Rwanda vipi tena? Hela inawaondolea heshima kiasi hiki

Rwanda vipi tena? Hela inawaondolea heshima kiasi hiki

Ofcourse madhara yapo tu siku zote, hii lazima italeta ahida hata kwa EAC yote. Ila, pesa ni pesa tu ndugu yangu
 
Atawamaliza wote.

Kagame hataki ujinga nchini kwake.
Na hio Ni guaranteed,muhalifu yoyote pale ndio amepelekwa kwny kifo mambo ya haki za binadamu aliyokua anayapata huko alikotoka asahau.

Pale Ni chuma tu kinakohoa, imeisha hio.
 
Hiki kipande ni amazing:

"Hâta ombi la kupewa ukimbizi UK likikubaliwa bado utapelekwa Rwanda na utahesabika uko UK!"

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
[emoji1][emoji1] Sasa na wanyarwanda waliokua wanakimbilia UK kwa ukimbizi wa kisiasa itatakiwa wabaki huko huko Rwanda afu watahesabika wako UK [emoji1][emoji1][emoji1] so funny.
 
A revealing of what to come.
Historia huwa inajirudia
...na sisi tuende, twende, tukubali, na kusign EPA.

Twaweza faidika, kiuhasara na uharamu.

Comrade Mkapa, Rest in Peace atleast your critical vision has averted us the foreseen. It bought us time for the unveiling, a revealing of what it may look like.

Aluta Continua.
 
Rwanda imeingia mkataba wa poundi takribani milioni 150 ili ipokee wakimbizi haramu watakaodakwa nchini UK.

Mpango aina hii muasisi ni Macron wa France. Yéyé aliingia mkataba na Libya. Pamoja na kuhamishiwa wakimbizi haramu Toka France Kwenda Libya mkataba wao pia unaitaka mamlaka ya Libya kuzuia wanapenda Libya ili waende France.
Mkataba huu umesababisha haya:

1. Kuongezeka kwa wahuni wanaosafirisha binadamu (human traffickers). Libya inalipwa kulingana na wingi wa wahamiaji haramu wanaorejeshwa Libya. Sasa kinachofanyika ni kuhakikisha wahamiaji haramu wengi wanaenda France Ili wakamatwe ili malipo yawe endelevu. Ni akili ya Biashara. Kama utalipwa kwa idadi ya mbuzi wanaokamatwa wakila mazao si utahakikisha mbuzi wengi zaidi wanakula mazao? Hutataka mbuzi waache kula mazao! Kuna Kila dalili Inasemekana mamlaka za Libya zinashiriki biashara hii. Zimefungua makambi ya kuhifadhi wakimbizi wapya na wanaodakwa France. Yaani biashara ya binadamu imefanywa halali na wanaodai wanajali haki za binadamu.

2. Libya kuna mamlaka zaidi ya 2. Japo Moja ndioo inatambuliwa na EU zote zimeona hii ni njia mojawapo ya kujipatia kipato cha kuendesha harakati.

3. Makambi yalioanzishwa kwa gharama za France yamegeuka mateso haswaa kwa watu weusi. Awali haikuruhusiwa kujenga makambi ya kuhifadhi binadamu. Sasa yanajengwa kwa héla ya France. Wati wanateswa! Hâta mtu alitaka mkazi wa ndani au kibarua anapenda "kumnunua" hapo!

4. Makambi haya yanaendeleza ubaguzi. Yapo ya wa gredi A (wahindi, waarabu, wazungu, walatino) na yapo ya gredi B (watu weusi). Yote huduma mbovu lakini ya waafrika weusi ndioo balaa haswaa. Kubakwa, kulawitiwa, kupigwa, kunyipwa chakula'). Dunia unaona lakini Iko kimya. Umoja wa Afrika unajua lakini nao haujafanya lolote la maana zaidi ya kukemea. Hakuna tena kina Nyerere, Kaunda, Mandela!

Sasa jirani na mwanachama mwenzetu wa EAC na AU kachukua héla naye apokee wakimbizi haramu Toka UK! Na huenda hatahojiwa! Hii kusema ukweli ni Biashara haramu na bidhaa ni binadamu!
Halafu mkataba huu una kipengele cha ajabu. Hâta ombi la kupewa ukimbizi UK likikubaliwa bado utapelekwa Rwanda na utahesabika uko UK!

Je sisi kama majirani wa Rwanda hatutaathirika? Fikiria mhindi wa Bangladesh aliyezamia UK aletwe Kigali? Hatatamani aende Dar au Nairobi kwenye wahindi?

Tumuulizeni Kagame kwa nini héla imemtoa utu kiasi hiki?

Hebu Fikiria kijana kutokea Pemba azamie London halafu adakwe apelekwe Rwanda? Si kichekesho? Saa ingine wazungu wanavaa suti lakini akili kolo!

Miaka 4 iliyopita Uholanzi ilianzisha mpango ukiitwa "a taxi for a returnee"! Ulianza kwa kuwalenga wazamiaji toka Ghana. Yaani Ukiwa Uholanzi ukikubali kupewa "taxi" urudishwe Ghana kuanzia biashara ya taxi ili usitamani Kwenda Uholanzi. Tukawaambia "mnajaza gunia upepo" wakadharau. Matokeo: waghana wakaambizana "twendeni uholanzi tukachukue taxi za bure". MTU anarudi Accra anaenda ubalozi wa Uholanzi anapewa taxi mpyaaa. Anampa ndugu yéyé anarudi Uholanzi au anawezesha NDUGU waende uholanzi. Waholanzi wakastuka! Wakimbizi ndioo wanamiminika tena wengine ni ambao walirudi n'a kupewa taxi. Wameanza "upyaaaaaaa" kama bwege!

Rwanda itashangaa imepokea wakenya, waganda, wazambia, warundi, wakongo, wanaija, wahindi, waarabu, n.k. Itaweza au itatusababishia matatizo EAC?

Au na Tanzania tuingie mkataba kama huu na Belgium, Canada, US na Finland ? Waletwe😄😂


CC Yahya Msangi

Kagame aangaliwe vizuri. Huyu anaweza kabisa hawa wahamiaji akawaruhusu kuingia Tanzania ili hata hela anazopewa azitumie kuwatunza afanyie mambo yake mengine.

Vyombo vya ulinzi Tanzania viwe macho na mipaka yetu yote
 
Rwanda wana akili na wanajua ni wapi watakapowatupa hao wakimbizi, ni huko Nyarugusu Kigoma Tanzania.
1st time wkt wanasema watawapokea wakimbizi kutoka Libya,Sudan na nchi nyinginezo pale Rwanda then mchakato wa kuwapeleka ulaya utaanzia Rwanda kelele zilipigwa za kutosha Kwamba Nchi jirani zitapewa huo mzigo wa wakimbizi lkn mpk Sasa zaidi ya miaka kadhaa Sasa hakuna hata mkimbizi mmoja wa kutoka huko Libya,Sudan etc aliyekutwa amevuka Boda kuingia nchi yoyote Ile ya E/Africa.
 
Denmark nao soon watasaini deal la aina hio na Rwanda.

Ikienda hivyo kwa miaka 20 watakunja hela za mabeberu mfukoni halafu ndani ya nchi watakua mchanganyiko mbalimbali wa makabila/races.
 
UK Refugee Council wamesema Hilo deal litaweza kuwagharimu walipa Kodi wa uingereza £1.4bil kwa mwaka,huku wakisema hio £150mil zitakazotolewa Ni kianzio kwa ajili ya majaribio ya project hio kwa serikali ya Rwanda.
 
Kagame aangaliwe vizuri. Huyu anaweza kabisa hawa wahamiaji akawaruhuru kuingia Tanzania ili hata hela anazopewa azitumie kuwatunza afanyie mambo yake mengine.

Vyombo vya ulinzi Tanzania viwe macho na mipaka yetu yote
Nasisi tulivyowazembe wanaweza kuingia kweli Tz
 
PAKA kwake pesa ni muhimu bila kujali inatoka wapi hata kwa shetani
 
Denmark nao soon watasaini deal la aina hio na Rwanda.

Ikienda hivyo kwa miaka 20 watakunja hela za mabeberu mfukoni halafu ndani ya nchi watakua mchanganyiko mbalimbali wa makabila/races.
Na nchi ndio itaendelea..kama ilivyo usa...karibisha wageni watumie..sio wadanganyika tumejifungia hatutaki exposure.

#MaendeleoHayanaChama
 
Na nchi ndio itaendelea..kama ilivyo usa...karibisha wageni watumie..sio wadanganyika tumejifungia hatutaki exposure.

#MaendeleoHayanaChama
Unamaanisha wakienda Rwanda watatumikishwa kama watumwa Kwa maendeleo ya Rwanda?
 
Back
Top Bottom