunaziomba shule kuanzisha miradi ya ufugaji wa nguruwe ili kuweza kumudu nyama ya nguruwe," alisema.

Mnamo mwaka wa 2019, mpango wa lishe shuleni ulitekelezwa katika shule za sekondari (zinazosaidiwa na serikali na za serikali) huku wanafunzi 680,000 wakipokea ruzuku ya Serikali ya chakula cha shule.

Takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuwa shule za msingi na sekondari ziliongezeka kutoka 2,877 mwaka 2017 hadi 2,963.

Mnamo 2021, Rwanda ilizalisha tani 185,989 za nyama. Idadi ya nguruwe imeongezeka kutoka 989,000 mnamo 2012 hadi takriban milioni 1.5 mnamo 2021.

Nchi hiyo iilizalisha wastani wa tani 23,000 za nyama ya nguruwe kwa katika mwaka 2019 na inalenga kuongeza uzalishaji wa nyama hiyo hadi kufikia tani 68,000 ifikapo 2024.

“Tunashughulikia mpango wa kutumia vyanzo mbadala vya protini kulisha mifugo badala ya mahindi. Hii itasaidia kuongeza idadi ya wafugaji wa nguruwe na uzalishaji wa nguruwe,” Kamana alisema.

---

NB. Afya haina dini
Kwa sie vegetarians itakuwaje?
 
Wawe wanaweka kaugali kadogo nyama nyingi ili waifaidi vizuri.
Hatari sana ......
 
Uislam umekataza kumla nguruwe ba wapo wenye kukufuru wanakula.
kwa sababu zipi hasa kama ni magonjwa tayari tumeyadhibiti ,shida nini watoto wasipate lishe bora inayozagaa bure. unafikiri kipi kitakukuta ahera iwapo ukapoteza maisha kwa utapia mlo ilihali nyama ya nguruwe ipo ya kutosha
 
Hata hapo Tanzania wewe uko wapi? Ulaya Nguruwe hana thamani, ni nyama yenye bei ya chini kuliko zote upo Malawi nini??? Umaskini tu ndio unamfanya mbongo afiklie kuwa nguluwe ni mtamu.
Unaugua wendawazimu? Kuna sehemu nimeandika HAPO? PUMBAVU SANA
 
Back
Top Bottom