Rwanda wamedhibiti Uhalifu 95% kwa mtutu

ili kupata usalama lazima nchi iwe kama ipo kwenye hali ya dharura. Ukilegezalegeza nchi inaanguka mikononi mwa wahalifu.
 
Usalama Kwanza. Demokrasia baadae
 
Umeongea ukweli mtupu
Kuna majinga yanatumia udogo kama kigezo
 
Hahahahahahahaha kumbe! Kwa hiyo,unatamani yale maisha?! Labda kesi za fulani kapotelea kusikojulikana,hapo sawa. Ukisikia mtu wako kakamatwa,ujue wana taarifa za uhakika 98%. Sasa labda majambazi ndo hawapo.
Lakini,
-ukae na flat ndani? Hiyo si yako bro.
-uache nguo nje uingie ndani? Hizo achia wenyewe wachukue.
-eti unaosha vyombo uache nje uingie ndani? Hivyo vya kwako.
-vichocholoni kupolwa simu na mikoba kwa akina mama,ni vya kufikia.

Uje ukae hata wiki nadhani utarudi na majibu sahihi.
Kwani hao wanajeshi wanaopatrol,uliwahi waona wakikimbiza kibaka? Kwa kifupi jeshi lipo vizuri kwenye majukumu yake, Polisi bado.

Ungesema tu ukiamua kuripoti na kufatilia, hazipiti siku 3 hata kama ni sahani utaipata
 
Ni vigezo gani unatamani Rwanda na Tanzania zifanane? Historia zinafanana?
 
Umenena. Polisi kule anajua akichafua tu,familia yake inaenda kuteseka mazima. Si kwamba wahalifu hawapo,lakini wao wanatumia akili nyingi kuliko unavyofikilia.

Hivi mfano, chukulia mtu kaua watu zaidi ya 20. Unamchukuliaje katika jamii kama si kumfatilia kwa karibu na ukali? Sasa fikilia uwe na watu zaidi ya 700,000!!! Hapo hapo, una watu kama Milioni 3 au zaidi,wenye kinyongo na hao 700,000 na familia zao! Wewe ukipewa kuongoza watu hao utafanyaje!!!
 
Hatuhitaji kujilinganisha na Rwanda! Ni serikali kutojisahau tu.
Mbona wakati wa utawala wa hayati Magufuri hatukusikia si cha majambazi au panyaroad!
Uharifu angala kwa 90 % ulidhibitiwa!
Pia ni kuangalia kama kuna uwezekano wa kurudisha na kuimarisha ulinzi shirikishi mf.enzi zile ambazo vikundi vya Sungusungu vilianzishwa, hivi vilisaidia kukomesha uharifu kiasi fulani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…