Rwanda kuanza kutumia nguruwe kama mlo mashuleni

Rwanda kuanza kutumia nguruwe kama mlo mashuleni

Hata hapo Tanzania wewe uko wapi? Ulaya Nguruwe hana thamani, ni nyama yenye bei ya chini kuliko zote upo Malawi nini??? Umaskini tu ndio unamfanya mbongo afiklie kuwa nguluwe ni mtamu.
Mkuu, nadhani swala la nyama ya nguruwe kuwa ya bei ya chini(kutokuwa na thamani) linazingatia zaidi gharama za uzalishaji wa nyama ya nguruwe na hizo nyingine.
 
Hata wakristo wenye kuifata biblia hawali nguruwe.

Ukiiona mijitu inakula nguruwre ujuwe hiyo ni mikafiri tu.
. Sikushangai, wewe hata nyama ya mtu utakula tu.

mimi ni moja ya wakristo wasiokula nguruwe toka nazaliwa, hilo la Rwanda nadhani watajitahidi wale wasiokula nguruwe hasa wanaokatazwa kiimani watapata mlo wao ulioandaliwa kwa kufuata misingi ya imani, na sidhani kama itakua sera ya kitaifa maana waislamu Rwanda ni wengi na naamini hawatoafiki
 
Afya Haina dini.. au nasema uongo ndugu zangu

Kwenye viwango vya ubora wa chakula, unafahamu kama food nutrients za kwenye dagaa ni bora zaidi kuliko nyama ya nguruwe, kwahivo hua naangalia hata bei ya nyama kwenye maduka mbalimbali Halaal meat kama kuku, ng’ombe, ngamia, mbuzi, unganisha samaki na dagaa bei yake iko juu kuliko nyama ya nguruwe ushawahi kujiuliza kwa nini? Jibu ni kua hata protini ipatikanayo kwenye nguruwe ni hafifu sana
 
Hata hapo Tanzania wewe uko wapi? Ulaya Nguruwe hana thamani, ni nyama yenye bei ya chini kuliko zote upo Malawi nini??? Umaskini tu ndio unamfanya mbongo afiklie kuwa nguluwe ni mtamu.
Labda unaongelea ulaya ya mpala kyala uko,ukitoa samaki nguruwe ndio nyama ya pili kwa bei.
Kuku broiler ndio nyama ya mwisho isiyo na bei
 
View attachment 2639065

Mipango inaendelea kuwezesha shule kujumuisha nyama ya nguruwe katika ratiba ya chakula nchini Rwanda kama njia ya kutokomeza utapiamlo, Olivier Kamana, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Rasilimali Wanyama amenukuliwa na gazeti la New Time nchini humo akisema.

"Tunaziomba shule kuanzisha miradi ya ufugaji wa nguruwe ili kuweza kumudu nyama ya nguruwe," alisema.

Mnamo mwaka wa 2019, mpango wa lishe shuleni ulitekelezwa katika shule za sekondari (zinazosaidiwa na serikali na za serikali) huku wanafunzi 680,000 wakipokea ruzuku ya Serikali ya chakula cha shule.

Takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuwa shule za msingi na sekondari ziliongezeka kutoka 2,877 mwaka 2017 hadi 2,963.

Mnamo 2021, Rwanda ilizalisha tani 185,989 za nyama. Idadi ya nguruwe imeongezeka kutoka 989,000 mnamo 2012 hadi takriban milioni 1.5 mnamo 2021.

Nchi hiyo iilizalisha wastani wa tani 23,000 za nyama ya nguruwe kwa katika mwaka 2019 na inalenga kuongeza uzalishaji wa nyama hiyo hadi kufikia tani 68,000 ifikapo 2024.

“Tunashughulikia mpango wa kutumia vyanzo mbadala vya protini kulisha mifugo badala ya mahindi. Hii itasaidia kuongeza idadi ya wafugaji wa nguruwe na uzalishaji wa nguruwe,” Kamana alisema.

---

NB. Afya haina dini
Safi sana, hiki ni chakula sahihi kwa afya ya wanadamu.
 
Hata wakristo wenye kuifata biblia hawali nguruwe.

Ukiiona mijitu inakula nguruwre ujuwe hiyo ni mikafiri tu.
Mungu aliumba nguruwe ila hakuumba dini.Ukijua kutofautisha vilivyoumbwa na Mungu na vilivyoumbwa na binadamu kamwe huwezi kupata shida.
 
Mungu aliumba nguruwe ila hakuumba dini.Ukijua kutofautisha vilivyoumbwa na Mungu na vilivyoumbwa na binadamu kamwe huwezi kupata shida.
Mungu kaumba vya kuliwa na visivyoliwa, au wewe vyenye uhai vyote unakula?

Unajuwa maana ya neno dini?
 
Labda unaongelea ulaya ya mpala kyala uko,ukitoa samaki nguruwe ndio nyama ya pili kwa bei.
Kuku broiler ndio nyama ya mwisho isiyo na bei
Na unajiita msweden... huoni aibu?? ulienda na group la kwaya na ukarudi nini?? Tuwekee hizo bei Kondoo au Ng'ombe alipozidiwa bei na Nguruwe??
 
Back
Top Bottom