Rwanda military trained Burundi rebels to oust Nkurunziza – UN Report reveals

Sisi waafrica ni ma taahira tunapenda kucheza mziki wa wazungu siku zote Lengo la mataifa ya magharibi ni kumng'oa Kagame Wazungu siku zote hawapendi kuona mwafrika mwelevu. hiyo ni chokochoko ili waingie Rwanda wala sio Burundi kwani ya burundi wanayafurahia sana trust me Mungu ataendelea kumlinda huyu Kagame ili waafrika tujifunze namna ya uongozi bora na jinsi ya kuwaletea wananchi maendeleo
 
Hao militants wamekiri kufundishwa na Rwanda Mzungu anaingiaje hapo?
 
Kila ukanda fulani kunakua na nchi yenye nguvu kuliko zingine na inakua inatoa miongozo fulafula, na hata wakati mwingine inaweza kuamua au kupanga nani anafaa kuwa rais ktk nchi jiran na hasa wanapoona mtu huyo Ana faida kwa nchi hiyo, mfano wa majirani zetu wa MALAWI, Yule mama wakati anataka urais alianza usumbufu kuhusu ziwa nyasa,mtaalam JK alimtembelea akamchekea kulee! Kilichomtokea kwenye urais nafikili mmeona, na aliewekwa kwa wafuatiriaji mnamjua venal.SASA KWA HUYU KAGAME ANAONEKANA KUTAMANI KUMILIKI UKANDU HUO NA SIJUI KAMA ATAWEZA. na ndiomaana kilasiku anajalibu kutukana viongozi wetu hapa, na nafikili anajifutia balaa na kunasiku yatamkuta yy mwenyewe.
 
Hoja yako inanikumbusha kifo cha Mch. Mtikila!
 
Suala la Rwanda kupanga mikakati ya kupindua serekali ya Nkurunzinza si mpaka tuambiwe na BBC siku nyingi ilishajulikana Kagame ndio kinara wa fujo eneo la maziwa makuu.

Alisambaratisha serekali ya Congo DRC kama si msaada wa nchi za SADC Kabila angeshaondolewa madarakani.Alijaribu kuitikisa serekali ya Tanzania kwa kupeleleza TPDF hadi mwanajeshi wetu mwenye asili ya kitusi (mwangaza) Col akakimbilia Rwanda mpaka leo kafichwa na serekali ya Kigali.

Rwanda ni muasisi wa CoW ukiwa ni mkakati wa kuyumbisha maslahi ya Tanzania EAC.Linapozungumzwa swala la Rwanda kwangu mimi naoana ni mkakati wa muda mrefu wa jamii ya kitutsi kutaka kutawala eneo lote la maziwa makuu na kujiona wao watutsi ni class ya juu kuliko jamii nyingine (HIMA EMPIRE).
 
Alitaka kucheza na moto huku ameshika petrol, alitaka kujipima nguvu na Tanzania akasahau mtusi mwenzake Buyoya alitaka kufanya hivyo kwa Tz moto ulimuwakia mpaka akaomba radhi tena kwa kupiga magoti, Nafikri Rwanda tunaweza kuisambaratisha within five minutes maana tuna base pale Congo, kwa hiyo tungepiga mpaka akajikojolea, Lakini kagame anasahau kuwa anachokutengeneza pale Rwanda ni bomu ambalo soon litamripukia anaugomvi na watusi wenzake, ana ugomvi na wahutu so ajipange.
 
Usisahau alitaka kutuwekea Rais mamluki hivi majuzi tu...kumbuka kauli ya Christopher Mtikila.
 
Hili sidhani kama lina uongo kulingana na aina ya mtu (nchi) inayotuhumiwa.
 
Kunaweza kuwa na mantiki flani hivi ya Nkurunziza kung'ang'ania madaraka!

Na Kagame pia kung'ang'ania madaraka!, Mpaka sasa ana miaka 20 akiwa rais na anabadili katiba ili aongoze tena kwa miaka 17 ijayo.
 
Nimefurahi tu Mushikwabo anaposema "hatutawarudisha Burundi mpaka hapo tutakapohakikishiwa usalama wa maisha yao" ahahahahaaaaa. Yaani Rwanda in-guts za kusema maneno haya kweli!!! Mbona wao wanawasaka wapinzani kila kona walikohifadhiwa na hili hata Kagame alishalisema kuwa watawasaka kokote waliko.

Waache kuchochea machafuko kwa majirani zao kwa kisingizio cha kuhifadhi wakimbizi wa kisiasa. Hilo tu.
 
Mkuu unawezakutupa chanzo au kuweka hiyo document au ni habari za virabu vya wanzuki?maana unachokiongea ni kitu kizito kuongea bila hata ushahidi ni kuropoka au umbea!Usijidanganye nyuma ya keyboard!
Chanzo kimeshatajwa kuwa ni reuters na vile vile BBC tayari wamesharipoti
 
Mchawi ni Nkurunziza,swala la msingi ni kujiuliza chanzo cha haya yote ni nn? Na je, isingekua uchu wa madaraka haya yote yangetokea?Yale yale ya Z'bar,tunatafuta mchawi nje wakati mchawi ni wa humu humu ndani.Think
 
Na Kagame pia kung'ang'ania madaraka!, Mpaka sasa ana miaka 20 akiwa rais na anabadili katiba ili aongoze tena kwa miaka 17 ijayo.
Acha kumnyoshea kidole Kagame wa mbali angalia yanayotokea Z'bar.
 
......naona ni bora tu rwanda na burundi zikaungana na kuwa taifa moja tu!/
 
Acha kumnyoshea kidole Kagame wa mbali angalia yanayotokea Z'bar.
CHAMA KIMOJA KUNGANGANIA MADARAKA YA NCHI KIKIJIWEKEA AU KUJICHAGULIA WATU WAKE PAMOJA NA KUPINDISHA MISINGI YA DEMOKRASIA / HAITOFAUTIANI NA SANA NA AKINA KAGAME! AU MUSEVENI.
 
Nyie mnaotumia chuki zenu dhidi ya Tutsi hamjui mnachoongea. Kwa taarifa yenu adui wakubwa wa Kagame ni Tutsi wenzake. Hutu sio tatizo sana ila fellow Tutsi ndio hasa Kagame anawahofia. Hili suala la vijana 18 wa Kirundi kudai kupewa mafunzo ya kijeshi halina mantiki. Nchi haipinduliwi kirahisi namna hiyo. Vile vile huwezi iamini BBC kwa kuwa ni chombo kilichobobea kwa kupiga tarumbeta kueneza propaganda hasi dhidi ya kiongozi au uongozi wowote usiowapendeza. BBC na serikali ya uingereza hawampendi Kagame kama walivyomchukia na kujaribu kumchafua Mugabe. Tujaribu kutenganisha pumba na mchele. Suala la Rwanda si u-Tutsi au u-Hutu bali ni kushika dola. Chuki za kikabila zipo za chini chini ila adui ni wa karibu kwa Kagame zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…